Gari la matangazo ya Ujio wa Lowassa Mbeya lazomewa

G.MWAKASEGE

Senior Member
Jun 29, 2007
153
15
Wafanyabiashara wadai ziara imewaathiri kiuchumi
*Mkurugenzi awaomba radhi akisema makosa yake

Na Rashid Mkwinda, Mbeya

UJIO wa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowasa mkoani hapa, umeendelea kugubikwa na utusitusi, baada ya gari la matangazo linalotumika kutangaza ujio huo kuzomewa katika maeneo ya Mafiat, Stereo na Mwanjelwa, ambako wafanyabiashara wamevunjiwa maeneo yao.

Hatua hiyo ya kuzomea gari hilo imekuja siku moja baada ya wafanyabiashara hao kutamka wazi kuwa hawako tayari kumpokea Waziri Mkuu kutokana na Halmashauri ya Jiji kutumia ziara hiyo kuwakomoa wafanyabishara kwa kuharibu miundombinu ya biashara zao.

''Ondokeni hapa...ondoeni kelele zenu, hatuna haja ya Waziri Mkuu sisi, yeye ndiye aliyesababisha sisi kuvunjiwa biashara zetu hatunufaiki chochote na kuja kwake,'' alisikika mmoja wa wafanyabiashara walioathirika na bomoabomoa ya Jiji.

Akizungumza katika kikao maalumu na waandishi wa habari waliofuatilia hatua hiyo kwa karibu, Meya wa Jiji la Mbeya, Bw. Athanas Kapunga, alikiri udhaifu juu ya utekelezaji wa hatua hiyo ambayo imetoa picha na mtazamo mbaya kwa mkoa na Taifa.

Alisema uendeshaji wake uliowakumba pia wauza magazeti, ulikuwa na makosa kutokana na ukweli, kwamba baadhi ya wafanyabiashara na wauza magazeti waliidhinishwa na halmashauri, kuweka vibanda vya aina moja ambavyo viliwekwa namba.

Bw. Kapunga alisema yeye akiwa Meya, atafuatilia kwa kina uendeshaji wa bomoabomoa kwa kuwasiliana na Mkurugenzi wa Jiji, ili haki itendeke na kuboresha uhusiano baina ya wananchi na Jiji.

''Nachukua fursa hii kuwaomba radhi wale ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika, ilmradi walikuwa wamefuata taratibu za kisheria katika uendeshaji wa biashara zao,'' alisema Bw. Kapunga.

Hata hivyo, Bw. Kapunga alisema machakato wa uendeshaji wa bomoabomoa hiyo ulitokana na maagizo ya Waziri Mkuu kuboresha usafi wa miji na kwamba ilichelewa kufanyika katika Jiji la Mbeya kutokana na kukosekana kwa fedha za kulitekeleza.

''Waziri Mkuu aliagiza miji ilirudi katika hali yake...sisi tumekuja nyuma katika utekelezaji wa maagizo ya Waziri, wenzetu walianza siku nyingi nadhani mmeona majiji mengine na mmesikia katika vyombo vya habari utekelezaji wake katika miji mingine,'' alisema.

Aidha, Bw. Kapunga alisema utekelezaji ulikuwa mkali kiasi cha kuathiri waliokuwamo na wasiokuwamo na kwamba fursa hiyo ya utekelezaji imepokewa kwa hisia tofauti na wananchi wakihusisha bomoabomoa na ujio wa Waziri Mkuu.

Awali Mkurugenzi wa Jiji, Bibi Elizabeth Munuo, ambaye siku mbili zilizopita aliwakwepa waandishi wa habari na baadaye kuzima simu yake ya mkononi na kupatikana jana baada ya kupigiwa, alidai kuwa yeye yuko katika operesheni usafi wa Jiji kwa ajili ya Waziri Mkuu.

