Gaddafi (Qaddafi) yuko sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gaddafi (Qaddafi) yuko sahihi?

Discussion in 'International Forum' started by ZuluBoy, Sep 2, 2009.

 1. Z

  ZuluBoy Member

  #1
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani,

  Dear all members of the home of great thinkers,

  Naomba ufafanuzi toka kwa watalaamu wa maswala ya Political Science au yeyote mwana JF kuhusu kauli za Rais Wa Libya Muamar Gadafi.

  Akihutubia wakuu wa nchi za Afrika Mei mwaka huu, aliunga mkono maharamia wa kisomali na kusema waliibuka kutokana na Choyo ya Nchi Za Magharibi. Akasema maharamia wapo kazini kulinda unyonyaji dhidi ya Wasomali.

  Wiki hii kawaambia wakuu wenzake kwamba nchi zote za Afrika lazima zifunge balozi za Israel mara moja ili kupinga kile alichokiita uzandiki wa Nchi za Magharibi.

  Baada ya Vita ya Kagera, tukiwa katika oil crisis, nchi haina mafuta, alimkejeli Hayati Nyerere akimtaka ampe mateka wa kivita kwa kubadilishana na mafuta kama alivyofanya kwa Merghani. Nyerere alikataa akamwambia thamani ya binadamu haiwezi kulinganishwa na mafuta na badala yake akamrudishia mateka bure.

  Huyu Ndiye Shujaa wetu baada ya akina Nyerere na Mandela>
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna uwezekana anachosema Gadafi ni sahihi, lakini inategemea kwa mtazamo wa nani? Ukweli ni kuwa ukiangalia undani wa Tatizo la uharamia Somalia ni maisha magumu. Uharamia ni ajira, ni tofauti sana na ugaidi. Ukiangalia kwa undani utaona kuwa nchi za magharibi hazitaki Somalia iwe islamic state and a safe haven for terrorists. Wanafanikiwa kwa hilo lakini hawajui matokeo yake ni kuwa wasomali wanabaki jobless. Sasa kama ni baba ana wake 3 na watoto 18 atalea vipi. Na walivyowavivu wa kazi unategemea watafanya nini? Gadafi ana point, though he is not politically right!
   
 3. Z

  ZuluBoy Member

  #3
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani una point lakini, nini suluhisho la haya yote? Kwa nini hawataki Islamic State? Kwani Somalia wemejaribu kuwa jamuhuri ya Kiislamu ikashindikana? Kwa nini wasikae mezani makundi yote yanayo pingana ili waandae kura ya maoni ili kama kweli Islamic State ndio muafaka, then iundwe.

  Mashaka yangu ni kwamba Gadafi anazeeka na hata busara zake sasa zinatia shaka sana. Kwake anapiga kelele umagharibi lakini miaka mitano iliyopita baada ya kichapo cha Sadam, akasalimu amri na kusitisha silaha za Nyuklia. Tuliona mara ya Kwanza katika miaka 40 Condoleeza Rice anatembelea Libya. Swali kama yeye mwenye mafuta na jeuiri ya fedha kanyoosha mikono, wenzake anawashauri watunishe misuli kwa masalahi ya nani?
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  namsapoti Gadafi
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Sep 2, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Gaddafi: Israel 'Aids Africa Wars'

  Muammar Gaddafi, the Libyan leader, has said much of Africa's violence is due to foreign meddling, pointing the accusing finger at Israel.

  Gaddafi, who is also chairman of the African Union (AU), was speaking on Monday at a special summit of the group, which is coinciding with the celebration of the 40th anniversary of the coup that brought him to power.

  Israel is "behind all of Africa's conflicts", Gaddafi told about 30 African leaders gathered under a huge tent at Tripoli airport.

  "As African brothers, we must find solutions to stop the superpowers who are pillaging our continent," he said.

  Forward policy


  He demanded the closure of all Israeli embassies across Africa, describing Israel as a "gang" and saying it uses "the protection of minorities as an excuse to launch conflicts".

  Israel has acknowledged operating what it called a forward policy in Africa between the 1960s and 1980s, intervening in wars in Ethiopia, Uganda and Sudan.

  Gaddafi claimed that a Darfur rebel group had opened an office in Tel Aviv while its leader lives under French protection, a reference to Abdelwahid Mohammed Nur, the head of the Sudan Liberation Army who lives in exile in Paris, France.

  Al Jazeera's Amr El-Kahky
  , reporting from the Libyan capital, Tripoli, said: "Libya is portraying itself as opening up, but it is still holding to the same principle: which is anti-Israel feeling, and that is what we have heard from Colonel Gaddafi today, saying that people - the African nations - should shy away from the Israelis because they are the ones behind all the African problems."

  The celebrations come amid angry reaction from the US following a hero's welcome Libya granted Abdelbaset Ali Mohmet al-Megrahi, the 1988 Lockerbie bomber, who was freed from a Scottish prison last month on compassionate grounds.


  Fomenting bloodshed


  Gaddafi, the longest-serving leader in Africa and in the Arab world, has also been accused of fomenting bloodshed in the 1980s and 1990s across West Africa and the Sahel.

  The AU summit - the third so far this year - will mark the 10th anniversary of the 53-member pan-African organisation and is expected to tackle conflicts in Somalia and Sudan.

  "We'll try to focus on all conflict situations... We believe that we can move forward in terms of peace and discussions," Ramtane Lamamra, the AU's peace and security council chief said, singling out Somalia.

  Among the leaders present were Omar al-Bashir, the Sudanese leader facing an International Criminal Court (ICC) arrest warrant for alleged war crimes in Darfur, and Robert Mugabe, the Zimbabwean president.

  Several leaders expected to be present stayed away, including Jacob Zuma, the South African president, and Hugo Chaves, Venezuela's president.

  Gaddafi seized power at the age of 27 in a bloodless coup in September 1969, overthrowing the Western-backed government of King Idriss.
  Agency
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Sep 2, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Huyu Gaddafi hana hata aibu kuhusu mauaji ya Uganda chini ya nduli Idi Amin ambaye alimsaidia vifaa vya kivita ambavyo vilitumika kuua waganda wengi sana! Wakati majeshi ya Tanzania yalipoanza kupigana na Amin Gaddafi alidai hiyo ilikuwa eti ni vita dhidi ya UISLAMU! Aliyekuwa rais wa Sudan wakati huo Nimeiry naye aliunga mkono kauli ya Idi Amin! Kama kuna mtu wa kumlaumu kuhusu kusaidia mauaji ya kutisha huko Uganda namba moja ni Gaddafi mwenyewe! Na hizo nuclear ametengeneza kumwangamiza nani? Mbona mwenzake Nejad, rais wa Iran anadai eti kuwa na silaha za nuclear ni kinyume na UISLAMU? Pia atambue kwamba adui wa waarabu, Israel, sio adui wa waafrika. Wao wana macho na masikio ya kutambua adui yao ni nani na rafiki yao ni nani, sio mpaka watonywe na mzee aliyefanya sherehe ya kupindua serikali halali ya nchi yake!
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Sep 2, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mbona uwalaumu hao Wayahudi kwa kumsaidia Idd Amini kumuweka madarakani?
   
 8. O

  Omumura JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Daima nimekuwa nasisitiza kwamba Ghadafi kuna kitu anapungukiwa kichwani na siwaelewi viongozi wetu wa afrika walipata wapi ujasiri wa kumpa uenyekiti wa AU.Ana kauli ambazo ni very contradictory kwa ustaarabu wa ulimwengu wa sasa ambazo hazitakiwi kufumbiwa macho. Anyway, to me Ghadafi ni mtu wa hatari kabisa kuwahi kutokea katika sayari hii ya wastaarabu aliyejifunika kwa blanketi la mapinduzi lililojaa dawa ya usingizi iliyowalevya wananchi wake wakabaki kupiga chafya mfululizo na kumwimbia mapambio yanayomzeesha mwili na ubongo wake!
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Waafrika wengine hatukosi visingizio.
   
