GAMBIA: Aliyewakuwa "Miss Gambia" amtuhumu aliyekuwa Rais, Yahya Jammeh kwa kumbaka

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
1572610972165.png

Aliyewahi kuwa Mrimbwende wa Taifa la Gambia. Fatou Jallow ametoa yuhuma hizo mbele ya Tume ya Ukweli na Maridhiao

Amesema kuwa Jammeh alimlazimisha amkatae mchumba wake ambaye walipanga kuoana

Yahya Jammeh aliikimbia nchi hiyo, Januari 2017 baada ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu na kukataa kutoka madarakani

Mataifa ya Afrika Magharibi yaliingilia kati na Jammeh kutorokea Guinea Ya Ikweta ikiwa ni baada ya kukaa madarakani tangu mwaka 1994

======
A Gambian former beauty queen on Thursday accused former President Yahya Jammeh of raping her to punish her for rejecting his marriage proposal, in evidence to the country's truth and reconciliation commission.

"What he wanted to do was to teach me a lesson, what he wanted to do is manifest his ego," Fatou Jallow said.

"There were words like 'who do you think you are?', that he is the president and that he gets any woman that he wants," Jallow told Gambia's Truth, Reconciliation and Reparations Commission (TRRC).

Jammeh fled the country in January 2017 after losing presidential elections and initially refusing to step down.

power in a bloodless coup in July 1994 and was repeatedly re-elected in disputed circumstances until being defeated in December 2016 by the relatively unknown Adama Barrow.

After other West African states intervened, he fled into exile in the central African state of Equatorial Guinea.
The TRRC was set up to review abuses under Jammeh.

-Daily Monitor-
 
Malkia wa urembo nchini Gambia amemshutumu Rais wa zamani wa taifa hilo Yahya Jammeh kwa 'kumbaka' baada ya kukataa kufunga naye ndoa.

Akitoa ushahidi kwa tume ya maridhiano na ukarabati, Fatou Jallow alisema kwamba rais Jammeh alimnyanyasa kingono katika chumba kimoja ili kumuadhibu.

Tume hiyo ilibuniwa ili kuchunguza madai ya unyanyasaji dhidi ya Jammeh wakati wa kipindi chake cha utawala wa miaka 22.

Ushahidi wa Bi Jallow ulikamilisha kikao cha wiki tatu kilichoangazia udhalilishaji wa kingono.

Ushahidi wake ni miongoni mwa ripoti ya shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch ambayo inaelezea madai mengine ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono uliotekelezwa na bwana Jammeh.

BBC ilijaribu kuwasiliana na bwana Jemmeh ambaye kwa sasa anaishi mafichoni Equitorila Guinea, kuhusu madai hayo.

Awali msemaji wa chama chake cha APPR alikana madai hayo yaliyotolewa dhidi ya bwana Jammeh.

''Sisi kama chama na raia wa Gambia tumechoka na msururu wa madai ambayo yameripotiwa dhidi ya rais wa zamani'', alisema Ousman Rambo Jatta katika taarifa iliotumwa kwa BBC.

"Rais huyo wa zamani hana muda wa kujibu uongo na kampeni za kumuharibia jina. Ni mtu anayemuogopa Mungu ambaye anaheshimu sana wanawake wa Gambia'', alisema naibu wa kiongozi wa chama hicho cha APPR.

Bi Jallow alisema kuwa alikuwa na umri wa miaka 18 wakati alipokutana na Jammeh baada ya kushinda shindano la malkia wa urembo wa 2014 katika mji mkuu wa Banjul.

Miezi kadhaa baada ya kupata taji hilo, anasema kwamba Rais huyo wa zamani alijifanya kama mzazi wakati alipokutana naye akimpatia ushauri, zawadi na fedha na kuandaa maji kupelekwa katika nyumba yao ya familia.

Na katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na msaidizi wa rais huyo , anasema alimuuliza iwapo wangeoana.

Alikataa wazo hilo mbali na zawadi alizokuwa akipatiwa.

Bi Jallow anasema kuwa msaidizi huyo baadaye alisisitiza kwamba anafaa kuhudhuria sherehe ya kidini katika ikulu ya rais kama malkia wa urembo mnamo mwezi Juni 2015.

Lakini alipowasili, alipelekwa katika makazi binafsi ya Rais huyo. Bi Jallow anasema alipigwa kofi na kudungwa sindano katika mkono wake.

Alipokuwa mjini Dakar mji mkuu wa Senegal, Bi Jallow alitafuta usaidizi wa mashirika kadhaa ya haki za kibinadaamu.

Wiki chache baadaye alipatiwa ulinzi na kupelekwa nchini Canada ambapo amekuwa akiishi tangu wakati huo.

Shirika la Human Rights Watch (HRW) na Trial International yanasema kuwa bwana Jammeh alikuwa na mfumo wa kunyanyasa wanawake, ambapo wanawake wengine walikua wakilipwa mshahara na serikali na kufanya kazi katika ikulu kwa jina 'wasichana wa itifaki'', ambao walikuwa wakifanya kazi za ukarani lakini umuhimu wao mkubwa ulikuwa kushiriki ngono na Rais.

Mwanamke mwengine ambaye aliajiriwa kama afisa wa itifaki akiwa na umri wa miaka 23 alilazimishwa 'kushiriki' ngono na bwana Jammeh mwaka 2015.

Mwanamke huyo ambaye aliomba kutofichuliwa jina, alisema kuwa siku moja Rais huyo alimwita chumbani mwake: ''Alianza kunivua nguo na kusema kuwa alikuwa ananipenda, angenifanyia chochote ningetaka na familia yangu, na kwamba nisiambie mtu yeyote na iwapo nitakiuka hilo nitakiona cha mtema kuni''.

Bwana Jammeh alitoroka Gambia 2017 baada ya kukataa kustaafu kufuatia kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais. Kwa sasa anaishi mafichoni nchini Guinea ya Ikweta.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hahaha wasichana wa itifaki
By the way hiyo ni kawaida kwa madikteta ukute hata huyo binti alikubali mwenyewe,
Kuna jamaa aliitwa omar bongo,yeye alimpeleka binti chumbani akabonyeza remote kitanda kikaibuka
 
Aliyewahi kuwa Mrimbwende wa Taifa la Gambia. Fatou Jallow ametoa yuhuma hizo mbele ya Tume ya Ukweli na Maridhiao

Amesema kuwa Jammeh alimlazimisha amkatae mchumba wake ambaye walipanga kuoana

Yahya Jammeh aliikimbia nchi hiyo, Januari 2017 baada ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu na kukataa kutoka madarakani

Mataifa ya Afrika Magharibi yaliingilia kati na Jammeh kutorokea Guinea Ya Ikweta ikiwa ni baada ya kukaa madarakani tangu mwaka 1994

======
A Gambian former beauty queen on Thursday accused former President Yahya Jammeh of raping her to punish her for rejecting his marriage proposal, in evidence to the country's truth and reconciliation commission.

"What he wanted to do was to teach me a lesson, what he wanted to do is manifest his ego," Fatou Jallow said.

"There were words like 'who do you think you are?', that he is the president and that he gets any woman that he wants," Jallow told Gambia's Truth, Reconciliation and Reparations Commission (TRRC).

Jammeh fled the country in January 2017 after losing presidential elections and initially refusing to step down.

power in a bloodless coup in July 1994 and was repeatedly re-elected in disputed circumstances until being defeated in December 2016 by the relatively unknown Adama Barrow.

After other West African states intervened, he fled into exile in the central African state of Equatorial Guinea.
The TRRC was set up to review abuses under Jammeh.

-Daily Monitor-
Alikuwa anamtosa Rais.
 
viongozi waafrika wengi ni wajingajinga. Sasa huyu alikuwa mganga hivyo vitendo si ajabu. Hivi viongozi wakiwa wajinga kama huyu, Zuma etc, inamaanisha wananchi wao wakoje?
 
Uislam safi unaupatia wapi ikiwa unabaka

Ukibaka automatically unaweza kua muislam sawa ila sio safi na wala hujijui kama ww ni muislam maana kama unajijua usingebaka

Pointless
Si alikua na mpango wa kuigeuza Gambia kua nchi ya kiislam?
 
Back
Top Bottom