Gadafi anafaa kuiongoza Afrika kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gadafi anafaa kuiongoza Afrika kweli?

Discussion in 'International Forum' started by Exaud J. Makyao, Feb 3, 2009.

 1. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Rais Muamar Gadafi ni mkuu wa Umoja wa afrika.Hivi kweli anafaa kuiongoza Afrika wakati nchi yake inamshinda?Kwani kuwa mkuu wa Umoja wa Afrika kunahitaji sifa gani?Au hakuna kigezo?
  Mimi sijui.

  LEO Tar. 1/7/2009,
  Kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP Rais Mahamoud Ahmednejad wa Iran ambaye alialikwa na kiongozi wa Libya Kanali Muhamar Gadafi kuhutubia mkutano huo sasa hatohudhuria.


  Hakuna taarifa zilizotolewa juu ya hatua hiyo.Kadhalika Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlosconi ambaye pia alialikwa na Kanali Gadaff amefuta ziara hiyo..


  Kanali Gadaffi ambaye ndiye kiongozi wa umoja huo wa Afrika kwa sasa, anategemewa kusukuma zaidi ajenda yake ya kutaka kuundwa kwa serikali ya Afrika.Hata hivyo ajenda kuu ya mkutano huo wa siku tatu wa wakuu wa Afrika ni kuimarisha uwekezaji katika sekta ya kilimo barani Afrika.

  Je hii ni dalili ya kwamba hakubaliki?
   
  Last edited: Jul 1, 2009
 2. M

  Mkuu Senior Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Jan 1, 2007
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyo Kkiwete alifaa kuwa kiongozi?
  Au kwa sababu ni gaddafi
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kigezo nikuwa Kiongozi wa Nchi ya Africa, na huwa wanapeana zamu, Anglo phone, Francophone, na wale waarabu kwa maana hiyo hata Mugabe anafaa kabisa....kama unakumbuka hata Idd Amin aliisha wakuwa kiongozi. Halikuwa dili sana kwa muungwana as usual hakufanya maajabu.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Uenyekiti wa AU ni mzunguko, hii ni zamu yake. Kuna aina mbili za viongozi bora. Kuna wale wanasiasa wenye nguvu kubwa ya ushawishi na wazungumzaji wazuri mfano wa JK, Makamba, Mugabe, Mbeki etc lakini sometimes vitendo ni zero.
  Na kuna viongozi wakimya, wenye nguvu kubwa ya kufanya mambo. Huyu ndiye Gadafi. Ana nguvu ya fedha ya kufanya mambo na mwaka huu mtaona mambo. Hawa ndio kama akina Mhe.Rostam na Mhe.Mkono hawaulizi maswali bungeni na hawachangii mijadala yoyote bungeni lakini wana uwezo wa kufanya mambo.
  Wao hutinga Dodoma kwa ndege zao kama rais, makamo na waziri mkuu. Tofauti na viongozi wakuu wa nchi, ndege ni za serikali, wao ni za kwao. Kikwete akitaka maendeleo kwao
  Bagamoyo, lazima amobilize wananchi na serikali, Rostam na Mkono wao wanatoa mfukoni. Huyo ndie Gadafi.
  Wakati wa vita na Amin, alimpelekea majeshi na sisi akatuletea vifaa vya kivita vya mabilioni.
  Enzi za Mkapa ni Gadafi ndiye aliyeleta yale mabenzi mapya makubwa meusi ya Ikulu.
  Pamoja na pesa yote hiyo, kuna tetesi Gadafi pia ni mbaya sana kwa wanawake wapenda pesa, baada ya kuwa rafiki na Dr. Salmini, akatembea na mkewe Salma. Salmini kusikia, akamtwaga talaka rejea. Gadafi akaoa jumla, ikabidi jamaa atoe talaka tatu.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Mod ihamishe hii thread na kuiunganisha na nyenzake. Two identical with the same starter.
   
 6. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MKUU,
  Makosa mawili hayafanyi jambo liwe sahihi.
  Suala je huyu anayeendelea sasa anafaa?
   
 7. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  USHIROMBO,
  Kama hakuna kigezo, basi ni kama mchezo wa kuigiza.
   
 8. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  PASCO,
  Hilo la TALAKA tuliweke kando.
  Tutazame uwezo wa Gadaffi kuiongoza afrika.
   
 9. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  toka lini gaidi akawa mtu wa kuongoza watu wastaarabu? gaidi mla rushwa anayependa kumpa kikwete mashangingi? for what? uzuri wake ni kwasababu huu uongozi hauna effect yoyote africa, uwepo usiwepo hamna tofauti, hivyo wacha tu gaidi akalie kiti.
   
 10. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa una mawazo mapya?
   
 11. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa updates hizi zinakupa mawazo mapya?.
   
 12. c

  cradibility Member

  #12
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anafaa sana na ikiwezekana mungu ampe maisha marefu komandoo gadafi
   
 13. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bado nina mashaka na Gaddafi.

  Eti amezitaka ofisi za ubalozi za Israel Afrika kufungwa.
   
 14. M

  Mchili JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Asichopenda Gadafi ni kuburuzwa na wazungu lakini kwa upande wa uongozi naweza kusema ni mzalendo namba moja katika marais wa Afrika na anawapenda sana watu wake.
   
 15. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Libya haijamshinda Gadafi. Libya imepata maendeleo makubwa kwa jitihada ya Gadafi. utajua haya kwa kusoma historia ya Libya au hata kwenda Libya. Suala la kutaka ofisi la ubalozi wa Israel zifungwe katika nchi za kiafrika, huo ni mtazamo wake na haufuti ukweli wa maendeleo katika nchi yake.

  Suala la uwekezaji katika kilimo ndiyo dira ya Tanzania pia kupitia ''KILIMO KWANZA" na hata wakati wa Nyerere tulikuwa tunasema KILIMO NDIYO UTI WA MGONGO WA UCHUMI WETU na kama utakumbuka azimio la Iringa ''SIASA NI KILIMO. hivyo wazo la gadafi siyo jipya masikioni kwetu.
   
 16. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa nini MCHILI na Patrick hamuoni kuwa Gaddafi ana chembe za Udikteta?
   
 17. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Gadafi ni mtu mmoja asiyeeleweka. unajua kuna tatizo moja, waislam wenye msimamo mkali kama gadafi, huwa na akili pungufu sana, wanafikiri kama wenye ubongo wa samaki hakika. Kuna siku mwaka jana alishasema at BIBLIA NI MANENO YA UONGO TU NI STORI TO, na kwamba, DINI PEKEE NI UISLAM NA WAKRISTO WOTE WANATAKIWA WASILIM.

  Leo tena anakuja anasema,AFRIKA WAFUTE BALOZI ZA ISRAEL. hivi anafikiri kila mtu hapa ni mwislam? au anafikiri hapa kila mtu anaupenda uislam? anafikiri kila mtu anapenda ushirika na waarabu? au tunaishi tu hapa kwa kuvumiliana kwasababu tu ndani ya nchi kuna dini nyingi na tunaishi kwa kuheshimu dini za wengine ili tuishi kwa amani?

  anasahau kuwa, ukianza kuuliza swali mtu mmoja mmoja ukipitia makanisa yoote Tanzania, au east Africa yoote hata dunia, watakaosema wanaichukia Israel hawapo. hata ukiwauliza kuwa, je ni vyema Israel kulipiza kisasi kwa wapalestina, wote watasema ndiyo. ukiwauliza wakristo wote nchi ya israel ni ardhi ya nani watakwambia ni ardhi ya israel. hadi leo hii haiingii kichwani kwa mkristo yoyote kusikia kuwa Bethlehem mji aliozaliwa Yesu ni makao makuu ya palestina..hahaha. lakini tunanyamaza tu tunaishi kwa kuvumiliana. ila kila siku tunaiiombea israel izidi kupanua mipaka yake ifike hadi damascus ikiwezekana, kwasababu kulingana na Mungu alivyowapa ile ardhi, hadi Jordan yote ni yao, and even part of syria au syria yote kabisa.

  Sasa, kama kuna siku kikwete atataka kuwajaribisha wakristo wa tz, aseme hakuna uhusiano kati ya israel na tz, hapo ndo ataona kuwa kumbe vile vita vya israel havipiganwi na waisrael peke yao.

  sasa gadafi anapokuja na maneno yake kama hayo akirikiri labda sisi wengine ni ndugu zake, anakuwa kama mtoto mdogo.anajiona amefikia maendeleo makubwa sana kule libya ya kuweza kuwafundisha waafrika maisha.
   
 18. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Amakweli hoja zako ni nzito.
  Lazima zijibiwe.
  Aatakayejibu, awe makini pia.
   
 19. K

  Koba JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ....eh he hehe tafadhari sana,eti anatupenda? anampenda nani mshamba yule,kakaa kwenye uraisi miaka 40 kwani hakuna wengine,watu kama hawa lazima waondoke na mawazo yao ya kishenzi!
   
 20. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ukitaka kujua hali ya Libya... nenda ukaone au ingia kwenye miandao yao wenyewe.
  Hilo halikamiliki bila kumsikila mwana mapinduzi na mwanaharakati wa mapambano ya uhuru kwa waliowengi Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson mandela ambaye aliwahi kukaririwa akimsifu Gaddafi na maendeleo ya watu wa Libya. Mandela alisema kwamba Demokrasia kwa vigezo vya nchi za magharibi haina maana sana kwa mtazamo wa wananchi wa LIbya na wote waliofaidika na ufadhili wa Libya ukulinganisha na huduma za kijamii na kiuchumi wanazopata wananchi wa Libya. Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikionyesha wasiwasi au kutomwamini Kanali Gaddafi hasa juu ya kuufadhili ugaidi duniani na kutokuwa na demokrasia yenye vigezo vya kimagharibi.

  Lakini kwa sababu mcheza kwao hutuzwa, wananchi wa Libya wanamwamini sana Gaddafi ambaye amekuwa na ndoto ya kuifanya Afrika kuwa Bara Imara kiuchumi, kijamii na kimaendeleo ili kufuta dhana potofu za magharibi.

  Baada ya Gaddafi kutangaza suluhu na nch za magharibi ikiwemo Uingereza na Marekani amekuwa akifunga magoli ya kidiplomasia tungu hapo; Hii ni pamoja kuondolewa vikwazo vya kibiashara, usafiri na hivi karibuni kuachiwa huru kwa mfungwa ugaidi wa Lockerbie na kumfanya kuwa mfano wa mwana mpotevu aliyerudi Kundini. Dunia inapaswa kuendelea kutafakari matendo yake na Azma na Dhima yake juu ya utangamano na amani duniani.
  Katika medani ya siasa za Afrika.kufuru alizofanya alipoukwaa uenyekiti wa Afrika ni dhana ya uongozi anaouota kuongoza Afrika kama Rais wa Kwanza wa Afrika. Ni mawazo mazuri lakini tunapaswa kuyatafakari kwa makini tusije tukawa tunapalilia mkaa kwa limbukeni wa ndoto za mchana za "uendawazimu".
   
Loading...