Gairo sasa kupata maji safi na salama mwishoni mwa mwezi wa 3 2019

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe, amewahakikishia wananchi wa Gairo kuondokana na tatizo la ukosefu wa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mtambo wa kuchuja chumvi.
GAIRO-2-2132308419-1550735611142.png

Mtambo wa kuchuja chumvi kwenye maji

Mkuu wa Wilaya amesema kuwa mtambo huo ambao unatengenezwa nchini Italy unatarajiwa kukamilika mwezi machi 2019.

Kwa upande wao Wenyeviti wa Serikali – Vitongoji vyote vya Mamlaka ya Mji Mdogo Wilayani Gairo,wamemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa hela kiasi cha shilingi bilion 2 kwa ajili ya mradi wa maji wilayani humo.

Mtambo huo utakaogharimu Bilioni 2 pesa za Kitanzania utasaidia kuondoa tatizo la maji katika Wilaya hiyo na wananchi wamemuomba mkuu wa Wilaya Mchembe, kuhakikisha Mamlaka ya maji ya Mkoa wa Morogoro(MORUWASA) kuanza kuhakiki mambomba na miundo mbinu ya mradi huo.

Mhe. Mchembe aliwaomba Wenyeviti wote wa Vitongoji kuhakikisha wanapitia maeneo ya kuunganisha maji kwenye mitaa yao ili kuhakikisha kama kuna changamoto zinafanyiwa kazi mapema.
 
Baada ya Miaka zaidi ya 50 ndio mna wwkumbuka leo ?.Akili yangu hainipi kuwa Serikali ilikosa Billion 2 za kuwezesha Mradi kama huu ,ili kuhakikisha Afya za Wananchi wake zinakuwa Salama..Hii Aya hapa inaonesha ni kwa namna gani Wananchi wana fikiri zaidi ya Watawala ;

Mtambo huo utakaogharimu Bilioni 2 pesa za Kitanzania utasaidia kuondoa tatizo la maji katika Wilaya hiyo na wananchi wamemuomba mkuu wa Wilaya Mchembe, kuhakikisha Mamlaka ya maji ya Mkoa wa Morogoro(MORUWASA) kuanza kuhakiki mambomba na miundo mbinu ya mradi huo.
 
Safi sana.......

Baada ya kilio cha muda mrefu cha wakazi wa wilaya hiyo ya Gairo kuhusu tatizo hilo la Maji, hatimaye kilio chao kimesikika
 
Back
Top Bottom