G.MWAKASEGE
Senior Member
- Jun 29, 2007
- 153
- 15
Wafanyabiashara wadai ziara imewaathiri kiuchumi
*Mkurugenzi awaomba radhi akisema makosa yake
Na Rashid Mkwinda, Mbeya
UJIO wa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowasa mkoani hapa, umeendelea kugubikwa na utusitusi, baada ya gari la matangazo linalotumika kutangaza ujio huo kuzomewa katika maeneo ya Mafiat, Stereo na Mwanjelwa, ambako wafanyabiashara wamevunjiwa maeneo yao.
Hatua hiyo ya kuzomea gari hilo imekuja siku moja baada ya wafanyabiashara hao kutamka wazi kuwa hawako tayari kumpokea Waziri Mkuu kutokana na Halmashauri ya Jiji kutumia ziara hiyo kuwakomoa wafanyabishara kwa kuharibu miundombinu ya biashara zao.
''Ondokeni hapa...ondoeni kelele zenu, hatuna haja ya Waziri Mkuu sisi, yeye ndiye aliyesababisha sisi kuvunjiwa biashara zetu hatunufaiki chochote na kuja kwake,'' alisikika mmoja wa wafanyabiashara walioathirika na bomoabomoa ya Jiji.
Akizungumza katika kikao maalumu na waandishi wa habari waliofuatilia hatua hiyo kwa karibu, Meya wa Jiji la Mbeya, Bw. Athanas Kapunga, alikiri udhaifu juu ya utekelezaji wa hatua hiyo ambayo imetoa picha na mtazamo mbaya kwa mkoa na Taifa.
Alisema uendeshaji wake uliowakumba pia wauza magazeti, ulikuwa na makosa kutokana na ukweli, kwamba baadhi ya wafanyabiashara na wauza magazeti waliidhinishwa na halmashauri, kuweka vibanda vya aina moja ambavyo viliwekwa namba.
Bw. Kapunga alisema yeye akiwa Meya, atafuatilia kwa kina uendeshaji wa bomoabomoa kwa kuwasiliana na Mkurugenzi wa Jiji, ili haki itendeke na kuboresha uhusiano baina ya wananchi na Jiji.
''Nachukua fursa hii kuwaomba radhi wale ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika, ilmradi walikuwa wamefuata taratibu za kisheria katika uendeshaji wa biashara zao,'' alisema Bw. Kapunga.
Hata hivyo, Bw. Kapunga alisema machakato wa uendeshaji wa bomoabomoa hiyo ulitokana na maagizo ya Waziri Mkuu kuboresha usafi wa miji na kwamba ilichelewa kufanyika katika Jiji la Mbeya kutokana na kukosekana kwa fedha za kulitekeleza.
''Waziri Mkuu aliagiza miji ilirudi katika hali yake...sisi tumekuja nyuma katika utekelezaji wa maagizo ya Waziri, wenzetu walianza siku nyingi nadhani mmeona majiji mengine na mmesikia katika vyombo vya habari utekelezaji wake katika miji mingine,'' alisema.
Aidha, Bw. Kapunga alisema utekelezaji ulikuwa mkali kiasi cha kuathiri waliokuwamo na wasiokuwamo na kwamba fursa hiyo ya utekelezaji imepokewa kwa hisia tofauti na wananchi wakihusisha bomoabomoa na ujio wa Waziri Mkuu.
Awali Mkurugenzi wa Jiji, Bibi Elizabeth Munuo, ambaye siku mbili zilizopita aliwakwepa waandishi wa habari na baadaye kuzima simu yake ya mkononi na kupatikana jana baada ya kupigiwa, alidai kuwa yeye yuko katika operesheni usafi wa Jiji kwa ajili ya Waziri Mkuu.
Bibi Munuo aliwambia waandishi kwa njia ya simu, kuwa wanaweza kumwona Meya kwa ufafanuzi, kwa kuwa yeye anaendelea na usafi wa Jiji kwa ajili ya ujio wa Waziri Mkuu anayetarajia kuanza ziara yake hapa leo.
Matangazo yaliyosikika yakitolewa kupitia gari la matangazo kuhusu ujio wa Waziri Mkuu yaliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo wa juu serikalini, lakini baadhi ya wananchi walidai kuwa hawawezi kumpokea kutokana na ujio wake kuathiri uchumi wao, kwa Serikali kuwabomolea maeneo ya biashara zao.