Bibi Munuo aliwambia waandishi kwa njia ya simu, kuwa wanaweza kumwona Meya kwa ufafanuzi, kwa kuwa yeye anaendelea na usafi wa Jiji kwa ajili ya ujio wa Waziri Mkuu anayetarajia kuanza ziara yake hapa leo.

Matangazo yaliyosikika yakitolewa kupitia gari la matangazo kuhusu ujio wa Waziri Mkuu yaliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo wa juu serikalini, lakini baadhi ya wananchi walidai kuwa hawawezi kumpokea kutokana na ujio wake kuathiri uchumi wao, kwa Serikali kuwabomolea maeneo ya biashara zao.
 
Rashid Mkwinda said:
''Ondokeni hapa...ondoeni kelele zenu, hatuna haja ya Waziri Mkuu sisi, yeye ndiye aliyesababisha sisi kuvunjiwa biashara zetu hatunufaiki chochote na kuja kwake,'' alisikika mmoja wa wafanyabiashara walioathirika na bomoabomoa ya Jiji.

Hapa ndipo awamu ya nne imetufikisha, Waziri mkuu ambaye ndio mtendaji wa Serikali kwa Ubeberu wake anaouonyesha bungeni anataka kupeleka kwa wananchi lakini hivi sasa amekutana na kisiki. Wale ambao wanamuhakikishia kula chakula chake vizuri (Utakumbuka jinsi alivyokataa kuongelea swala la wanafunzi waliokuwa wanapigwa na baridi nje ya ofisi za kibalozi (UK) kule Ukraine) alisema anakula. Sasa wananchi walalahoi wanayempa hiyo kula hawataki mchezo na angefanya jambo la maana kung'atuka wakati muda bado upo ingawa halipo katika kamusi yake.
 
Naam
hatimaye haya sasa ni mapambazuko ya kifikra.Hii ni ishara tosha kabisa kuwa sasa hii awamu ya nne inaelekea mwisho kabisa wa patience kutoka kwa wananchi.Walizoea sana kuburuza watu hatimaye waburuzwaji wanaanza kuamka.Naye Muungwana ndo anazidi kuchanja mbuga tu kuelekea nchi za watu ambao wanajua nini maana , ya kujienga nchi na utawala bora usiokumbatia rushwa na ufisadi.Anawaachia nchi wenzake hali yeye anakwepa majukumu yake.Lakini hii ni logical and unavodable consequence ya serikali ya kishkaji na kuhi kabsa.Pole EL kwa yatakayokukuta Mbeya.Juzi tu Mwanza DC alikutunishia kifua na yule mtoto wa Ukerewe akakutwanga swali ambalo mpaka leo majibu huna...pole sana Mzee...
 
Naam
hatimaye haya sasa ni mapambazuko ya kifikra.Hii ni ishara tosha kabisa kuwa sasa hii awamu ya nne inaelekea mwisho kabisa wa patience kutoka kwa wananchi.Walizoea sana kuburuza watu hatimaye waburuzwaji wanaanza kuamka.Naye Muungwana ndo anazidi kuchanja mbuga tu kuelekea nchi za watu ambao wanajua nini maana , ya kujienga nchi na utawala bora usiokumbatia rushwa na ufisadi.Anawaachia nchi wenzake hali yeye anakwepa majukumu yake.Lakini hii ni logical and unavodable consequence ya serikali ya kishkaji na kuhi kabsa.Pole EL kwa yatakayokukuta Mbeya.Juzi tu Mwanza DC alikutunishia kifua na yule mtoto wa Ukerewe akakutwanga swali ambalo mpaka leo majibu huna...pole sana Mzee...

Msijali atapata watu, kwani wanaweza kuwa na mpango wa Kwenda Na Ze Comedy wakawaongezee nguvu wana TOT.
 
''Ondokeni hapa...ondoeni kelele zenu, hatuna haja ya Waziri Mkuu sisi, yeye ndiye aliyesababisha sisi kuvunjiwa biashara zetu hatunufaiki chochote na kuja kwake,'' alisikika mmoja wa wafanyabiashara walioathirika na bomoabomoa ya Jiji.

