Elections 2010 Gachuma akanusha madai ya Dk. Slaa

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Mkurugenzi wa kampuni ya vinywaji Coca Cola na mjumbe wa Nec mwita Gachuma amezungumza na waandishi wa habari na kukanusha madai kuwa alikaa kikao na J. Kikwete, Ridhiwan, Rostam Aziz na Lowasa. Amesema kuwa yeye hawezi kukaa katika hoteli ya La-Kairo ambayo haina hadhi kuliko hoteli yake ya Mwanza Hoteli na kwamba siku ya kikao alikuwa Tarime.
 
Mbona kwenye walaka jina lake limo sasa anawatuhumu CCM kwa kuweka jina au Slaa kupata copy ya waraka?
 
Mkurugenzi wa kampuni ya vinywaji Coca Cola na mjumbe wa Nec mwita Gachuma amezungumza na waandishi wa habari na kukanusha madai kuwa alikaa kikao na J. Kikwete, Ridhiwan, Rostam Aziz na Lowasa. Amesema kuwa yeye hawezi kukaa katika hoteli ya La-Kairo ambayo haina hadhi kuliko hoteli yake ya Mwanza Hoteli na kwamba siku ya kikao alikuwa Tarime.
People will never cease to amaze me. What an attitude!
 
Wote watakataa kwa sababu ni kitendo cha aibu. Lakini ingekuwa ni sifa wangerukaruka na kushangilia!
 
Mkurugenzi wa kampuni ya vinywaji Coca Cola na mjumbe wa Nec mwita Gachuma amezungumza na waandishi wa habari na kukanusha madai kuwa alikaa kikao na J. Kikwete, Ridhiwan, Rostam Aziz na Lowasa. Amesema kuwa yeye hawezi kukaa katika hoteli ya La-Kairo ambayo haina hadhi kuliko hoteli yake ya Mwanza Hoteli na kwamba siku ya kikao alikuwa Tarime.

Hey! What a SHAME AND IRRENSIPONSIBLE RESPONSE. Kwamba hawezi kukaa hoteli ya hadhi chini ya ile yake? Ndo kusema baba yake, wadogo zake, shangazi zake, na watu wangine hawezi kukaa kwako mpaka wawe na hoteli au nyumba yenye hadhi sawa au kubwa kuliko yake?

Ndo kusema ni mbaguzi kiasi hiki? Sihitaji hata kujua kama alikaa au hakukaa, ila nimeumia sana na jibu la kuwadharau watu wasiokuwa na makazi yenye hadhi kama aliyonayo yeye-ndo tafsiri kwa uelewa wangu mdogo!

Pole.
 
Kama hawakukaa La-Kairo basi si aseme walikaa wapi?...Uzuri kuna watu wetu pale hotelini ambao waliwaona live, kwahiyo kubisha kunawaharibia zaidi, na kuwafanya waonekane vituko!
 
sasa huyo gachuma hadhi yake tunavyojua ni kama LAKAIRO (lameck airo) coz wote ni class seven
:nono::nono::nono::nono::nono::nono:
 
Wote watakataa kwa sababu ni kitendo cha aibu. Lakini ingekuwa ni sifa wangerukaruka na kushangilia!
Nani anaweza kukubali kwamba alikaa nakupanga kuhujumu uchaguzi ni scandal. Hata Nixon wa USA alikanusha watergate scandal lakini mwishowe ilimtoa Ikulu. Hata EPA walikataa mpaka Spika Sitta alitishia kumpeleka Slaa polisi lakini wote tunajua matokeo. Wanaona aibu na kuogopa backlash ya Jumuiya ya Kimataifa.
 
Na hiyo sahihi ya Mkurugenzi wa JiJi la Mwanza waseme imegushiwa, Au waseme Mkurugenzi kawasingizia pia
 
Mkurugenzi wa kampuni ya vinywaji Coca Cola na mjumbe wa Nec mwita Gachuma amezungumza na waandishi wa habari na kukanusha madai kuwa alikaa kikao na J. Kikwete, Ridhiwan, Rostam Aziz na Lowasa. Amesema kuwa yeye hawezi kukaa katika hoteli ya La-Kairo ambayo haina hadhi kuliko hoteli yake ya Mwanza Hoteli na kwamba siku ya kikao alikuwa Tarime.
Utetezi gani na huyo naye kama alikaa kikao na jk,ridhi,RA na ER kuna dhambi gani? shida labda agenda zao zilikua nini?
 
Turudi kwenye hoja ya Dr. Slaa ambayo inataja waraka uliotaja watu hao kwamba walikuwepo kwenya kikao. Hoja ijibiwe hivi:
1.kweli kulikuwa na na kikao cha namna hiyo ua hakukuwa na kikao cha namna hiyo.
2. Kulikuwa na kikao cha namna hiyo na washiriki walikuwa hao waliotajwa au siyo hao au walikuwa baadhi ya waliotajwa.
3. waraka ulikuwa wa kweli au wa kughushiwa.

Hivyo, mtu kusema kuwa hawezi kukaa katika Hoteli hiyo kwa sababu siyo ya hadhi yake haijibu hoja zinazopaswa kujibu hoja za msingi. Hivi kwa mfano, mtu umetuhumiwa kuiba baiskeli ya mtu unaweza kujibu kuwa sina hadhi ya kuiba baiskeli badala ya kujibu tu kwa sentensi moja kuwa sikuiba au niliiba, ni kweli au si kweli?

Ninachokumbuka kuhusu waraka uliwataja walioshiriki kikao hicho ni kuwa Kabwe alikiri sahihi ni ya kwake. Kwa hiyo anayejua kuwa Gachuma alishiriki au la ni yule aliyeandika waraka siyo Dr. Slaa.
 
Mkurugenzi wa kampuni ya vinywaji Coca Cola na mjumbe wa Nec mwita Gachuma amezungumza na waandishi wa habari na kukanusha madai kuwa alikaa kikao na J. Kikwete, Ridhiwan, Rostam Aziz na Lowasa. Amesema kuwa yeye hawezi kukaa katika hoteli ya La-Kairo ambayo haina hadhi kuliko hoteli yake ya Mwanza Hoteli na kwamba siku ya kikao alikuwa Tarime.

Wewe Gachuma nenda Mahakamani basi kama umesingiziwa, siyo unaongelea chini ya Meza - mnafikiri Tanzania ni ile ya miaka 10 iliyopita? info zina flow zaidi ya vile mnavyojua ninyi. kazi kwenu - zigo hilo mmetwishwa na wenzako.

Wizi mwingine una nafuu lakini huu wa kura ni zaidi ya wizi yaani UHAINI- Kajisafisheni mahakamani wakubwa.
 
Its not amazing nilijua tu atakana, taarifa uloletwa na dr wa ukweli ilionesha jina lake, labda kama atasema jina lililotajwa si la kwake. Kuhusu hadhi ya Lacairo na Mz Hotel hii imekaa kibiashara zaidi!
 
Hiyo kansa ya hujuma itawatafuna tuu.Ila kweli ukila nyama ya mtu huachi kamwe pamoja na kashfa zote EL na RA hawajakoma tuu.Kweli TZ iko hatarini kama wananchi hatutaikomboa.
 
Ahaha. Huyu mzee Gachuma ameniacha hoi. Yani ametumia hii nafasi kutangaza biashara yake. Huyu mzee ana cheo cha udhamini wa CCM kama yule mzee wa upareni Peter Kisumo. Na ni kiongozi nadhani mkoa wa mara.

Jamani tukubali tukatae hata tufanye nini CCM hii imechafuka sana haiwezi kutakata. Huu mchezo wa hujuma upo siku nyingi. Mbowe 2005 aliibiwa zaidi ya kura laki 5 dar peke yake ila inaonekana watu hawakufuatilia sana na hata yeye mwenyewe hakulalamika. Sasa haya tunaona ni madhara aliyosema Nyerere ya kula nyama ya mtu. Kwamba last time waliiba ikafika 80% hivi haiwezekani kuzidisha hapo kidogo?? Wote tuna tabia ya kufanya vema zaidi kila tunapopata nafasi nyingine ya kufanya kile kile. Kosa la mkuu ni kuwahusisha wanae vilaza kwenye mambo mazito. Watu wanaperform ze komedi kwenye mambo ya msingi.
 
Labda angekanusha kuwepo na kikao kilichotoa hayo maazimio na yeye kushiriki..
Kukataa kwamba hakua Lakairo wakati huo hakufuti hoja kuwa waliaazimia hayo maovu..
Waache wajing'ateng'ate mwisho wa siku tutajua lililo kweli..
 
yeye huyu gachuma ndo alilipia garama zote za kile kikao

mbona kila kitu kinajulikana!!!!
 
waraka wenyewe huo hapo

wasikane hawa
 
Attachments

  • nyaraka ya siri.doc
    178 KB · Views: 122
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom