Garama za kutoa na kutuma pesa mitandaoni ni kubwa sana. Kutoa laki 4 kwenye ATM ni TZS 1,000, M-PESA TZS 7,000.

Sina hamu na SIM BANKING mwanzaoni nilikua nahamisha 1000, 500 kuja Tigopesa aisee sikujua makato kumbe ilikua inalambwa 1500, unahamisha 500 ila makato 1500/= statement nilitumiwa kwenye email nilibaki mdomo wazi na ndo ikawa siku ya mwisho kutumia SIM BANKING.
Nilienda bank nikijua nimeibiwa
Jamaa alicheck akasema ndugu una miamala ya kufa mtu
Sigusi tena
 
Hili nalo pia ni la Serikali? Kwani si wameweka Gharama zao wazi au wameficha? Kwani serikali ndio imewapangia hizo gharama za kuwatoza wateja?
 
Sema watu hawajui tu. Kama una mtu unamtumia pesa mara kwa mara kama mzazi, mwanafunzi nk... na yupo jirani na ATM, ni bora wote mjiunge NMB kwa sababu kutuma pesa ni kama bure tu, then kutoa ni hiyo buku tu na ni 1200 kwa CRDB.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
hapa ndo naamini kuhusu ile 10%
aliekwambia hii mitandao ipo kukusaidia ni nani ? Hii ni biashara na hawa jamaa wapo pale kutengeneza maximum profit kwa ajili yao na shareholders wao.., na watachaji kadri ya watu watakavyotoa.., pia kumbuka unalipia convinience kama benki ni cheap kwanini usiende benki ?, na kama serikali inaona hii haifai si ina shares nyingi airtel na inamiliki TTCL kwanini isipunguze kule ili iongeze ushindani...

People we need to decide kama ni ubepari na free market we want hii ndio its inner workings.., hatuwezi kuwa nusu nusu.., huku tunapenda ubepari huku tunataka government intervention...,
 
Kuna bank huwa wanatuma msg kuwa unaweza kuweka akiba kwenye akaunti yako ya bank kupitia tigopesa, mpesa nk. Nikajaribu kuangalia makato yake, aisee nilidhani wanatania.
Yaani KUWEKA sh 10,000 unakatwa kati ya 800 na 1000.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom