FYI: Baada ya uturuki ni Tanzania; na sisi tuko juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

FYI: Baada ya uturuki ni Tanzania; na sisi tuko juu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ochu, Aug 28, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa utozaji mkubwa wa kodi za mawasiliano,ambapo inatoza gharama ya asilimia 30 ukilinganisha na Uturuki ambayo ni ya kwanza kwa asilimia 45.Viwango hivyo ni vikubwa,na kwa upande wa hata nchini gharama hizo ni kubwa na zinaonekana kuwafaidisha zaidi kampuni za simu.
  Hiyo yote inatokana na nchi kutokuwa na mkongo wake wa mawasiliano ambayo ungesaidia kupunguza gharama hizo na kuwabana wenye kampuni za simu ambao hutumia minara yao binafsi.Hivi karibuni Waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Profesa Peter Msolla aliwasilisha bungeni makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2008/09 ambayo ilisisitiza pia ujenzi wa mkongo huo.
  Mkongo wa mawasiliano wa Taifa ambao uko mbioni kujengwa,utasaidia kupunguza gharama za mawasiliano nchini zinazopanda mara kwa mara.Profesa Msolla anasema mara ukamilikapo ujenzi huo,itakuwa rahisi kwa Mamlaka ya mawasiliano kuwa na sababu za kuwabana kampuni binafsi za simu kupunguza gharama za mawasiliano kuliko ilivyo sasa.
   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ....niliwahi kusikia story kama hizi,naomba wataalam wa mawasiliano watueleweshe hapa namna ya investment kam hiyo(mkonge wa simu) unavyofanya mawasiliano yawe chini maana technically nchi zilizoendelea bei za simu ni chini sana nafikiri ni kwa ajiri ya investment kam hizo...pls tuelewesheni maana kuna watu hawafanyi kazi yao pale kazi yao kununua magari tuu na kutufisadi....bei ya simu bongo ni kufa mtu na inatisha.
   
Loading...