Crucifix
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 1,651
- 588
Lile duka kubwa kabisa pale mlimani city limefungwa kwa amri ya kamishna wa TRA kutokana na majibishano juu ya kutumia kifaa cha electronic cha kufanyia mauzo (EFD). Wakati TRA wanalazimisha vifaa hivyo kutumika katika teller zote, wao Game wanaona ni njia itakayowapunguzia mapato kwa sababu walizowaeleza TRA lakini zikakataliwa.
Wakati huo huo ujumbe mzito kutoka ubalozi wa Afrika Kusini umetinga kwa kamishna wa TRA kutafuta ufumbuzi wa suala hilo leo hii. Habari kutoka kwa watendaji wa TRA zinadai kuwa inaweza kuchukua hadi wiki 2 kwa duka hilo kubwa kabisa kufunguliwa tena.
Vyanzo vya habari kutoka katika duka hilo (staff) ni kwamba kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi hadi sasa na ndio maana TRA wameshtuka na kukataa hoja za Game. Lakini wamelalamika kuwa hata wao mfumo wa zamani uliwawezesha 'kuwaibia' kidogo makaburu kwa kucheza na computer tu na sasa wana wasiwasi kama nao wataweza kuzichezea EFD.