Sasa kama watu wanazomea gari tu la matangazo kabla mkuu hajafika Mbeya, itakuwaje jamaa akifika? Atahutubia kweli? Ama ndio jamaa wataweka washangiliaji wa kukodi. Au watawatumia Fungua Fanta Unywe kudhibiti wazomeaji! Maana kwa jinsi ninavyozifahamu siasa za Mbeya nina shaka na hili.
Yangu masikio.

Mushobozi na wana JF wengine kama mpo Mbeya tunaomba taarifa rasmi za ziara ya EL.
 
Wanasema ni rahisi sana kuchezea korodani za Simba wakati amelala.Lakini pindi aamkapo huwezi kumchezea chezea na yeye anakuangalia tu ..hapo utegemee kifo au majeraha makubwa!!.
Poleni CCM kwa yanayowapata.
Wembe
 
Wembe mkali waonekana kutumia maneno mazito mno!!!!!!!!!!!!!
Ulimwengu alisema angalia sana upole wa mtanzania ambaye ukimkanyaga anaomba msamaha kwa kuweka mguu wake chini ya mguu wako.
Watanzania tumekukwa dormant mno kwa kipindi kirefu kuhusu masuala yanayohusu maslai ya nchi kwa ujumla labda kwa kuwa tulimuamini Mwalimu Jk na tukauendeleza uaminifu ule ule kwa viongozi wa sasa kumbe sivyo.
We have now seen the light we need to stand up for our right my fellow Tanznians
 
Wanasema ni rahisi sana kuchezea korodani za Simba wakati amelala.Lakini pindi aamkapo huwezi kumchezea chezea na yeye anakuangalia tu ..hapo utegemee kifo au majeraha makubwa!!.
Poleni CCM kwa yanayowapata.
Wembe

Wembemakali,leo nimetambua nini maana halisi ya jina lako,maana
umenivunja mbavu.Sasa simba kaamka,EL na ccm yake wana kazi kweli kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Huko Mbeya anajitakia Aibu, maana kule kanda ya ziwa walizomewa wabunge, sasa huko Mbeya yawezekana ikawa zamu yake, ama akazomewa, au asipate watu wa kutosha kwenye mikutano yake labda wawatoe Iringa au wakodi washangiliaji kama kawaida yao.

Ngoja tusikie
 
EL kichwa nyinyi.....ataenda na washangiriaji wa kukodi! unafikiria atakubali aibu kama ile ya mawaziri wake imkute!!! huyo atakuwa sie EL nnaemjua mie
 
mwakasege, nilishaanzisha thread ya mapokezi yake na hotuba yake, ila sasa ngoja nikaihamishie hapa. maana hii nilikuwa sijaiona.
 
heshima yenu wakuu.

jana ilikuwa siku ya kuanza ziara ya lowasa hapa Mbeya itakayochukua siku nane kikazi. pia ni siku ya huzuni kwake maana kama WAANDISHI huandika habari za kila mkoa vizuri, basi hamna mkoa ambao uliwahi tia fora kama huu mkoa wa Wanyakyusa, Wasafa, Wamalila, Wanyiha ambao ni wenyeji.

kabla ya ndege yake kutua katika ardhi hii, watu walisikika wakidai kuwa hawangeenda kumpokea maana serikali yake haifai.

mida ya saa 6 mchana, ndege yake iliwasiri katika Uwanja ule mbovu wa Somora Machehe; ukiwa na wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wenye uniform, scout, watu wenye jezi za kijani, na watu wenye vitambi. idadi ilikuwa ndogo sana kulingana na uwiano wa watu wa Mbeya. watu wengine walikuwa kandokando mwa barabara huku wakijaribu kujenga hoja za hapa na pale. hata mimi nilikuwepo.

mida ya saa 10 ndipo hotuba ya Lowasa ilipoanza kwa maswali kutoka kwa wananchi.

viongozi waliojaribu kujibu maswali huku wakiwa wanazomewa ni Chenge, mkuu wa mkoa, Meya wa jiji, Naibu waziri wa elimu nk, huku Lowasa akilazimika kutoa ufafanuzi kwa kiongozi.

Baadaye, Lowasa alianza hotuba iliyojaa utetezi wa Karamagi kuwa mkataba aliousahini ni bora kuliko mkataba wowote ule Tz na kwamba hauna tatizo lolote kisheria.

Akadai kuwa cement imepanda bei kwa sababu Afrika Kusini wananunua kwa wingi ili kujengea viwanja vya mpira wa kombe la Dunia, n.k

Pale uwanjani, Lowasa hakuzomewa sana kwa sabau zifuatazo.

1. kama mnavyojua, Lowasa ni msanii. alinza kwa kuuliza maswali ili apate cha kuongelea. mimi nilidhani hotuba inabidi ianze ili watu waulize pale ambapo hawakuelewa.

2.alikuwa anakatakata hoja. mfano, pale anaposema "karamagi hakufanya kosa:.......ghafla anasema .Mbeya oye....na kuingiza hoja nyingine kabla watu hawajatulia.

3.Tofauti na Wasira, uwanja huu ulikuwa umesheheni watu wengi, ingawa hawakukaribia wa Zitto. ila pia niliona magari aina ya Kenta pale uwanjani, idadi inazidi 10, na nikafikiri kuwa labda kwa sababu Mkutano ni wa kimkoa, yawezekana magari hayo yalisomba watu toka wilaya tofauti, ili waonekane wengi. pia ulijaa wanafunzi.

4. sababu, wengi waliokuwa karibu na jukwaa walikuwa na jezi za kijani, na ndio waliokuwa wanauliza maswali, basi inawezekana maswali yaliandaliwa ili kuondoa sumu iliobaki kipindi cha wasira, na hivyo maswali yenyewe hayakuwa na msisimko, waliouliza maswali ni sanasana wanafunzi wa sekondari.

5.labda kwa sababu Mwandosya, ambaye Mkoani hapa anaonekana kama sio mwanamtandao alikuwepo, na alikuwa hakuvaa Uniform za sisiem basi watu waliridhika kumwona. maana watu wa hapa wako tayari kumwaga damu ilimradi tu waone haki ikitendeka. mfano ni kile ninachosadikika kwa Akukweti, baada ya kuwaambia kuwa vibanda vyao vya mwanjelwa vilistahili kuungua sababu vilikuwa vinatia kinyaa mipanga ya serikali. siku hiyohiyo anapanda ndege hakuvuka hata km. 1; na pia woga wa kikwete kuja huku Mbeya, maana hata yeye walishamwambia akikanyaga hapa atakiona.

Baada ya mkutano;

wakati wageni wanaondoka, watu walisubiri uwanjani na kuanza kumshangilia Mwandosya. na wachache tu kuzomea lowasa na mkuu wa mkoa. ieleweke kuwa mkuu wa mkoa ni Mwakipesile, ambaye ni mzaliwa wa mkoa huu, na kipenzi cha muungwana au Kingwendu kama ajulikanavyo huku.

lakini Mwakipesile hapendwi kabisa, na aliwekwa huku ili kuondoa mbegu zote za wasio wanamtandao, akiwemo Mwandosya. pia anadistribute unequally, lasrimali za mkoa kwa sehemu zenye upinzani na zisizo na upinzani. sehemu zenye upinzani ni pamoja na Tukuyu, Kyela na Mbeya Mjini, wakati zenye unafuu ni mwambao wa Mbozi nk.

Mwanjelwa ndipo watu walipojipanga mstari kumzomea. ilikuwa hatari. ilibidi nipaki usafiri wangi mbali maana nilidhani kuna watu watasombwa na FFU, au kama wakati wa Lurdism, vijana wanaweza kuanza kuponda mawe na kuharibu kila kitu chenye thamani wakidhania kila mwenye gari ni miongoni mwa wale wale mafisadi.

Walianza kudai. hoo.hooo.., *******, shenzi, haya ndiyo maisha bora? viwanja vya kujenga vinapanda bei, sement inapanda bei, mnatuvunjia vibanda vyetu, alafu eti maisha bora, . tunamtaka kikwete aje hapa, kwa nini anaogopa. hu........nenda bwana hatukutaki......

walikuwa na miti, mawe, fimbo . utadhani kuna mtu alikuwa anawaratibu . kama kweli vyombo vya habari huwa vinaripoti, basi Tz nzima haijawahi tokea. niliogopa, nikamhurumia lowasa, nikasema laiti hasingeingia siasa.

unajua, mwanzoni wakati wanaanza kumzomea, lowasa hakujua, alitoa mkono kwenya dirisha kuwapungia, ndipo ghafla akaurudisha na kuangalia chini baada ya kuona mambo sio kawaida.

Maoni ya watu; nilijaribu kuuliza kwa nini hawakwenda kumzomea palepele uwanjani,

wakasema kuwa kulikuwepo na mpango wa askari kuwapiga na kuwakamata kama kisasi kwa Wasira iwapo zomeazomea ingetokea hapo uwanjani. pia walisema wanamtaka rais, kwa nini hataki kuja huku Mbeya. anaona Mbeya ni mbali kuliko marekani na ufaransa? eti tangu apate urais hajawahi kuja mbeya, kila kitu alichokiandaa Mkapa hakijakamilika kama vile Uwanja wa Ndege wa Songe ambao ni wa kimataifa, anachokifanya ni kugawagawa mkoa tu.

wanasema walibeba mawe na miti ili FFu wakitaka kuwashambulia basi vita ianze.

Ikumbukwe pia kuwa wakati wa ziara ya wasira, ilibidi akatishe ziara ya kutembelea Tukuyu na Kyella baada ya zomea zomea aliyoipata Mbeya mjini. sasa sijui na Lowasa ataikatisha au la. maana alipokuwa akisema .'Mbeya hoyeeee' walikuwa wanaitikia wachache. ila akisema 'SISIEM oyeeeeee' minung'uniko kutoka kwa watu inasema 'hapo ndipo anapoharibu kabisa'

Mh..... siasa za Mbeya we ziache zilivyo. unaweza andika siku nzima.

mimi ninatarajia kuanza safari ya kurudi Dar. wakati wowote, ila kitakachotokea wakati bado nipo nitawakujulisheni
 
Naona EL ameamua kuyaweka wazi zaidi baada ya kukiri kwamba Mkataba wa Buzwagi ni bora zaidi kuliko iliyopita. Pia ulikuwa na baraka za JK ... swali la msingi, je hata kile kipengere kilichopigwa mkasi kwa wino wakati wa kusaini nacho kina baraka za JK? Hapo ndipo ninapoona kiini macho cha JK na wanamtandao wake akina EL, RA na Karamagi. Yaani hapa ni kutetea uozo kwa nguvu zote ili mradi tu mtandao uendelee kuitafuna nchi. Halafu anasema bure ilikwisha wakati wao wanaongoza kwenye ufisadi na kutafuna mali ambazo wanazipata kwa njia za panya. Ukiwahoji unaambiwa lete ushahidi! Kweli Tanzania tumeliwa haswa!
 
ndio maana wametumia njia ya kwenda na Prof Mwandosya at least kupuinguza makali ya wananchi wa Mbeya,
 
unajua aliposimama kuongea, waziri mkuu hakushangiliwa zaidi kwenye mkutano, ila aliposimama Mwandosya, duh.. watu walishangilia kama kwamba hawana akili nzuri.
 
unajua aliposimama kuongea, waziri mkuu hakushangiliwa zaidi kwenye mkutano, ila aliposimama Mwandosya, duh.. watu walishangilia kama kwamba hawana akili nzuri.

Alijisikiaje au alikuwa ameinama chini?
 
Back
Top Bottom