Gaddafi na mkewe chupuchupu, mtoto na wajukuu wake waangamizwa

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
Gaddafi na mkewe chupuchupu, mtoto na wajukuu wake waangamizwa
seiful%20arabi%20g.jpg
Seiful Arabi mtoto wa dikteta Muammar Gaddafi kiongozi wa Libya pamoja na wajukuu wake watatu wameuawa kwenye mashambulizi ya ndege za Nato huko Tripoli, mji mkuu wa Libya. Taarifa zinasema kuwa, Kanali Muammar Gaddafi ameponea chupuchupu kwenye shambulio hilo. Vikosi vitiifu kwa Gaddafi vimeeleza kuwa, mashambulio hayo yamepelekea kuharibiwa vibaya kituo kimoja cha watoto mjini Tripoli. Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa, kwa akali watu 15 akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka tisa wameuawa, baada ya ndege za Nato kushambulia mji wa Misratah. Gaddafi amesikika akisema jana kwamba, hatong'atuka madarakani, amma yuko tayari kufanya mazungumzo iwapo vikosi vya Nato vitasimamisha mashambulizi yao. Hata hivyo majeshi ya Nato na hali kadhalika wanamapinduzi nchini humo wametupilia mbali pendekezo hilo la Gaddafi, na kusisitiza juu ya kung'olewa madarakani dikteta huyo.

Kwa hisani ya Idhaa ya Kiswahili ya Redio Tehran, Iran
 
simuungi mkono Gadafi lakini pia siungi mkono NATO na washirika wake. So paining kuona mwenzetu anaonewa viongozi wa kiafrika wameuchuna kimya hata kwa kuwakemea wazungu japo kwa mdomo tu. Duh!
 
Labda sijaelewa kidogo mbinu za medani katika vita. Simuungi mkono Ghadafi lakini Nato kwa nini wanapiga nyumba za makazi za Ghadafi?. Nilitarajia wapige vituo vya kijeshi na zana za kijeshi za Ghadafi ili kupunguza nguvu zake za kijeshi!. Why all those killing and destroying citizens areas wakati kila siku Ghadafi ana wa bonb wapinzani wake!?. Kama kuna mtu anajua hii stratejia na atujuze.
 
hawa makafiri wekundu shida yao sio kutetea haki za libyan shida yao ni mafuta 2! Waarabu wakuwa wajinga mpaka wanatoa sapot kwa nato haya sasa wanapiga mpaka makazi ya kiongozi tofauti sheria ya umoja wa mataifa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom