Gari iliyobeba mwili wa Kim kumbe ni ya Kimarekani!!!!

Aaah sasa watakuwa wanamsingizia mzee wa watu daaaah!

Huenda zikawa ni propaganda za Wamagharibi tu hizo...
 
Kim was believed to have been very fastidious about how his rice was prepared. According to his first wife's nephew, the Dear Leader made female staff inspect each grain individually to ensure they were the requisite length, weight and colour. He also insisted it was cooked over a fire made with wood taken from trees that only grow on a particular Chinese mountain
Duh! Hiyo hapo juu ni kali!

Hivi watamsingiiziaje kama hii? teh teh...Huyu mzee bana, let him rest in peace, duh! Sasa mtoto sijui ndo vipi...Ila wanasema ni kama mdingi wake tu, ila even more.
 
Hawa wakuda wana mambo ya ajabu sana..kuna mwandishi mmoja aliendaga kwene show yao ya innovation kwene late 1990s au early 2000s nafikiri, wakawa wanaonesha eti computer ya 'Kikorea' na OS yake, sasa yule mzungu akataka kujua inafanyaje kazi ile kui-restart ndo ikareveal kuwa it is actually a PC. he he he..
Hahahaha! Inaonekana hiyo nchi Kim amewapiga sana wananchi wake mchanga wa macho...
 
Some of them really strain credulity!

Kim was believed to have been very fastidious about how his rice was prepared. According to his first wife's nephew, the Dear Leader made female staff inspect each grain individually to ensure they were the requisite length, weight and colour. He also insisted it was cooked over a fire made with wood taken from trees that only grow on a particular Chinese mountain
 
Wakorea kaskazini wanaweza kuwa masikini lakini ni maskini jeuri wa kweli. Huwezi kuwa maskini jeuri wa kweli kama hutayarishi nchi yako kuwa na uwezo huo. Katika wale walioitwa kama Axis of Evils na Bush, wawili wamebaki. DPRK na Iran. Sadam kaondoka. Sadam Kaondoka kwa sababu baada ya kutishiwa nyau na Marekani kuhusu silaha zake za Nyuklia akaamua kuachia ngazi akiamini kwamba hiyo itampa urafiki na Marekani na kuweza kuendelea kutawala kwa mabavu Iraq bila Marekani kumuuliza swali na kufanya mambo yake kama anavyotaka. Baada ya Wamarekani kuhakikisha kwamba Saadam hana tena uwezo wa Nyuklia baada ya kufuata masharti yao, kilichofata ni kumshukia kama mwewe!!!!!!!! DPRK na Iran wameweza kumudu mikimiki ya vitisho kwa sababu hawakuwa tayari kufuata masharti ya Marekani ya kuachana na mipango yao ya silaha za Nuklia kwa sababu waliamini kwamba huo utakuwa mwisho wa utawala wao kutokana historia ya Marekani kushughulikia nchi dhaifu. Hivyovitisho walivyopewa na Wamerekani na washirika wao kwao ilikuwa motisha ya kutumia rasilimali zao kujijengea uwezo wa kujilinda na kuwa tayari kuonyesha kwamba ukijaribu kutushambulia basi gharama yake utaiona. Waliweza kuonyesha utayari wao wa kukabiliana na Marekani kwa kutokubali masharti waliyowekewa kuhusu mpango wao wa silaha za nuklia na kuonyesha uwezo wao wa kutengeneza silaha ambazo ni tishio kwa maslahi ya Marekani. Matokeo yake ni fundisho kwa viongozi wengine kwamba taifa lako litajengwa na watu wake na sio kutegemea misaada au kuogopa vitisho kutoka nchi zingine. Mfano wa yaliyomkuta Khadafi ni uleule uliomfika Saadam, kukubali masharti ya kuua nguvu za kujilinda za taifa lako na matokeo yake wamekufa kifo cha udhalilishaji kuliko wangekataa masharti na kukubali kufa kifo cha kiume wakikaidi masharti dhalilishi kwa nchi zao.
Kim amekufa kifo cha kishujaa hata kama mataifa ya magharibi yamesusia kifo chake. Ndo maana habari za kifo chake zinatolewa na waandishi wa habari wa mataifa ya magharibi kwa heshima ukilinganisha na vifo vya Saadam na Khadafi ambavyo vinatangazwa kwa uzalilishaji kutokana na wao kuwa wajinga!
 
Pia nimesikia CNN kuwa wale wote waliokuwa wakiangua vilio kwenye mazishi hawakuwa wakilia machozi ya kweli. Yote hiyo ilikuwa ni propaganda tu kuonyesha kuwa "Dear Leader" alikuwa anakubalika.

Sasa sijui kama ni kweli au la but I can't put anything past those people.

Nilikuwa naamini unaweza sikia hii lugha vizuri kumbe inakupa tabu kidogo... kwa kuwa wanarudia rudia sikiliza tena
 
20. His biography also says that he does not defecate or urinate

enhanced-buzz-24766-1324316602-9.jpg

Anazo 2o ridiculous things, nimeipenda hiyo hapo juu namba 20...Yani wananchi walidanganywa mzee mzima haendi haja lol
20 Ridiculous Things You Never Knew About Kim Jong-Il

Mkuu, kweli tunawapenda wamerekani sana lakini sio kila wanachosema na kuandika ndiyo ukweli, sidhani kama hawa jamaa ni wajinga kiasi hicho!

Ziko wapi zile silaha za maangamizi kule Iraq, Colin Powell, alitoa ushahidi dunia yote ikaamini mwisho wa siku ilikuwaje?
 
hata kama ni kweli .....unawezaje amini media ya chama pinzani ikitathmini habari ya chama kinacho kizana nacho..there is great chance of propaganda kuhusika,,and if your name is idiot is not by chance you are real idiot.
 
Ukimiliki Media unamiliki na akili za watu..
Mfano mdogo kila siku uwe unasoma gazeti la Uhuru na Mzalendo tu, unadhani akili yako itakuwaje?
 
Masikini we,...dunia yote imelaghaiwa na western media. Mambo mengi yanayosemwa na CNN, BBC n.k kuhusu nchi hasimu na Western ni propaganda. Si vizuri kuamini kila jambo, tafuta info zaidi.
 
ha ha ha ha bizarre stuffs! lol

Watu wanaojifanya wanachukia Taifa fulani hivi na watu wake in general huwa nawaona mapunguani kiaina yake. Unamkuta mtu anachukia Marekani ile mbaya, hadi individuals. Ukimuuliza atakwambia ni foreign policy yao au mambo yao ya kihistoria. Sasa maamuzi yanayochukuliwa na watendaji Kitaifa wewe unapelekea chuki zako kuwa personal, wapi na wapi!!

Mfano kuna rafiki yangu mmoja M-polish, yeye anachuki wajerumani hata kusalimiana nao kwa kumshika mtu mkono hawezi! Ukimuuliza ni kwanini, anasema kutokana na jinsi alivyofundishwa katika historia. Cha ajabu favorite car yake ni BMW, halafu mjomba wake anaendesha Audi. Na kwa vile anamatatizo ya meno, huwa namwambia, the likelihood kwamba hospitali anayoenda kutibiwa precision instrument zake zote zimeshikwashikwa na Wajerumani ni kubwa...anabakia kununa tu!!

Vivyo hivyo, kuna Mchina rafiki yangu anachukia Wajapani kutokana na mambo ya kihistoria, lakini tv yake na entertainment system zote ni za Wajapani.

Mtu unamkuta anatumia GPS na vifaa vingine kibao ambavyo viko controlled na Wamarekani, lakini chuki inapelekwa hadi kwa watu binafsi. Ni sawasawa na wenzetu wale wanaochukia Wachaga, lakini wakikata kona kwenda kununua vocha inabidi tu wasalimiane na Mangi pale kiosk! Dunia duara, ni kama utando wa buibui. Wee jenga uhasama wako, lakini siku ya siku utanasa tu!!
 
Hahahahaha,

Who does this sound like?

18. Kim Jong-Il's biography claims his birth was "foretold by a swallow and heralded by a glorious double rainbow and the appearance of a new star"
 
Hahahahaha,

Who does this sound like?

18. Kim Jong-Il's biography claims his birth was "foretold by a swallow and heralded by a glorious double rainbow and the appearance of a new star"

unatuchomekea kishkaji waumini??!!! lol
 
ha ha ha ha bizarre stuffs! lol

Watu wanaojifanya wanachukia Taifa fulani hivi na watu wake in general huwa nawaona mapunguani kiaina yake. Unamkuta mtu anachukia Marekani ile mbaya, hadi individuals. Ukimuuliza atakwambia ni foreign policy yao au mambo yao ya kihistoria. Sasa maamuzi yanayochukuliwa na watendaji Kitaifa wewe unapelekea chuki zako kuwa personal, wapi na wapi!!

Mfano kuna rafiki yangu mmoja M-polish, yeye anachuki wajerumani hata kusalimiana nao kwa kumshika mtu mkono hawezi! Ukimuuliza ni kwanini, anasema kutokana na jinsi alivyofundishwa katika historia. Cha ajabu favorite car yake ni BMW, halafu mjomba wake anaendesha Audi. Na kwa vile anamatatizo ya meno, huwa namwambia, the likelihood kwamba hospitali anayoenda kutibiwa precision instrument zake zote zimeshikwashikwa na Wajerumani ni kubwa...anabakia kununa tu!!

Vivyo hivyo, kuna Mchina rafiki yangu anachukia Wajapani kutokana na mambo ya kihistoria, lakini tv yake na entertainment system zote ni za Wajapani.

Mtu unamkuta anatumia GPS na vifaa vingine kibao ambavyo viko controlled na Wamarekani, lakini chuki inapelekwa hadi kwa watu binafsi. Ni sawasawa na wenzetu wale wanaochukia Wachaga, lakini wakikata kona kwenda kununua vocha inabidi tu wasalimiane na Mangi pale kiosk! Dunia duara, ni kama utando wa buibui. Wee jenga uhasama wako, lakini siku ya siku utanasa tu!!

Haya mambo bana hata Marekani anaichukia sana China anaona kama inatishia uchumi wake, lakini anakwenda kukopa huko huko China, hahahah!
 
Mimi mwenyewe leo asubuhi nilipokuwa yahoo.com nikaona zile picha nikajiuliza hili si old school LTC kweli?

Ila nafikiri walitumia hiyo hearse makusudi kuonesha mtazamo wao mpya.
 
Mimi mwenyewe leo asubuhi nilipokuwa yahoo.com nikaona zile picha nikajiuliza hili si old school LTC kweli?

Ila nafikiri walitumia hiyo hearse makusudi kuonesha mtazamo wao mpya.

Either that or Kim kawafungia mpaka hawajui concept nzima ya brand kiasi kwamba hawakujua kwamba hiyo soo.

Ni kama Nyerere aliyehubiri Ujamaa na kujitegemea Tanzania na kuvunja uhusiano na Waingereza over Ian Smith kwenda kufia hospitali ya St. Thomas, London Uingereza wakati tuna Muhimbili yetu.
 
Back
Top Bottom