Gaming Act inaruhusu watu wazima kucheza kamari. Sasa mbona Waziri Mkuu anamzuia huyu jamaa?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,168

Waziri Mkuu amemuonya mtumishi wa umma kuacha kucheza kamari kwa kuwa muda wote ataliwa tu. Atachukua mikopo benki na bado ataendelea kuliwa ambapo ataingiwa na msongo wa mawazo.

Amempata kazi mtumishi mwingine kumfuatilia mtumishi huyo
 
Kamari Ni balaa. Nimepoteza pesa nyingi Sana kupitia Redio Free Afrika na sijawahi kushinda hata Mara Moja.

Screenshot_20221130-173122.png
 
Gaming Act inaruhusu Addiction ?

Lakini hizi ni Siasa wanashindwa nini kupunguza / kutoa matangazo ya Kamari kwenye vyombo mpaka pale usiku wakati minors wamelala ? Au sababu Serikali inachukua takribani asilimia 15 kwa kile anayeshinda ?

Yaani unatangazia watoto kila dakika kuhusu kamari na kila mtaa hata minors wanashiriki alafu.... !!!!!
 
Waanze na sheria ya kuzuia SMS za kamari. Niliwahi kuwapigia mtandao mmoja na kuwataka wasinitumie SMS zao za kamari lakini hawakomi.

Siku hizi hadi TV ya taifa inahamasisha kamari. Vijana wa shule ni wataalamu wa kusuka mikeka kuliko mipango ya kujibidiisha kwenye mambo yenye tija kama soft skills.
 
Inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom