Game Officer amenitoa ushamba ni kuhusu FISI DUME NA JIKE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Game Officer amenitoa ushamba ni kuhusu FISI DUME NA JIKE

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chongombili, Oct 28, 2012.

 1. C

  Chongombili Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 26, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa muda mrefu nimekuwa nikihangaika kujua kama kuna fisi dume na jike kama watu wengi wanavyoamini kuwa FISI ana maumbile ya kike na dume. Nilijaribu kupita na kuuliza kwa wataalam wanaofanya kazi ktk HIfadhi za taifa na mapori ya akiba lakini wengi wamekuwa wakinipiga kalenda kuwa watanieleza baadaye na wengine kunijibu bila ufafunuzi wowote. Ktk pitapita mtaani nikakumbana na kijana (GO) mmoja mtaribu, mpole anayefanya kazi ktk moja ya Pori tengefu mkoani Arusha. Nilimuuliza swali hili na kunijibu kwa urefu akiwa anachanganya kidogo na kimombo. Maelezo yake yalikuwa hivi:- ktk Afrika tuna aina 3 fisi, kahawia, miraba na madoa. Kuna fisi dume na jike lakini fisi madoa (spotted hyena) amekuwa akiwashanganya watu kushindwa kutofautisha dume na jike na hivyo wa2 wengi kuamini kuwa fisi huyo ni Huntha (kiumbe chenye mifumo yote ya uzazi wa ke na me). Fisi huyu siyo huntha bali maumbile ya nje (vagina na penis) zinafanana. Fisi huyu jike hana lile tundu k...m... bali kiungo chake (kinembe) kimerefuka na kufanana kabisa na ya dume penis. Anasema siyo rahisi kutofautisha labda umkamate na kumchunguza. Alisema tafouti ni kwenye ncha ya dume imechongoka kidogo wakati ya jike ncha yake ni kama flat vile ya kinembe kipo blunt. Kinemba hicho anatumia ktk shughuli zote muhimu(kuzaa,kujamiana na kukojoa). Fisi huyu ametuchanganya zaidi kwa kuwa na kiungo (vaginal labia) yaani mashav ya k..m.. Iliyofanana na korodani (testicles) ya dume. Afisa elinielimisha kuwa tofauti ya fisi huyu jike ni umbo la kike kubwa kuliko dume, matiti ya jike ni makubwa hasa wakati wa mimba au wakiwa ananyonyesha. Pia alisema jike ni shari kuliko dume. Hayo ni maelezo machache ktk mengi aliyenipa afisa huyo na kiukweli amenipa ufahamu kuhusu utata wa fisi dume na jike. Kwa mwenye ufahamu zaidi tafadhali tupia humu tuelimike. Karibuni
   
Loading...