G4s Waibiwa

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,207
0
Mchana wa saa 7 na dakika 14 nilikuwa natoka kitumbini kuvuka kuelekea lumumba kabla sijafika katika geti la mlango wa benki ya wananchi wa Tanzania , nikaona watu wanafukuzana kwa mbale .

Mzee mmoja wa makamo alikuwa anafukuzwa na mwenzake anamuita mwizi , alipofika karibu na nilipo mimi , vijana wengine wakatoka kusikojulikana wakamkata ngwala yule mzee .

Huyu mzee alikuwa ameficha hela ndani ya shati lake kwahiyo zile hela zote zikaruka watu wakagombaniana kila mmoja , ndio walinzi wengine wa G4S wakafika eneo hilo na kumkamata yule mzee .

Nilipochunguza zaidi nilikuta kumbe wale G4S walikuwa wamebeba pesa hizo ndani ya gari lao , katika foleni ya bibi titi ndio mwenzao akachukuwa hizo pesa na kuamua kukimbia nazo .

Hata alivyokuwa anakimbia inaonyesha wale walinzi wote sio wakakamavu ndio maana alimkimbiza kutoka bibi titi mpaka mnazi mmoja bila kumshika mpaka alipokatwa ngwala .

Walinzi hawa walishindwa hata kupambana na vijana waliomkata ngwala mpaka kumpora hela au wakati wanamkimbiza walishindwa kutumia njia yoyote ile kumsimamisha inawezekana hawakuwa na silaha ndani ya gari lile .

Kama wangevamiwa na majambazi basi pia wangeporwa kwa sababu hawakuwa na silaha yoyote ya kujitetea ndani ya gari lao , huu ni udhaifu mkubwa sana .

Pia inashangaza kwanini pesa hizo hazikuwekwa katika mifuko au sefu maalumu mpaka mlinzi anajichukulia tu na kushuka kama ilivyotokea mchana wa leo .

Hali hii inatia mashaka sana kuhusu uwezo wa wafanyakazi wengi wa haya makampuni binafsi , kuanzia Knight Support , Ultimate sina uhakika nao na sijawahi kusikia choko choko zao , Gema Security na nyingine nyingi .

Kuna umuhimu wa wizara husika sasa kuendesha uchunguzi kwa kampuni hizi kujua uwezo wa wafanyakazi wao katika kupambana na matukio kama haya wengi sio wapambanaji na hata hawana muda wa mazoezi kwa kweli .
 

Dotori

JF-Expert Member
Nov 3, 2007
544
0
Intersting story. Vetting system inahitajika katika kuajiri security guards. Kwa mfumo hata kibaka anaweza kuwa Security Guard
 

Mtaalam

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
1,338
1,250
nshawahi sikia wahindi nowdays wanatumia ambulance kusafirisha mijihelaa yao......kingora juu mwapisha njia mkijua mgonjwa...kumbe mijihelaaaa
 

Kuntakinte

JF-Expert Member
May 26, 2007
702
0
nshawahi sikia wahindi nowdays wanatumia ambulance kusafirisha mijihelaa yao......kingora juu mwapisha njia mkijua mgonjwa...kumbe mijihelaaaa

Tehe hee tehe! Kweli wahindi Kiboko. Ukisema hivyo unanikumbusha kuna jamaa yangu mmoja Bongo aliniambia habari za ambulance sasa hivi watu bongo wanatumia sana kuwahi MAOFISINI asubuhi kukwepa Foleni za Magari hasa Barabara ya Morogoro mitaa ya Jangwani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom