Gari inauzwa, iko kwenye hali nzuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari inauzwa, iko kwenye hali nzuri

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MwanaHaki, Mar 26, 2009.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Waungwana,

  Nimeamua kuuza gari yangu, aina ya Mitsubishi Pajero Mini, ya mwaka 1997, 4WD, ambayo iko kwenye hali nzuri.

  Bei ni TShs 2.5 million, sishuki chini ya hapo. Nina shida ya hela, si kwamba gari ni mbovu... inatembea... lakini nataka kubadilisha usafiri. Kwa mawasiliano, tutafutane kwenye namba za simu +255-786-019019 na/au +255-715-019119

  Asanteni.

  ./Mwanahaki

  P.S. Nimeambatanisha picha

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Inaonekana kitu bado kiko fresh kiaina, ila mkuu naona umekula taa za nyuma zote na kule mbele upande wa kushoto naona pua ilitaka kutoka, sijaona vizuri upande wa kulia, kuna onekana kama nako kuna kubonyea fulani hivi......!
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  mzee kinachonitisha ni hiyo bei 2.5 kama TATA NANo
   
 4. N

  Ndele Member

  #4
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndugu yangu hiyo bei mbona imekaa vibaya! lakini nitakucheck ili nikiinunua nimpatia wife.
   
 5. Shemzigwa

  Shemzigwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  mkuu hapo mbele vipi kushoto kama pamebonyea
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Bei inatisha! 2.5?

  Je ni mkweche? Mashine safi?
   
 7. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pia ingependeza kama ungetaja hapo kwenye ..... japo weakness yake moja.
   
 8. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #8
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tehee INVISIBLE lini unauza la kwako nije kununua??????
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mh, sasa itabidi JF waanze ku-charge wanaotangaza biashara humu... i think its fair;

  sasa na hiyo nyumba utaiuza pia? imekaa poa with good space outside
   
 10. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 340
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Would u accept 2 mil cash!
   
 11. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Purely kibongo bongo!!
   
 12. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #12
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa hakuna kiso kasoro, nawapeni historia fupi ya gari hili, ili mwenye kutaka kulinunua aamue, asiyetaka naye aamue.

  1) Kuna "mtu mzima ovyo" fulani alijidai mjanja wa magari, nilimpa kazi, lakini yeye akapitiliza maelekezo, sawa na daktari unampa kazi ya kufanya operation ya appendicitis na yeye akaamua kufanya ya tonsilitis pia! Ameulizwa? Huyu jamaa, ambaye alijiona yeye ni fundi bab-kubwa alishusha engine ya gari kwa kazi moja ndogo sana... kuziba matundu yaliyotokea kwenye engine oil sample na gearbox sample... ni kazi ndogo, si kubwa. Jamaa huyu akaamua kufanya kazi nyingine ambazo alidhani ni sawa na kwenye magari aina ya Toyota, kwamba, unafungua, kisha unafunga, mambo mswano! Wapiii! Alifungua "main fold", akafungua "turbo charger". Hivi vitu viwili vina utaalam wake, na wakati alipofungua kumbe aliharibu vibaya "water jacket", hakujua kwamba ilikuwa imetoboka. Aliporudisha engine na vifaa vyale, vyote, "main fold" na "turbo charger" vilikuwa vinavujisha engine oil kutoka kwenye engine, na baadaye, lile tundu lililokuwa kwenye "water jacket" likapanuka. Hatimaye, baada ya kuhangaika saaaaaaaaanaaaaaaaa na hiyo engine, ILI-SEIZE, na hapo ikawa mwisho wa awamu ya kwanza ya matengenezo ya gari, wakati huo tayari nimeshatupa (pamoja na kununua "turbo charger" nyinhgine) zaidi ya Shs. 800,000/=! Nikasema isiwe tabu, nitaingia kwenye awamu ya pili!

  2) Awamu ya pili akaja fundi mwingine, akaivuta gari mpaka gereji kwake, Mabibo Mwisho. Gereji ya kwanza ilikuwa ni Ilala, kwenye mitaa ya Shaurimoyo na Songea, nadhani wenyeji wa Dar mnapafahamu. Huku fundi huyu akaamua kuwa mbunifu, akabadilisha mfumo mzima wa "firing system" ya engine, kutoka kwenye "turbo charged" kwenda kwenye "electronic fuel injection" system. Sawa, ni system nzuri, lakini wakati wa kufunga kila kitu baada ya kufanya engine overhaul (piston 2 na piston rings zote zilibadilishwa), alikosea kuweka "gasket maker", kwa hiyo, kwa upande wa nyuma wa engine, oil ilikuwa inavuja, kwa hiyo nilitumia gari kwa siku tatu na hatimaye "tappets" zilisagika, zikaanza kupiga kelele, nikaamua kuacha kuitumia gari. Kwenye awamu ya pili nimetumia zaidi ya Shs. 1,500,000/=. Naomba wenye calculator mpige hesabu.

  Sasa baada ya haya yote kutokea, nikaona bora hii gari niiuze, kwani nimechoka kuitengeneza, na kwa kuwa, kwa sasa, kinachotakiwa ni kubadilisha Cylinder Head pekee, atakayependa kuinunua, atalazimika kuingia gharama hizo za ufundi, au, akipenda, mimi ningemshauri anunue engine ya Nissan pick-up, aina ya 120Y au A12, ambazo kwa modifications kidogo unaweza kufunga (bila kubadilisha gear box) na unakuwa unaachana na haya matatizo ya fuel injection, coils, control box, etc.

  Gari hii nimenunua kwa Shs. 5,000,000/=, nimeigharamia zaidi ya Shs. 2,000,000/= kuitengeneza, kwa kuwa mpuuzi fulani aliamua kwamba yeye ni mjuzi sana wa magari aina ya Mitsubishi, akanitia hasara isiyo na kifani.

  Lakini, kwa kuwa ina matengenezo kidogo, nimeamua kukubali hasara zaidi, ya Shs. 2,500,000/=, kwa hiyo, kwa wastani, gari hii nitakuwa nimeigharimia kwa takriban Shs. 5,000,000/= toka nimeinunua, na wala sijaifaidi. Sina bahati nayo. Si riziki.

  Nimeamua kuwa mkweli, kwani nadhani kwa kufanya hivyi, ninyi wenzangu, wana-JF, mtaamua kwamba, (a) kama mtaweza kuinunua na kuitengeneza, na (b) au mtaona kwamba mtakuwa mnapoteza muda wenu.

  Kwa upande wa mbele, kushoto, nililkuwa nimeegesha gari nikarudi na kukuta imegongwa, kwa upande wa bumper ya mbele, chanzo cha hiyo mud-guard kuvimba. Lakini fundi wa panel beating ameniambia hiyo ni kazi ya dakika 45, kuinyoosha, inakuwa kama inavyopaswa.

  Kuhusu taa za nyuma, lens ya upande wa kushoto imevunjika kidogo, ilikuwa hivyo wakati ninainunua, ila, kwa upande wa kulia, nilipata ajali ya kugonga nguzo ya parking shed pale No. 50 Mirambo House, wakati nilipokwenda kuwatembelea maswahiba zangu wa Africa Online. Nilikuwa ninaegesha gari kurudi kinyumenyume, kulikuwa na mtu alikuwa na haraka zake, hakuwa mstaarabu, akawa anapiga honi nimpishe, kwa ile presha niliyokuwanayo, nilikata kona haraka na kurudisha gari nyuma na kufikia kugonga nguzo ya chuma. Hata yeye aliyekuwa akiniharakisha alitahayari na kuniomba msamaha, akajuta kitendo kile.

  Asanteni, nadhani kama ni udhaifu wa gari hili, nimeutoa wote, ila, kwa sasa, gari iko kwenye hali nzuri, isipokuwa kubadilishwa Cylinder Head, na vitu vingine vidogo tu, ambavyo havina gharama kubwa.

  Asanteni kwa ushirikiano wenu, nyote mlionipigia simu.

  Narudia tena, bei yangu ni Shs. 2.5 million, pekee! Sitashuka zaidi ya hapo, kwani tayari nimeshakula hasara kubwa. Ikishindikana, nitapata hela nyingine za kutengeneza, nitaitengeneza, nitatembelea, na ikiwa inatembea nitauza kwa bei nzuri zaidi.
   
 13. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2009
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Asante sasa kaka kwa kuwa mkweli!ubarikiwe!sasa hebu tujuze kitu kimoja!Cylinder head ya Pajero inauzwa kiasi gani?na nikiamua kuichukua na kubadili engine kuweka ya TOYOTA itagharimu kiasi gani?
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Speaking Openly, without fear!
   
 15. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mwanahaki tuliongea sana jana kuhusu hii issue. Nilimtuma mdogo wangu akuone, bahati mbaya hakuja jana kutokana na msiba tulionao hapo Dar. Hata hivyo matatizo uliyoyaelezea hapa yamenitoa kwenye hii safari. Katika vitu ninavyoviogopa ni haya mambo ya modifications. Hata hivyo nashukuru kwa kuwa muwazi. Hope next time we can make business, but for this am out. Sorry brother.
   
 16. A

  Audax JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi nina 2.3 what do u think?
   
 17. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu Audax,

  Duh si umemsikia mwenyewe anakwambia hauzi chini ya hapo (i.e 2.5m) ndugu yangu? Mbona unamtia majaribuni mwenzio?
   
 18. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nasikia hizi gari za mitsubishi ni mabomu sana sijui ni kweli? Kuna hizi mitsubushi io zinalingana na escudo kwa size, naona kwa sura zinapendeza na watu wamezichangamkia nami nazitamani, sijui ni nzuri au nazo mabomu kama RVR?
   
 19. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #19
  Mar 31, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Audax,

  Kama kweli unataka kuinunua, na umeridhika kwa bei hiyo, karibu. Nitafute, ni yako.

  ./MwanaHaki
   
 20. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Jaribu kumPM audax kwamba uko ready kumpa at that price kama kweli anania ya kununua hiyo gari!
   
Loading...