Gadgets zimewapotezea watoto uwezo wa kuandika kwa mkono

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,266
Dunia ya utandawazi imerahisisha sana elimu. Siku hizi mtoto kujua jina la mji mkuu wa Zambia hahitaji kusoma vitabu library, ana Google tu search engine inampa jibu.

Pamoja na hayo matumizi ya computer, smart phones, tablets nk yamepunguza uwezo na ushawishi wa vijana na watoto kuwa na mwandiko mzuri au hata kujua kuandika kwa mkono.

Mtoto wako akifika umri wa miaka miwili, mnunulie mkasi wa plastic, mtoto akiweza kushika mkasi na kuutumia hatopata shida kushika kalamu.

Akifika miaka 3.5 - 4 anza kumpa maneno ya kurudia kuandika akianza na jina lake na mahali anapoishi. Hii ya kumfundisha mtoto kujua anapoishi itamsaidia pia akipata majanga ya kupotea.

Kuna watoto miaka saba hawajui wanaishi wapi, akipotea inabidi usubiri kuona sura yake kwenye luninga.

Wazazi tuna jukumu la malezi bora kwa watoto wetu.
1576025755530.jpeg
 
Nilikuwa nakerwa sana mwanangu alichukuwa muda kujua anaishi wapi na jina lake halisi.
 
Weunasema watoto waupanga na masaki huko osterbay huku mwananyamala ipad aipate wapi na baba Ana Tecno sio watoto woote Wamelelewa hivyo ndio maana kuna st.kayumba
 
Weunasema watoto waupanga na masaki huko osterbay huku mwananyamala ipad aipate wapi na baba Ana Tecno sio watoto woote Wamelelewa hivyo ndio maana kuna st.kayumba
Watoto wa huku kwetu Kwamtogole wajua kuandika mahali anapoishi ni skill kubwa mkuu. Maana kile neno tu Kwamtogole.
 
Back
Top Bottom