Gari la kubeba takataka laua: Kwa nini tunawatumia wakandarasi 'poa'? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la kubeba takataka laua: Kwa nini tunawatumia wakandarasi 'poa'?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shadow, Feb 15, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Jamani,

  Nimesoma na kuona picha ya ajali ya bajaji na gari taka iliyotokea siku ya wapendao na kuua mama na mtoto wake wa miaka mitatu( viewer discretion is advised as the photos are not in a good state)Global Publishers - Picha

  Jamani kwa nini manispaa zetu zinaruhusu na kupitisha kandarasi hizi kwa watu wenye magari ambayo si magari bali taka kubeba takataka jijini? Jamani hizi si ndio ufisadi wenyewe huu. Mkandarasi hana hata uwezo wa kuagiza gari la mtumba, anafufua lori la mwaka sabini na kuanza kulitembeza barabarani. Dar es salaam inaongoza kwa haya matakataka gari. Hayana break na hata sura yake ukiiona zaidi ya kuwekewa 'mkorogo' halifai hata kutembezwa kwenye barabara zetu.

  Suluhisho: Idara ya usalama barabani inabidi ibadilishwe na kuleta wanausalama wanaojali utawala wa sheria.

  Pili, kuna hili suala la manispaa zetu kutangaza zabuni na kuchagua wakandarasi uchwara, nafikiri inabidi kuwepo na usimamizi wa kudondokea (spill over supervision) kutoka takukuru, police na wale watu wa Procurement Authority hili kukwepa dhaama za hawa mabazazi wanaopitisha tenda kwa njia za ajabu ajabu.

  Hitimisho: Hili suala limetokea nje ya ofisi za Halmashauri ya manispaa Kinondoni na mpaka sasa hakuna tamko lolote linalomhusu mkandarasi wao.

  Mwisho, serikali kuruhusu bajaji na pikipiki bila kuratibu hao watu wanaokaa nyuma ya vyombo hivyo (madereva) naona ni kama utambi wa bomu umeanza kuungua.
   
 2. J

  Japhet Member

  #2
  Feb 16, 2009
  Joined: Jan 26, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magari hayo-TAKA yameishalalamikiwa sana kwa kuhatarisha usalama barabarani. Magari yenyewe hayana break, taa, reflector n.k. Lakini trafiki wamekuwa wakifumbia macho malalamiko ya wananchi. Mpaka ajali zitokee, ndio matrafiki wanawajibika.....
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Japhet, hapo umenena kweli. Kuna hii kasumba iliyojengeka hasa Dar Es Salaam, kuruhusu hiyo migari 'taka' ambayo yenyewe ni taka fayaa kutupwa. Gari la kubeba taka si lazima na lenyewe liwe taka. Utawala wa sheria ulishakufa huko bongo. Yani madiwani wanakaa kama kamati na kupisha tenda ya mtu aliyeokota gari jalalani manake alifahi kutembea. Trafiki naye anaruhusu kwamba linaweza kubeba uchafu bila hata ya kuangalia kama ni salama kutembea barabarani, TRA naye analikatia kodi.

  Mungu awarehemu hao waaanga wa gari taka.
   
Loading...