Game Supermarket yafungwa (Ubalozi wa SA waingilia kati)

Kamishna wa TRA akiamua kujitoa kafara, anaweza kumfungia yeyote na sheria imempa nguvu kubwa sana. Anaweza hata kuzuia akaunti yao ya benki au kuwanyang'anya leseni kabisa na kuwaachia uhamiaji wamalizie ya kwao.

yes nakubaliana na wewe .... hatuwezi kuubeza uwezo na mamlaka aliyopewa commissioner wa TRA

Details zaidi zinahitajika.
Ila ninachojua ni kwamba hicho kimtambo EFD cha TRA kina matatizo sana kwa sababu kuna wakati mwingi tu huwa network yake iko down. Hii husababisha maduka ya kawaida kutoa risiti za mkononi wakati kiko down sasa kwa duka kubwa kama GAME itawabidi wabuni mbinu mpya kabisa ya kutoa risiti wakati mtandao wa TRA uko down.
Again, sijui details lakini in general to every law there is exception to the law. TRA wakitumia busara hii inaweza kusaidia bishara kuendelea na kodi kukusanywa.

Kamishna wa TRA akiamua kujitoa kafara, anaweza kumfungia yeyote na sheria imempa nguvu kubwa sana. Anaweza hata kuzuia akaunti yao ya benki au kuwanyang'anya leseni kabisa na kuwaachia uhamiaji wamalizie ya kwao.

Sawa, lakini kamishana kabla hajaanza kuonyesha mabavu ni lazima ajiulize ni watanzania wangapi wanatumia GAME to make ends meet?
Hiko kimtambo kina matatizo mengi sana. Idea ya TRA kwamba one size fits all haiko realistic, wanatakiwa kuwa flexible in some cases.

WALIPE KODI HAO WAACHE USHENZI. SISI WAFANYAKAZI P.A.Y.E INATUMALIZA, THEN WAO WASILIPE? FUNGIA KABISA HAO HADI WATAKAPO COMPLY UNLESS WAACHE KUTOZA VAT KWENYE PRODUCTS ZAO WHICH OFFCOURSE IS NOT ALLOWED IN THE EYES OF LAW(vat threshold)

Suti anayo jamani, wamnunulie kanda ya muziki wa Lucky Dube atawaachia!
Game wakitaka mambo yao yawanyookee na wasiandamwe na TRA, wampeleke JK Johanessburg wakamnunulie suti kama walivyofanya waarabu.

Walipe kodi hao wezi wakubwa TRA bwana wakikushukia hata ukiwa bill gate watakulamba tuu kwa hiyo hawana ujanjaa kodi watalipa tu,mkuu TRA ikikushukia lazima ukome. Mwulize slaa atakuambia.

Slaa siyo MNC.

Sawa, lakini kamishana kabla hajaanza kuonyesha mabavu ni lazima ajiulize ni watanzania wangapi wanatumia GAME to make ends meet?
Hiko kimtambo kina matatizo mengi sana. Idea ya TRA kwamba one size fits all haiko realistic, wanatakiwa kuwa flexible in some cases.

check context ndugu zemarcopoo, nilikuwa namjuza aliyekuwa akibeza uwezo wa kamishna wa TRA. Nakubali pia flexibility is required almost katika kila jambo.

Mlimani City imeuzwa kwa kampuni ya Botswana. Strategically, the GAME supermarket might also be 4sale!

Kamishna wa TRA akiamua kujitoa kafara, anaweza kumfungia yeyote na sheria imempa nguvu kubwa sana. Anaweza hata kuzuia akaunti yao ya benki au kuwanyang'anya leseni kabisa na kuwaachia uhamiaji wamalizie ya kwao.

Safi mkuu kwa kunyambua nguvu za kamishena. Wasiwasi wangu ni je ana huo utashi wa kuzitumia nguvu hizo alizopewa kisheria hadi mwisho ukizingatia MNC walivyo wazuri wa kurandaranda ktk corridors of power? Akiweza safi na inakua nzuri kwa nchi sababu tunahitaji watu kama wao wanaosimamia sheria.

Mlimani City imeuzwa kwa kampuni ya Botswana. Strategically, the GAME supermarket might also be 4sale!

Mlimani City iko mbioni kuuzwa, lakini biashara ile haina uhusiano na hili la Game kufungiwa. Hawa wamefungiwa kwa sababu za kukataa kutumia EFD. City ikiuzwa Game watakuwa wapangaji wa landlords wapya.

Safi mkuu kwa kunyambua nguvu za kamishena. Wasiwasi wangu ni je ana huo utashi wa kuzitumia nguvu hizo alizopewa kisheria hadi mwisho ukizingatia MNC walivyo wazuri wa kurandaranda ktk corridors of power? Akiweza safi na inakua nzuri kwa nchi sababu tunahitaji watu kama wao wanaosimamia sheria.

