View attachment 30576
Nasikia huko mtaani kitabu hiki cha Professor Euphrase Kezilahabi kinasakwa kama almasi kila mtu anataka kukisoma yaelekea humu ndo kuna gamba halisi la nyoka eeeh.....!
Hiki kitabu, kilinikuza kifikra na kutokana na kitabu hiki ndiyo maana nikaamua kujiita Gamba La Nyoka!, kusema kweli muandishi alifanya kazi nzuri sana kwenye hiki kitabu.
Katika hiki kitabu kuna mzee mmoja anaitwa Mzee Chilongo, yeye anapinga juhudi za maendeleo kwa hoja za ajabu ajabu kwa kudai eti " kuna haja gani ya kujenga vyoo wakati kijiji kimezungukwa na mapori?".hahah.
Katika hicho kitabu kuna vijana wamemaliza chuo kikuu, wanataka kuleta theory walizofundishwa darasani katika maisha ya kawaida ya kila siku, wanakuja kukuta kumbe hali halisi ni tofauti kabisa!
Ni kitabu kizuri kwelikweli, kama wewe ni greatthinker anayetaka kuelewa jamii ya Kitanzania imetoka wapi, ni vyema ukakisoma kitabu hiki, Mwandishi pia aliandika kitabu kinachoitwa "Dunia Uwanja wa Fujo".