Gambia, Gololi hutumika kuchagua Rais wa nchi

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,141
13,215
Huenda Jambo Kubwa sana ulilojua kuhusu uchaguzi wa Gambia ni Kuondolewa kwa Kiongozi Nguli wa Nchi Hiyo Yahya Jameh na sana kama unafuatlia medani za siasa katika duru la Kimataifa utagundua pia kwamba Gambia ilikataa katu kuruhusu waangalizi wa umoja wa Ulaya bila kutoa sababu zozote
849x493q70ISS-Jammeh-marbles.jpg


UCHAGUZI wa Taifa dogo la Afrika Magharibi la Gambia lililopo kilometa chache ukingoni mwa Jangwa la Sahara, uligubikwa na mvuto wa kipekee kutokana na wasifu wa wagombea wawili waliochuana vikali. Rais aliyebwagwa katika uchaguzi huo, Yahya Jammeh, aliyetawala kwa miongo miwili na ushei aliyeingia madarakani kwa Mapinduzi ya kijeshi amekubali kushindwa na kuahidi kukabidhi madaraka kwa amani kwa mpinzani wake aliyeshinda, Adama Barrow, ambaye hajawahi kuongoza katika ngazi yoyote ya kisiasa.
161201154325-gettyimages-626665158-super-169.jpg


Wagombea wote wawili wanawiana kwa umri (miaka 51) ambapo Jammeh aliyeingia madarakani kwa Mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu mwaka 1994 alijipatia asilimia 36 ya kura zote zilizopigwa, Barrow alijipatia asilimia 45 na mgombea wa tatu Kandeh alijipatia asilimia 17.8.

Pengine matokeo hayo yaliyopokewa kwa nderemo na vifijo si kivutio kikubwa zaidi cha uchaguzi, lakini ni mfumo mbadala wa Taifa hilo katika kupiga kura unaotofautiana na mataifa mengine kwa kutotumia kadi za kupiga kura bali kinachotumika ni gololi zisizokuwa na rangi wanazotumbukiza wapiga kura katika pipa lenye rangi inayomwakilisha mgombea wanayetaka kumchagua.
_42116860_drumone.jpg
_42116862_marbles203.jpg

Kuanguka kwa gololi hiyo ndani ya kitako cha pipa na kutoa sauti ya kugonga humwezesha msimamizi wa uchaguzi kutambua endapo mpiga kura yeyote atajaribu kupiga kura zaidi ya moja anayopaswa kutumbukiza. Ni mfumo ulioanza kutumika mwaka ambao wagombea Jammeh na Barrow walizaliwa (1965), kutokana na kiwango duni cha elimu miongoni mwa Wagambia wengi ambao wasingeweza kutumia mfumo uliozoeleka unaohusisha kuandika.
(Asilimia 49 ya Wagambia hawajui KUSOMA WALA KUANDIKA PIA)

WEB_PHOTO_Gambia.jpg

Kutokana na upande wa chini kwa ndani ya pipa kutoa sauti inayorandana na kengele ya baiskeli siku ya kupiga kura hairuhusiwi kuja na baiskeli katika kituo cha kupiga kura ili kutosababisha mkanganyiko. Mapipa hayo huwekwa sanjari ili isiwezekane kuinua mojawapo na kubaini matokeo kabla ya kuhesabiwa kutokana na uzito kwa wingi wa gololi, kila pipa hupakwa rangi ya chama cha mgombea na kuwekwa jina la chama anachowakilisha na picha ya mgombea.
2011112581850380734_20.jpg

Baada ya kupiga kura mpiga kura huchovya kidole katika wino kuthibitisha kuwa ameshiriki katika kupiga kura. Katika kuhesabu kura gololi hizo huwekwa kwenye ubao wenye vishimo kati ya 200 hadi 500 ili kurahisisha kazi ya kuhesabu.
31107459191_f87d62a9af.jpg

WEB_PHOTO_Gambia.jpg
 
Kweli nzuri ndio maana rais hakuleta shida kama kina Fulani kwenye nchi fulani
 
Yaani bavicha hamjui mnachokitaka kwa sababu umeshaambiwa wagambia asilimia 49 hawajui kusoma mnataka ije tanzania
hiyo yenyewe ya karatasi kwa Tanzania uchaguzi unafanyika kutimiza ilimradi

hata upinzani wakishinda matokeo yanapinduliwa
 
Mleta uzi makala yako nzuri sana, nimeipenda kwa kweli.

Faida ya huo mfumo:
-Hakuna habari za kula kualibika

Changamoto za huo mfumo:
-Hakuna usiri katika upigaji kura so unapo elekea kwenye pipa la kijani au njano kila mtu aliyepo kituoni anakuona unaye enda kumpa kura. Mfumo wa namna hiyo kwa eneo lenye siasa za chuki kama Zanzibar ni hatari zaidi.
-Na inawezekana hii system ni janja ya watawala kudhibiti watu wakati wa kuchagua. Wananchi wenye uelewa mdogo na wanyonge lazima watahofia kwenda kudumbukiza gololi zao kwenye pipa la upinzani huku akitazamwa na polisi, wanajeshi na wasimamizi wa uchaguzi wanaoletwaga na serikari.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom