Gari Kutetemeka (Vibrate)

benja

JF-Expert Member
May 10, 2011
318
196
Wadau nina gari langu Toyota Starlet Carat. Tatizo ni kwamba nikiwasa linatetemeka (vibrate). Mounting za Engine ziko vizuri.

Je, tatizo itakuwa ni nini?
 
Inawezekana tatizo likawa kwenye plug au coil, tafuta fundi wa umeme akuangalizie, ila hata ww mwenyewe unaweza angalia kama ukiwa mtundu wa magari
 
Ukishajiridhisha kama engine mounting zote ziko sawa, basi washa gari, akisha anza kuchomoa Coil moja baada ya nyengine, ukiona umechomoa coil akisha hakuna mabadiliko yoyote kwenye engine ujue hio coil imekwisha habari yake. Ukiona imebadilika basi endelea. Na ukigundua zote zipo sawa, anza kutizama plug nazo, kama zipo sawa, anza kuchomoa connection ya fuel injection moja moja kama vile coil ukiona hakuna mabadiliko engine kunguruma ujue hapo pana fitna.
 
Mkuu nimekuelewa sana nitakupa mrejesho. Thanks
 
Linavibrate hasa nikibadilisha gia (kwa sababu ni Manual) kwahiyo ile mda gia inatake motion unasikia mtetemo haswa na pia likiwa silence unasikia mlio ambao hata masikio yanataka kuziba hivi
Okay nenda kwa mafundi waambie wakuchekie hilo tatizo
 
Linavibrate hasa nikibadilisha gia (kwa sababu ni Manual) kwahiyo ile mda gia inatake motion unasikia mtetemo haswa na pia likiwa silence unasikia mlio ambao hata masikio yanataka kuziba hivi
Ni either gearbox mounting au bolt kwenye gearbox imekatika
 
Ukishajiridhisha kama engine mounting zote ziko sawa, basi washa gari, akisha anza kuchomoa Coil moja baada ya nyengine, ukiona umechomoa coil akisha hakuna mabadiliko yoyote kwenye engine ujue hio coil imekwisha habari yake. Ukiona imebadilika basi endelea. Na ukigundua zote zipo sawa, anza kutizama plug nazo, kama zipo sawa, anza kuchomoa connection ya fuel injection moja moja kama vile coil ukiona hakuna mabadiliko engine kunguruma ujue hapo pana fitna.
Mkuu wewe ni fundi?
 
Mkuu wewe ni fundi?
Sio fundi mkuu, ila kawaida yangu ni kupenda kujifunza. Nikipeleka chombo kwa fundi garage huwa nnauliza maswali mengi na huwa namtizama mwanzo mwisho anavofanya ufundi. Vile vile nafanya research yangu kwenye mitandao. Kusudi ili gari ikipatwa na tatizo najua nini nimwambi fundi na nakuwa nshajua anatakiwa aanzie wapi. mafundi wenyewe si unawajua walivo tena....
 
Back
Top Bottom