Gari aina ya Nissan Qashqai

maiwa

Member
Dec 16, 2013
23
7
Tafadhali waungwana gari kuna mtu anataka kuniuzia gari iliyotajwa, kuna anayefahamu kuhusu uimara wake, upatikanaji wa spare na bei zake kwa hapa bongo aweze kunishauri kabla sijaingia mkenge? Naomba ushauri kwa anayefahamu tafadhali.
 
Nissan_Qashqai%2B2_dCi_(Facelift)_%E2%80%93_Frontansicht,_16._April_2011,_D%C3%BCsseldorf.jpg

Nissan sio mbaya ila aina hiyo ndio kwanza nimeiskia baada ya kuona uzi wako, wasiwasi wangu ni spea itakugharimu sana maana inaonekana sio gari common na ukizingatia Nissan spea huwa ghali japo mi natumia nissan pia
 
Hiyo Qashkai ni ya Kiingereza, imetengenezwa kwa ajili ya uko, Spares zinaweza kuwa shida, manake hata Toyota zilizotengenezwa kwa ajili ya UK Huwa spare zinatofautiana kidogo, ukinunua spare unahitaji kufanya modification kidogo, kuna wakati niliitamani sana hiyo Qashkai hila kuna mdau alinishauri vizuri.
 
Tafadhali waungwana gari kuna mtu anataka kuniuzia gari iliyotajwa, kuna anayefahamu kuhusu uimara wake, upatikanaji wa spare na bei zake kwa hapa bongo aweze kunishauri kabla sijaingia mkenge? Naomba ushauri kwa anayefahamu tafadhali.

gari nzuri sana......zinatengenezwa UK for european market....kwahio jiandae kuagiza spare kutoka UK,sina uhakika kama spare zake utapata tanzania....watu wanaogopa NISSAN lakini ingawa spare zake ni bei ghali lakini ukifunga spare inakaa muda mrefu...pia NISSAN ni stable na comfortable kuliko TOYOTA
 
Nashukuru kwa ushauri wenu, utanisaidia kufanya maamuzi ya maana.
 
Nashukuru kwa ushauri wenu, utanisaidia kufanya maamuzi ya maana.

kaka usiogope kununua gari uipendayo kisa watu wamekushauri.
Ukitaka genuine ushauri mtafute fundi wa CFAO Motors pale akupe genuine advice. Wanapatikana pale Morocco TOTAL petrol station na M-City TOTAL petrol station. Mtafute mmoja akupe keen advice cause wao wanauza hayo magari (ingawa kwa sasa sijaona tena) na wanayajua vizuri kuhusu ubora wake juu ya spare na kuhimili hali ya huku kwetu tropical zone.
Kaaaaziiiiii ni Kwaaaaakoooooo
 
Tafadhali waungwana gari kuna mtu anataka kuniuzia gari iliyotajwa, kuna anayefahamu kuhusu uimara wake, upatikanaji wa spare na bei zake kwa hapa bongo aweze kunishauri kabla sijaingia mkenge? Naomba ushauri kwa anayefahamu tafadhali.

WAKUU HESHIMA MBELE, PIA NA MIMI NAOMBA MWENYE KUFAHAMU Nissan X Trial ya 2002, Bei yake mpaka kufika barabarani, Manake nimeona kupitia Be foward bei mpaka Dar ni USD 3941, je ili niiweke barabarani itanigharimu kiasi gani, NAOMBA MSAADA WENU wakuu.

Gari yenyewe in kama Hii.
PwAAAABJRU5ErkJggg==

Tafadhali msikasilike kwa kutumia uzi wa mtu mwingine.
 
Bonge la gari hiyo, achana na mawazo ya maskini ooh mara spare; ndege je si utaambiwa kuna mvua sana Afrika usinunu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom