TANZIA FW de Klerk, rais wa zamani wa Afrika Kusini na mzungu wa mwisho kuiongoza nchi hiyo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,137
2,000
Tunamwitaji De Clerk mwingine pale CCM...

Ingawaje zama za ubeberu zilikuwa ukingoni lakini De Clerk angeamua kama wenzake, nae angeweza kuendelea kuendeleza utawala dhalimu wa Kikaburu pale South Africa!!

Hata kama Nelson Mandela hatimae angetoka gerezani, bado ingewezekana kuendelea kuwa korokoroni kipindi chote cha De Clerk!!!

Ingewezekana hadi kesho yale yanayoendelea Palestine na Israel, kuwa yanaendelea hadi kesho pale South Africa!!

Hata hivyo, Fredrick De Clerk akasema NO... zama za tawala za kibeberu na kidhalimu zimeshapitwa na wakati, so "let's end this"!

"Of course", I believe that's how De Clerk started to tell his team "...we still have the backup of our fellow Imperialists from UK, US, Israel, and elsewhere! We still have enough number of our black puppets everywhere in the continent, including in this our holly land! We can still keep slaughtering these black monkeys whatever we want, but for how long!"

So, tunahitaji De Clerk mwingine pale CCM!! Fredrick de Clerk ambae hataanza kuonesha dalili za kuwa rebellious mapema!

Tunahitaji mwana-CCM atakayeficha kucha zake kama ambavyo alifanya De Clerk, kwa sababu lau kama Fredrick de Clerk angeonesha mapema nia ya kurudisha utawala wa walio wengi, KATU asingepewa hata nafasi ya "Mkuu wa Wilaya"!

Tunahitaji mwana-CCM anayejionesha yupo tayari kufa kwa ajili ya CCM, na mara anapopata nafasi ya kuongoza nchi basi atumie fursa hiyo kuiporomosha CCM na kuirudisha nchi kwa wananchi ambao wameshachoshwa na CCM... dubwasha lililojishindilia kila mahali, na lililo tayari kunyonya damu ya kila mtu kuhakikisha linababaki madarakani hata kama litabaki kutawala mbuzi na kondoo!!

Hivi ndivyo Fredrick de Clerk alifanya kule South Africa kiasi kwamba hata wakati anachaguliwa rasmi kuwa rais, no one expected him to be different kwa sababu hata wakati akihudumu kama waziri, alionesha wazi ku-support ubaguzi wa rangi!!

Watu wakaja kushituka, pale Blacks walipotaka kuandamana na polisi kutaka kuwazuia, Fredrick de Clerk akawaambia "HAPANA... waacheni waandamane, mlango wa Afrika Kusini mpya umefunguka!!

Huo ni ushahidi tosha kwamba hata wakati de Clerk anaonesha ku-support ubaguzi wa rangi, huenda alifanya hivyo ili kuendelea kuaminika na chama chake cha National Party lakini kumbe moyoni hakuwa nao pamoja!

Rest In Peace Frederik Willem de Klerk...

Kwangu, huna baya! Na yale ambayo ulifanya zama za Ubaguzi wa Rangi, sina shaka Mungu wako atakuwa amekusamehe kwa sababu you'd to be one of them to complete your mission of the new South Africa!!
Kweli kabisa alikua mtu kiungwana Sana tofauti na Yule Peter Botha.
Yule alikua mkatili kama Jiwe.
 

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
2,040
2,000
...
IMG_20211111_131823.jpg
 

Mwambwaro

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
2,001
2,000
Kuna watu ambao hawajui history wanamwona Kama mtu mbaya huyu mtu kwa sababu tu n kaburu, Huyu jamaa ndiye aliyeleta uhuru wa democracy na ndiye aliyeleta aman south n mwanamabadiliko na mwanamageuzi
 

Ngigana

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
1,876
2,000
Pumzika kwa amani mwana mageuzi wa RSA. Uamuzi wako ulileta mageuzi makubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi. Nitakukumbuka kwa hilo na wapenda amani watakuenzi kwa ujasiri wako wa kusimamia unachokiamini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom