Gaddafi angesoma alama za nyakati kabla mambo hayajaharibika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gaddafi angesoma alama za nyakati kabla mambo hayajaharibika.

Discussion in 'International Forum' started by Anold, May 9, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Gaddafi ni kiongozi wa muda mrefu ambaye amefaya au kutoa mawazo yenye manufaa kwa Libya na bara zima la Africa. Mara kadhaa Gaddafi amekuwa akitaka Africa iungane na kuwa kitu kimoja, sitaki kujua agenda ambayo anayo kuhusu shinikizo lake la mara kwa mara la kutaka umoja huo ila ninachojua alikuwa na mawazo ya kizalendo. Hata hivyo inavyooelekea mambo si mazuri kwa kiongozi huyo, baadhi ya wananchi wake wamemchoka na nchi za magharibi zimedaka ajenda hiyo kuhakikisha kuwa adui wao waliokuwa wanamuwinda kila kona anaondoshwa. Natambua kuwa Gaddafi ni mtu mwenye msimamo mkali asiyetaka kuburuzwa, hata hivyo ili aibu na balaa kubwa lisije likampata shujaa huyu ni afadhali asome alama za nyakati ili yasije kumkuta yale ya Bagbo na kuwa kichekesho na aibu kwake na hata bara zima la afrika ambalo halionyeshi bidii zozote za kusuluhisha au kuingilia kati kwenye mgogoro wa Libiya na migogoro mingine ya afrika.Ni bahati mbaya sana kuwa viongozi wengi wa Africa hawana uwezo wa kusoma alama za nyakati, hii ni dosari ambayo itawakumba viongozi wengi ambao hawana muda wa kupoteza kusoma alama za nyakati, mimi sio mtabiri ila mwisho wao utakuwa kichekesho na balaa kubwa kwao.
   
Loading...