Gari la askari polisi lakamatwa na nyara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la askari polisi lakamatwa na nyara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Michael Amon, Jul 19, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  POLISI katika mji mdogo wa Himo, mkoani Kilimanjaro, wamefanikiwa kulikamata gari aina ya Toyota Noah, linalomikiwa na askari mmoja wa polisi likiwa na shehena ya pembe za ndovu.

  Taarifa za uhakika zilizopatikana jana, zilisema gari hilo linalomilikiwa na askari polisi mwenye cheo cha koplo lilikamatwa saa 2:00 asubuhi nje kidogo ya mji wa Himo.

  Ofisa mmoja mwandamizi wa polisi, alisema kuwa gari hilo lililokuwa na abiria 10, liliondoka katika mji mdogo wa Tarakea wilayani Rombo, kwenda mjini Moshi.

  Alisema baaada ya kufika eneo hilo, lilisimamishwa na polisi wa kikosi cha kudhibiti magendo wakishirikiana na trafiki na lilipopekuliwa lilikutwa na vipusa hivyo.

  “Hizo pembe zilikuwa kwenye mifuko ya kuhifadhidia mboea, hivi tunavyozungumza gari limeletwa hapa kituo cha kati cha polisi na abiria waliokuwa katika gari hilo wanahojiwa,”alisema.

  Wilaya ya Rombo inapakana na Hifadhi ya Taifa ya Tsavo, nchini Kenya na haikufahamika kama nyara hizo za Serikali zilitokea huko au katika hifadhi ya jirani ya Amboseli nayo ya Kenya.

  Hata hivyo wakati gari hilo likikamatwa, polisi huyo anayefanya kazi katika Kituo cha Polisi cha Tarakea, hakuwamo katika gari hilo lakini baada ya kuarifiwa alitoa ushirikiano kwa polisi.

  Taarifa nyingine zilisema awali polisi walikuwa wamedokezwa kuwa gari hilo lilikuwa libebe waharamiaji haramu kutoka nchini Somalia, lakini hadi kufika subuhi mtego haukufanikiwa.

  Kamanda wa Polisi mkoani ilimanjaro, Robert Boaz, alikiri kuwapo kwa tukio hilo lakini akaahidi kulitolea ufafanuzi kwa njia ya ujumbe mfupi (sms) kwa vile alikuwa ziarani.

  “Hilo tukio lipo lakini kwa sasa niko kwenye msafara ngoja nikuandikie kwa meseji” alisema Kamanda Boaz .
   
 2. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hiyo ndio kazi wanayoiweza
   
 3. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hawakutoa kitu kikubwa
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hili litaishia humu humu JF!


  Na lazima ndiyo kazi ya hiyo gari!

  Serikali DHAIFU ndiyo matunda yake hayo!
   
 5. Collins

  Collins Senior Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aaah ndo zao hao
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Sitashangaa wakisema "walikuwa wamekamata watuhumiwa"
   
 7. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,476
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  .


  Ni rahisi kusema hivo lakini ni vigumu sana kuamini hivyo.
   
 8. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mbona ndiyo magari maalaumu ya bidhaa za aina hizo??? Inaelekea walidhulumiana ndiyo maana wamefanyiziana.
   
 9. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Inawezekana abiria mmoja alikuwa na mzigo huo,,dereva wala mwenye gari(Koplo) hajui lolote. Sheria za mali asili hivi sasa zikoje wakuu inapotokea gari kukutwa imebeba/safirisha Nyara?
   
 10. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kumbe ndio kamchezo kao eee?
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  The difference is the same!!!!!!
   
 12. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Reverse angle, polisi na wizi tena? aibu lakini ndo walivyoandaliwa.
   
 13. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  tatizo sio polisi ila ni mfumo mbovu wa ajira za polisi, wengi wanaopata kazi haitokani na elimu au uwezo wao isipokuwa ni wale watoto watukutu wa waheshimiwa.
   
 14. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,478
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Kwa ninavyojua mshahara wa polisi na gharama za maisha zilivyo huwezi kununua Noah, hapa tukichunguza kwa makini utakuta huyo pilisi ni muharifu sugu na anafanya uharifu zaidi ya huo, cha muhimu hapa ni kusafisha jeshi la polisi kuanzia IGP na wengineo ambao hawana uadilifu wala maadili ya kazi. Lakini kama serikali ni dhaifu hilo haliwezi kutekelezeka kwani sasa hivi katika nchi hii tunaishi kikambale ajulikani baba, Mama wala mtoto ni nani.
   
 15. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,476
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180

  Lakini yana mwisho.
   
Loading...