Gambo: Twambieni Hifadhi ya Burigi Chato imeingiza kiasi gani?

Hifazi zote zina faida na bado tunatakiwa kuyapandisha hazi mapori tengefu, Tatizo ni Serikali kutoruhusu wawekezaji kwenye hizo hifadhi, na makodi makubwa na mengi, na hakuma matangazo hizo ndio shida kubwa, Hifazi ya Chato na zingine ni zahabu, Wajaribu kutoa hayo makodi, uone kama hujaona private jeti zikitua chato,nyerere np, ruaha, kila mahali, Dar es salaam ni Jiji ambalo unaweza libadilisha ndani ya mies 6 likapokea watalii milioni kumi kwa mwezi, Tanga, Mtwara kila mahali ni pesa, weka Watu wawekeze, ruhusu Ndege zitue, punguza makodi, alika hotel Kubwa kuwekeza, weka usalama wa kutosha, ondo sheria mbovu za pesa, ruhusu Kampuni wajende majumba ya kupangisha watu/office. ni Rahisi sijui hawa viongozi wanashindwa nini kufanya kazi Ndogo kama hii.
Amka amka toka kwenye huo usingizi uokufanya unaota vitu usivyovijua.
 
Akishajia then inamsaidia nini wakuu. Hiyo sii ni mbuga ikiingiza hela au kutoingiza hela serikali inapungukiwa nini. Hili ndio tatizo la ukosefu wa elimu ya uelewa Tanzania.
Unaelewa kweli kinachozungumzwa hapa.Kwahiyo kwa akili zako unaona ni sawa uwe na kitu kinachochukua gharama kubwa kukiendesha bila faida wakati kimsingi kilipaswa kizalishe kwa faida na kijiendeshe.
 
MBUNGE wa Arusha Mjini, Mrisho Mashaka Gambo ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya ukaguzi wa Hifadhi zote za Taifa na kupeleka ripoti bungeni kuhusu watalii wanaotembelea kila hifadhi na kiasi cha pesa kinachoingizwa na kila hifadhi kutokana na utalii huo.

Gambo amesema hayo leo Ijumaa, Juni 4, 2021, wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bungeni jijini Dodoma huku akiitaja Hifadhi ya Burigi Chato iliyopandishwa hadhi na Hayati Dkt. John Magufuli kuwa hifadhi ya taifa.

“Kwenye taarifa ya Waziri anasema hapa kuwa utalii unachangia pato la taifa kwa asilimia 17 na fedha za kigeni kwa asilimia 25, mimi nadhani taarifa ya Waziri ni ya zamani sana kwa namna ambavyo janga la corona limeathiri sekta ya utalii nchini na duniani kote.

“Ukiangali taarifa yake amesema hadi Aprili mwaka 2019 target ilikuwa kukusanya Tsh bil 584 na sisi tumekusana Tsh bil 89 ambayo ni sawa na asilimia 15 tu.

“Mchango wa utalii kwa GDP umeshuka kutoka kutoka asilimia 17.5 mpaka asilimia 11.5 na bado wamepandisha tozo za utalii wakati nchi nyingine za Afrika Mashariki zimeshusha. Dunia nzima inatoa ahuweni kwenye utalii lakini sisi tunaongeza gharama Mimi naona bado kuna kazi ya kufanya

“Ninashauri tupitie hifadhi zote za Taifa especially ya Burigi Chato, mlete hapa mtuambie imepokea wageni wangapi na imeingiza kiasi gani na inatumia gharama kiasi gani kuendeshwa, sio tunaanzisha hifadhi nyingi na gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa kwa sababu utapeleka watumishi kule utawalipa, gharama hizi unakuwa mzigo kwa mtalii ndio maana tunapandisha tozo kila mara.

“jambo jingine, ukienda Kenya, kupima corona ni dola 30 kwa hospitali za Serikali na dola 50 kwa hospitali private lakini hapa kwetu ni dola 100, sasa najiuliza kwani corona nayo ni fursa? Kituo cha kupimia corona (maabara) tuncho kimoja tu. Hili jambo inabidi tuliangalie upya,” amesema Mrisho Gambo.
Gambo anashangaa nini? Corona ni fursa ndiyo! Hivi mnadhani mabeberu wanatukomalia kupima corona na kuchanja unadhani wanatupenda sana au? Ni fursa, wanataka kupiga pesa!! Tena wanalazimisha!!
Mimi nashauri anayetaka kupima kwa hiari na hana safari ya lazima kwenda nje ya nchi atozwe dola 500. Ila yule anayelazimika kupima ili kutimiza masharti ya kusafiri je ya nchi alipe dola 50.
 
Unaelewa kweli kinachozungumzwa hapa.Kwahiyo kwa akili zako unaona ni sawa uwe na kitu kinachochukua gharama kubwa kukiendesha bila faida wakati kimsingi kilipaswa kizalishe kwa faida na kijiendeshe.
Wewe ndio huelewi ambaye unapenda kujadili vitu vyisivyo na msaada kwako.
 
Ni sahihi alivyouliza lakini pia kama lengo ni kukuza na kuongeza vivutio vya utalii ni lazima tubuni vipya, kuboresha vilivyopo na kuvitangaza kama ilivyo kwa Burigi chato.
Sasa sijui kivip hapo JPM alikosea kama comment za wengi zilivyo. Chuki tu
Vya sasa tuu vimekushinda hivyo vipya wewe vinakusaidia nini?
 
Gambo yuko very smart kichwani.

Kuna kipind siasa za chuki zilitakakuharibu kichwa chake

Ana hoja ya msingi
Wabunge wengi waliotokea kwenye utumishi wa umma huwa wapo vizuri,swma ile uchama ndio unawakaba akili zinakuwa 2.
 
Huyu ni Gambo Gani,
Ni Yule Ambae Aliagiza Pesa Za Lambi lambi kwenye Ajali Ya Luck Vicent School Zisiende Kwa Family Bali Sikarabati Hospital??.
Ni yule yule anaenda na upepo ili aambulie angalau uwazari wa mazingira kama siyo naibu,maana ukimponda Mwendazake unajiweka Pazuri.
 
Back
Top Bottom