Gandhi:Amri kuu SABA za Jamii: Ya Saba ni kuu kuliko zote "Politics without principle"

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
mahatma-gandhi-31.jpg

Kwa Mujibu wa Mahatma Gandhi
Kuna Dhambi saba hatarishi katika jamii. Dhambi ya saba na mbaya ni Siasa isiyo na Ukweli/kanuni au POLITICS WITHOUT PRINCIPLE.

Siasa/politics - "Ni mapambano ya kikundi cha watu kwa ajili ya kupata madaraka yatakayompa mtu mmoja au zaidi uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya Watu wengi"

SIASA ISIYO NA UKWELI HULETA MACHAFUKO MFU NA BAADAE HUFUFUKA NA KUWA HAI.
Kuwa na siasa isiyo na Ukweli ulionyuma ya kila maamuzi yanayochukuliwa na mwanasiasa huleta sintofahamu katika jamii, sintofahamu hii inaweza kuchukua Mimba na baadae kuzaa machafuko au kutokuelewana miongoni mwa wanajamii. Mifano ipo kila kona ya dunia.

Kutokuwepo na ukweli na dhamira safi kumesababisha wanasiasa wetu kubadilika rangi kama vinyonga. Siasa iliyosimama juu ya jukwaa la ulaghai na ujanja ujanja inafaa Ibatizwe upya kwa fimbo ya jamii. Jamii iliyoleweshwa mvinyo wa siasa hazi anaweza kuona ni afadhali kumkabidhi madaraka Mwanasiasa laghai kidogo dhidi ya mwenye ulaghai alioaminishwa ni Mwingi hata kama anauhakika wote hapo ni walaghai.

Asubuhi la leo nimepitia nasaha za mzee wetu huyu wa duniani nasaa alizozitoa mwaka 1925 lakini hadi kesho Ingawa wewe hatunae duninani lakni nasaha zake zingali zinaishi wenda zikawa dawa wa wafuatiliaji wa siasa na wanasiasa hapa kwetu.


Kwa hisani ya wikipedia
Seven Social Sins - Wikipedia
 
downloadfile.jpeg


HAPA KWETU VIONGOZI MA RAIS WALIOPITA WANAKENUA TU MENO HUKU BWANA YULE AKISIGINA KATIBA.


swissme
 
swissme hayo ni maoni ya mchora katuni ambayo yanaweza kutokuwa sawa pia.
Politics without principle kwa mujibu wa Gandhi upinzani pia imetapakaa zaidi ndio maana unawaona wanatangatanga kila chama.
 
Back
Top Bottom