Galila: CCM ya leo haitakubali mizengwe ya uchaguzi ndani ya chama

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Kutoka Shinyanga Mjini,

Naibu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Galila Wabanh'u amewasili mkoani Shinyanga kwa ziara ya siku moja ambapo atakutana na mabaraza ya jumuiya ya Wazazi na UVCCM.

Aidha,wakati wa kuzungumza na viongozi wa chama na jumuiya zake katika kikao cha ndani Ndugu Galila amehimiza umoja na mshikamano ndani ya chama hususani wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu kwani hiyo ndio siri ya ushindi wa CCM.

Pia amewakumbusha viongozi na vikao vya chama kujiepusha na siasa za mizengwe, fitna, rushwa na makundi badala yake upendo na haki viwe mbele daima ili kuleta amani na utulivu miongoni mwa wanachama na chama chenyewe.

"Niwahakikishie kama yupo kiongozi anapanga kumchezea rafu mwanachama yeyote wakati wa mchakato wa uchaguzi ndani ya chama asithubutu maana atakuwa anachezea moto. Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa Ndugu John Pombe Magufuli na katibu mkuu wetu Ndugu Bashiru Ally wanataka demokrasia, haki na usawa vionekane kutendeka kwani huo ndio msingi wa CCM."

Mwisho, Ndugu Galila aliwataka viongozi na wanachama wa CCM kuendelea kuyaeleza mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015-2020 unaofanywa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ambaye amedhamiria kwa dhati kuijenga nchi yetu.

Ndugu Galila aliambatana na Ndugu Chollaje katibu oganaizesheni jumuiya ya Wazazi Taifa.

#UchunguWaMwana #AujuayeMzazi
#MagufuliChaguoLetu
#MaamuziYetuCCM2020

IMG-20200128-WA0042.jpeg
IMG-20200128-WA0038.jpeg
IMG-20200128-WA0037.jpeg
IMG-20200128-WA0035.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anawasanifu wenzake na kupandikiza hofu. Ukweli ni kuwa watakaopitishwa ni wale wanaomuunga au wanaotakiwa na mwenyekiti wa CCM na genge lake fullstop. Hapo anawatisha ili atakayepitishwa na hilo genge la mwenyekiti akubalike bila msuguano.
 
Kwa hiyo sisi tufanyeje? Waende wakaparurane huko ni bora uchaguzi wa simba, kifaru, kiboko, mamba, Buffalos kuliko mtifuano utakaotokea ktk uchaguzi na uteuzi wa ndani ya chama hiki NAONA WABABE WA CHAMA AMBAO NI WAOGA KULIKO KUNGURU NA SHORWE WANDA WAMEANZA KUWAPIGA BITI WENZAO KWAMBA WASIWABUGHUDHI HAKIKA WANAJIDANGANYA WATAPIGWA KIPIGO CHA MBWA KOKO
 
Back
Top Bottom