 10. S

  Shamu JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gaddafi kazungumza very good point; ni Waisrael ndiyo wanaosababisha matatizo ya Afrika. Western countires walikuwa wanaiblame China kuwa ndiyo tatizo; lakini ni wao nchi za Magharibi ndizo zilizosababisha matatizo ya Afrika. Western Countries wameitawala Afrika kwa miaka mingi kwa uendeleza utumwa, imperialism bila ya kujali utu wa mtu wa Afrika. Matatizo yote tuliyokuwanayo sisi Afrika ni kwa sababu hatuna foundation ya uongozi, uchumi nk. Wazungu walikuwa wanajenga nchi zao tu bila ya kujenga Afrika.
   
 11. S

  Shamu JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gaddafi anazungumza point. Acha jazba sa siasa.
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 1,987
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Waarabu wana malalamiko yao kuhusu western coutries. Africa hatutakiwi kuwa anti-west, tunaweza kuwa na utamaduni wetu na kukaribisha na kufanya kazi na kila mtu. Hakuna sababu za kufunga ubalozi wakati uchumi wa nchi zetu unaendelea. Jamani tuache malumbano angalia Asia ilivyoendelea kwa miaka michache hawana mambo ya anti west.
   
 13. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Definately u are right. wakati kuna wazungu na waasia wakitafuta riziki Africa waafrica nao wametapakaa pande zote ikiwemo na Israeli kutafuta maisha.kwa dunia ilivyo sasa binadamu wanapaswa kutumia diplomasia na siyo kufunga mabalozi kusuluhisha matatizo. Africa kila tatizo tunawalaumu wazungu mbona wao hawatulaumu kwa matatizo yao?Serikali yenyewe wasomali hawataki. Huku ni kukwepa wajibu. gadafi NAFIKIRI NI MVIVU WA KUFIKIRI.
   
 14. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,209
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Walipata pale pale walipopata wa kumpa Idi Amini Dada.
   
 15. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,634
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  He is my hero!
   
 16. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  matatizo mengi ya somalia ni ya kikabila (clan based clashes) ku blame west ni kisingizio tu, hawa magaidi wamechukua advantage ya kuchomeka dini kwasababu nchi haina uongozi so chaos tupu. Gadaffi ni muuaji na aliua watanzania wetu, alichangia sana vita vya kagera kwa kumsupport Idi Amin, inasikitisha kuna watanzania wanadhani Gaddafi ni shujaa wao.
   
 17. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #17
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  a

  wewe mtu mzima sasa..waisrael wamesababisha vp umaskini wenu..wazungu na waarabu waliowatawala angalau ukiwataja hao nitakuelewa..kwamba walileta ukoloni na kuchukua mali na kuzipeleka kwao..tena waarabu ndiyo washenzi sana maana wanajenga misikiti tu siku hizi..shule hawajengi wala hospitals..kama zipo chache sana..lkn vile waarabu wenyewe hawajasoma labda...waafrika mwapigana wenyewe...mwashika mitutu wenyewe..mtu kama gadafi ndiyo mshenzi..alimsaidia sana idd amin atupige sie leo aongea utumbo pale..nashangaa kikwete alikaa kimya badala ya kumzaba kibao..
   
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Sep 5, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Watu macho yanawatoka kutetea ukoloni mambo leo...!
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,474
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Did anyone listen to Qaddafi's speech at the UN? Did you notice the little book he was reading from?

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=VvOo5LK22sg[/ame]

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=QjjICLYDKlg[/ame]
   
 20. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  The long awaited Muamar Gadafi ndio anahutubia UN, amevaa nguo zake za asili kama kawaida na amebandika kifuani ramani ya Afrika which made me proud of him.

  Salamu na introduction yake ametumia mwamvuli wa African Union not sure if this is the required protocol. Anaonekana yuko all over the place, hotuba yake haina mtiririko, aidha hakujiandaa vizuri au ana jazba.
   
Loading...