Kama sikosei kamishna wa sasa ni Kitillya, jamaa asiye na utaratibu wa kuzungumza sana na wana habari, therefore ni vigumu kujua misimamo yake au kama ana utashi na nia ya kweli ya kuokoa pesa za taifa letu. Isijekuwa wakuu wamepishana kwenye issue za 10% so wakaamua kutumia rungu zito. Lakini jamaa nao hawakubali na balozi wao mwenyewe ndiye anaye-spearhead negotiation na TRA. Kazi kweli kweli......

Vyanzo vya habari kutoka katika duka hilo (staff) ni kwamba kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi hadi sasa na ndio maana TRA wameshtuka na kukataa hoja za Game. Lakini wamelalamika kuwa hata wao mfumo wa zamani uliwawezesha 'kuwaibia' kidogo makaburu kwa kucheza na computer tu na sasa wana wasiwasi kama nao wataweza kuzichezea EFD.

Wabongo bwana kwa uchakachuaji, wee acha tu!

sidhani kama ni lazima utumie EFD tu ndio uwe unaweza ku-capture all sales; hizi EFD ni dili la watu

the Game inventory system can do that

HASWAAAA NA TENA UJIONGEA VZR NA VISHOKA WA TRA WANAKUFUNZA JINSI YA KUWEKA MAMBO SAWA

mkuu hujaelewa,tatizo ni utaratibu mbovu kabisa wa kutoza kodi,nimetembea nchi nyingi sana sijawahi ona utaratibu kama huu

Hizo mashine nadhani nao ni ulaji mwingine kwa wlafi wetu walioko huko nafasi za juu. Hazisaidii chochote katika uongezaji mapato (kutokana na ushahidi toka kwa mhasibu aliyenieleza jinsi ambavyo unaweza kukwepa kurekodi mauzo yako-mfano: nikishirikiana na muuzaji na kununua bila risiti)....Pia ikumbukwe kuwa tabia ya kukubali kutopewa risiti kwa makubaliano ya kupunguziwa bei ni kawaida hapa Tanzania (hata kama itapingwa katika jamii hii)
Kama ungefanywa utafiti huru baada ya miaka miwili tangu mashine zimeanza kutumiwa na tuambiwe ni ongezeko la kiasi gani la mausnyo ya kodi limepatikana kutokana na mashine hizo naamini kabisa halitolingana kabisa na thamani halisi ya zoezi zima la kutengeneza system hiyo na manunuzi ya mashine kwa watumiaji (japo gharama hiyo inakuwa offset kwenye kodi walipayo; hiyo nayo ukiitafsiri ni kodi iliyopotea kwa kwenda kwa wenye matumbo yajuayo kula KULIKO WANANCHI WANAOKULA MLO MMOJA KWA SIKU NCHINI HUMU

Lile duka kubwa kabisa pale mlimani city limefungwa kwa amri ya kamishna wa TRA kutokana na majibishano juu ya kutumia kifaa cha electronic cha kufanyia mauzo (EFD). Wakati TRA wanalazimisha vifaa hivyo kutumika katika teller zote, wao Game wanaona ni njia itakayowapunguzia mapato kwa sababu walizowaeleza TRA lakini zikakataliwa.

Wakati huo huo ujumbe mzito kutoka ubalozi wa Afrika Kusini umetinga kwa kamishna wa TRA kutafuta ufumbuzi wa suala hilo leo hii. Habari kutoka kwa watendaji wa TRA zinadai kuwa inaweza kuchukua hadi wiki 2 kwa duka hilo kubwa kabisa kufunguliwa tena.

Vyanzo vya habari kutoka katika duka hilo (staff) ni kwamba kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi hadi sasa na ndio maana TRA wameshtuka na kukataa hoja za Game. Lakini wamelalamika kuwa hata wao mfumo wa zamani uliwawezesha 'kuwaibia' kidogo makaburu kwa kucheza na computer tu na sasa wana wasiwasi kama nao wataweza kuzichezea EFD.

Jamani TRA waulizwe hizi copy and paste zitakosesha jamhuri yetu mapato,EFD kwenye ulimwengu wa Giza,Electronic...Device ,umeme unapokuwa hamna kwa asilimia zaidi ya 70 ina maanisha wafanyabiashara wote wenye VRN wanarekodi vipi mauzo. EFD ni ufisadi mwingine ndani ya Nchi yetu.TRA wangeangalia namna ya kudhibiti mauzo.Ushauri wa bure,ni wakati muafaka kwa serikali yetu kutenga wauzaji wa jumla na wale wa rejareja,Kuwe na Leseni mahsusi kwa wauzaji wa jumla wa bidha ambao hawataruhusiwa kuuza rejareja,na wauzaji wa rejareja,ni rahisi pakiwa na uwajibikaji kupitia record za mali tangu inaingia bandarini hadi kufika kwa mlaji wa mwisho kwa mali za kutoka nje,kutoka kwa mzarishaji kwenda kwa muuzaji wa jumla mpaka kwa muuzaji wa rejareja kwa bidhaa za ndani.MHIMU ni UWAJIBIKAJI KATIKA KUSIMAMIA.EFD ni Upuuzi sana.

Back
Top Bottom