Gagulo hadharani

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Kituko kimetokea Iringa, ambao Francis Godwin anaripoti katika blogu yake kuwa ilimlazimu mrembo mmoja kukimbilia katika studio za Photo Next katika stendi ya mabasi ya Miyomboni ili kujinusuru na kundi kubwa la watu waliokuwa na azma ya kumchania nguo zake kutokana na kuvaa nguo za ndani (gagulo) nje.

Nguo ambayo aliivaa iliuacha mwili wake nusu uchi, kitendo kilichowakasirisha wananchi walioamua kuanza kumfukuza kwa lengo la kuitaka kuichana nguo hiyo ili ahttps://www.jamiiforums.com/template/JamiV1/default/editor/insertimage.pngtembee uchi kabisaa!

Polisi walimwokoa mrembo huyo ambaye alipewa upande wa kanga na mwanamke mwenzake ili ajisitirie.

Ati mrembo huyo ni Mtanzania aliyeishi sana Uingereza na hufika Iringa kufanya kazi katika Benki moja.

Baadhi ya wanawake waliokuwepo katika tukio hilo walidai kuwa pamoja na kuwa hawaungi mkono hatua ya vijana hao kutaka kumchania nguo mrembo huyo ila bado wao kama wanawake wamesikitishwa na mavazi ya mrembo huyo nakuwa mavazi hayo yalipaswa kuvaliwa clab usiku sio mchana.

1268887_orig.jpg
 
Hao watu wa Irringa wanalao jambo, mbona ukifika kwenye vibanda vya video wamejazana kuangalia picha za ngono? sasa wanapoona live mbona wanajifanya watakatifu? acheni watu wavae wanavyotaka!
 
Haya bana.......
Hao watu wa Irringa wanalao jambo, mbona ukifika kwenye vibanda vya video wamejazana kuangalia picha za ngono? sasa wanapoona live mbona wanajifanya watakatifu? acheni watu wavae wanavyotaka!
 
Haahahaaaahaaaa:tonguez:GAGURO njee mie nilidhani kalivaa ndani ya sketi au gauni ila limeovateki nguo ya nje!! Kumbe kaipiga gaguro yenyewe kavukavu??!!!! Ana bahati walikuwa hawajapata ULANZI; WANGEMNYONGA Wanyalu hawataki mchezo!!!!!
 
Haahahaaaahaaaa:tonguez:GAGURO njee mie nilidhani kalivaa ndani ya sketi au gauni ila limeovateki nguo ya nje!! Kumbe kaipiga gaguro yenyewe kavukavu??!!!! Ana bahati walikuwa hawajapata ULANZI; WANGEMNYONGA Wanyalu hawataki mchezo!!!!!

Likiovateki nguo ya nnje rasmi limavaliwa style ya PHD ie Petticoat Hanging Down,kinadada tunaweza werraaaa!
 
hata hapa Dar inatakiwa sana. Yaani kama vile watu wanavyomkimbiza mwizi ndiyo wakimbizwe hao madada waliokwisha poteza mwelekeo wa kimaadili. wahusika toeni ruhusu ya kuzuia wimbi kubwa la wadada wanaopoteza utu kwa kutembea uchi
 
Haahahaaaahaaaa:tonguez:GAGURO njee mie nilidhani kalivaa ndani ya sketi au gauni ila limeovateki nguo ya nje!! Kumbe kaipiga gaguro yenyewe kavukavu??!!!! Ana bahati walikuwa hawajapata ULANZI; WANGEMNYONGA Wanyalu hawataki mchezo!!!!!
ni kama unavyo liona hapo chini
1268887_orig.jpg


6341811_orig.jpg
 
sasa huyu ni mrembo au ni malaya tu ambae hata thamani ya mwili wake haijuwi tena, huyo ni changu.
 
Masikini.....halafu usoni anaonekana decent tu! Pengine sio gagulo (material/texture yake inonekana ngumu!) kwa maana yake ila ni aina tu ya gauni akaweka na koti kwa juu! Hata hivyo hakufanya uamuzi wa busara (hasa kwa mji mdogo kama Iringa)!
 
...Tatizo la watu kukosa kazi! Angalia hiyo nguvu kazi yote inayomfuata huyo mwanamke na kumzomea ati kwa kuwa kavaa nguo INAYOFANANA na nguo ya ndani! Wote hao kila mtu angekuwa bz na kazi yake wangeishia kumuangalia tu,
kumdharau na kuendelea na kazi zao!
 
Ila kazidisha kweli...kama kagauni ka kulalia vile!!Ukivaa hivi atleast uwe ndani au kwenye gari muda mwingi sio unakata mbuga mtaani!
Pole yake!
 
Du na watanzania kwa kushobokea mambo madogo? cheki hilo nyomi, wote wamesimamisha kazi zao kisa mrembo kavaa kimini.

We still have a long way to go. Lawama zote kwa JK.
 
ni kama unavyo liona hapo chini
1268887_orig.jpg


6341811_orig.jpg

Kuna hako kajamaa nyuma ya huyo dada kalikovaa shati kubwa bila kufunga vifungo,kanaweza kuwa kabakaji serikali ikawekee ulinzi maalumu ikibidi ule wa marehemu Shekhe yahaya. Yaani kanatolea macho mapaja ya huyo dada mpaka kanasinzia
 
Ndio tuone athari ya umagharibi inavyoathiri watu wetu.nenda pale chuo kikuu mlimani,uone zaidi ya hayo.tena hao ni wasomi ambao jamii inaamini kuwa kwa kutumia elimu yao wana nafas kubwa ya kuchagua tamaduni bora ya kufuata.binafs nishaona had maeneo nyeti ya binti tena ilikua chumba cha mtihan pale nkurumah hall,ilibid nimwambie invigilator anihamishe,alipokataa nkamwonesha nae aone.akamfata binti ili akae vizuri,lakin kwa vle nguo yake ilikua haijai hata kiganjan,kila alivyojitahd kukaa vzr ndivyo alvyozid"kumwaga radhi".je unadhan pamoja na yeye kuwa huru kuvaa anavyojisika,je amewatendea haki wengne{watazamaji}?
 
Miguu kama mwanariadha? Watu hao wanahitajika huku bongo watufundishiie adabu wale wanaume wanaovaa mlegezo na hao mafuska wanaovaa vimini vilivyopitiliza.

Nimegundua kitu kimoja hata wazazi wetu hawana maadili kama unaweza kumwacha mwanao anatoka ndani hivyo kama huyo msichana ni hatari sana.

Pole yake wangembaka hao ooooh!
 
huu ni uonevu na unyanyasaji wa kijinsia. Mbona sie mibaba mizima inatembea vifua wazi na vijikaptula hatupigiwi kelele. na huko Iringa wazungu wapo na wanatembea hivyo kwanini wasifanyiwehivyo kama kweli ni haki
 
Back
Top Bottom