FUWAVITA: Changamoto na upungufu wa walimu wenye uelewa wa lugha ya alama

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Chanzo: Report of Deaf Youth’s Living Situation in Tanzania.

Shule maalumu za viziwi Pamoja na uchache wake, zinakabiliwa na upungufu wa waalimu wenye utaalamu wa kufundisha wanafunzi viziwi kuanzia ngazi ya awali, msingi, sekondari, chou kikuu na vyuo vya mafunzo ya ufundi.

Walimu wanaopangiwa kufundisha katika shule maalumu za viziwi huwa na nadharia kwamba lugha ya alama ni ngumu, hivyo hata katika kuifanyia kazi huwa na changamoto.

Mwalimu aliyehojiwa Moshi Technical Secondary School amefundisha wanafunzi viziwi kwa muda mrefu aliamua kujifunza lugha ya alama ilia pate ajira ya serikali.

Serikali inapopangia waalimu vituo vya kufundisha, huwa inawapa muda mfupi kujifunza lugha ya alama na haizingatii kupima uwezo wa walimu katika lugha ya alama kwa kiwango cha kuweza kufundisha wanafunzi viziwi.

Walimu ambao huchaguliwa kufundisha katika shule maalumu za viziwi hupata mafunzo ya alama za lugha kupitia asasi za kiraia kama CHAVITA, UMIVITA, CHAVIZA, FUWAVITA na nyinginezo.


Imeandaliwa na:
FUWAVITA
 
Back
Top Bottom