Game Supermarket yafungwa (Ubalozi wa SA waingilia kati)

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Lile duka kubwa kabisa pale mlimani city limefungwa kwa amri ya kamishna wa TRA kutokana na majibishano juu ya kutumia kifaa cha electronic cha kufanyia mauzo (EFD). Wakati TRA wanalazimisha vifaa hivyo kutumika katika teller zote, wao Game wanaona ni njia itakayowapunguzia mapato kwa sababu walizowaeleza TRA lakini zikakataliwa.

Wakati huo huo ujumbe mzito kutoka ubalozi wa Afrika Kusini umetinga kwa kamishna wa TRA kutafuta ufumbuzi wa suala hilo leo hii. Habari kutoka kwa watendaji wa TRA zinadai kuwa inaweza kuchukua hadi wiki 2 kwa duka hilo kubwa kabisa kufunguliwa tena.

Vyanzo vya habari kutoka katika duka hilo (staff) ni kwamba kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi hadi sasa na ndio maana TRA wameshtuka na kukataa hoja za Game. Lakini wamelalamika kuwa hata wao mfumo wa zamani uliwawezesha 'kuwaibia' kidogo makaburu kwa kucheza na computer tu na sasa wana wasiwasi kama nao wataweza kuzichezea EFD.
 
mkuu .... je? supermarkets nyingine za south Africa kama Shoprite na Mr. Price store wanatumia EFD
 
Nunua vifaa hapo at your own risk(kama vimetengenezwa SA)
Vingi ya vifaa hivyo ni rejects kutoka maduka ya SA
Nina tochi,lawnmower na vitu vingine ambavyo vimeharibika baada tu ya kuvitumia muda mfupi, nao hawataki virudi kwao
Buyer beware!!!
 
aseee! Hakuna anaetaka kulipa kodi.

wana haki ya kugoma hao tra ni washenzi wakubwa wakaidai barrick waone ssasa kama madini yanachukuliwa kwanin wasouth wasije kuchota endeleeeeeeeeeeeeeeaaaaaaaaaaaa
 
Kamishena anacheza tu, huwezi pigana na multi national companies. Tusubiri tuone kama halitafunguliwa tena.
 
sidhani kama ni lazima utumie EFD tu ndio uwe unaweza ku-capture all sales; hizi EFD ni dili la watu

the Game inventory system can do that
 
Nunua vifaa hapo at your own risk(kama vimetengenezwa SA)<br />
Vingi ya vifaa hivyo ni rejects kutoka maduka ya SA<br />
Nina tochi,lawnmower na vitu vingine ambavyo vimeharibika baada tu ya kuvitumia muda mfupi, nao hawataki virudi kwao<br />
Buyer beware!!!

I support you fully. I have a first hand account., yet nobody seemed to have had voiced their contempt!
 
Kamishena anacheza tu, huwezi pigana na multi national companies. Tusubiri tuone kama halitafunguliwa tena.

Walipe kodi hao wezi wakubwa TRA bwana wakikushukia hata ukiwa bill gate watakulamba tuu kwa hiyo hawana ujanjaa kodi watalipa tu,mkuu TRA ikikushukia lazima ukome. Mwulize slaa atakuambia.
 
Kamishena anacheza tu, huwezi pigana na multi national companies. Tusubiri tuone kama halitafunguliwa tena.

Kamishna wa TRA akiamua kujitoa kafara, anaweza kumfungia yeyote na sheria imempa nguvu kubwa sana. Anaweza hata kuzuia akaunti yao ya benki au kuwanyang'anya leseni kabisa na kuwaachia uhamiaji wamalizie ya kwao.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom