Gabo Zigamba afanya filamu ya kisa cha Mkulima Mwamwindi kumuua mkuu wa mkoa Iringa, Dkt. Kleruu

Gabo Zigamba afanya filamu ya kisa cha Mkulima Mwamwindi kumuua mkuu wa mkoa Iringa, Dkt. Kleruu

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
810
Reaction score
2,039

Mnamo Sikukuu ya Krismasi mwaka 1971, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Wilbert Kleruu, aliuawa na mkulima Said Mwamwindi huko Isimani.

Tukio hilo lilitokea wakati wa utekelezaji wa sera za serikali za kutaifisha mashamba makubwa, baada ya kuzuka mgogoro mkali kati yao.

Mwamwindi alijisalimisha polisi mara baada ya tukio na baadaye alihukumiwa kunyongwa mwaka 1972.

Kifo cha Kleruu kilibaki kuwa miongoni mwa matukio yaliyotikisa sana historia ya Tanzania baada ya uhuru.

Soma
 
Mbona kama imemuabisha sana mkuu wa mkoa

Au ndiyo ilivyotokea ?
Kwa tuliosoma kisa chake ipo sawa 95%, hapo alipomuweka kwenye gari akaanza kupiga misele mitaa ya Iringa, raia wakawa wanashangaa Mwamwindi imekuwaje anaendesha ndinga ya RC . Baadaye akapeleka gari kituo cha polisi na kuwaambia kachukue mbwa (sina hakika) wenu kwenye buti.
 
Safi sana ndo kazi za sanaa zinazotakiwa, ajitokeze mwingine aandae zinawahusu akina Mkwawa, Mirambo na machifu wengine namna walivyoongoza himaya zao na kupigana na wakoloni
 
Back
Top Bottom