Guru Master
JF-Expert Member
- Jan 14, 2017
- 224
- 591
Tarehe 10 February mwaka 2017 ilikuwa ni siku ya kutimiza miaka 100 tangu kifo cha Geronimo ambaye alikuwa ni shujaa kutoka Jamii ya Apache( hawa ni mashujaa wa wahindi wekundu au wakazi asilia wa Taifa la marekani maarufu kama Red Indians) Ndugu mmoja katika jamii hii alifungua mashtaka akiwashtaki Skull and bones jamii ya Siri ambayo ilianzia chuo kikuu cha Yale huko marekani kuwa iruhusika na kuiba mabaki ya Geronimo. Miaka kadhaa imekuwa ikipigiwa kelele jamii hii ya Fuvu na Mifupa kuwa imeshikilia mabaki ya Geronimo ikiyatumia kwa shughuli zake za kiimani.
Haryln Geronimo mwenye miaka 61 anasema “ naamini kabisa toka moyoni mwangu kuwa roho ya Geronimo haikuachiliwa” akiwaambia waandishi wa habari waliokusanyika wakifuatilia tukio hili lililohusisha jamii hii ya Skull and Bones. huyu ni kitukuu cha Geronimo .
Inasemekana kuwa Wakongwe Kama Prescott S. Bush ambaye ni baba wa Aliyekuwa Rais George W. Bush na Babu wa George W. Bush . huyu na wenzie wengine wanachama wa Skull and Bones walichimba mabaki ya Geronimo toka kaburini mwaka 1918 WAKAIBA FUVU LA HUYU SHUJAA, NA MIFUPA MIWILI na mavazi ya kivita kutoka katika Kaburi lake huko Fort Sill ( Ujue kuwa hizi imani za kuchimba makaburi na kuiba vitu flan zipo hata kwa wazungu si afrika tu ) na jamii hii ikachukua mabaki haya na kuyaweka Makao yao Makuu ambayo yalikuwa yameanzishwa toka mwaka 1832.
Conspiracy Mbalimbali Kuhusiana na Skull and Bones
Kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusiana na kundi au jamii hii. Inasemekana hawa ndio waliohusika na utengenezaji wa bomu la nyuklia mpaka kuuawa kwa J.F. Kennedy. Ni kundi ambalo wengi nchi za huku kwetu hawajalifaham lakini kwa Huko kwa wenzetu ni Kundi kubwa na la kutisha sana. Hili ni Kundi lenye viongozi wakubwa sana duniani likihuishwa na miaka ile lilipokuwepo kundi la mafia.. kuwa hili ni kundi la mafia la kimataifa.
Skull and Bones wamehusika na Ku endesha Utajiri wa Carnegie, Rockefeller na Familia ya Ford na pia kujihusisha na CIA, American Psychological association , Baraza la Mahusiano ya Kimataifa na pia Baadhi ya Makampuni makubwa ya Sheria Kimataifa.
Mwaka 2004 wakat wa uchaguzi wa Urais waliokuwa wagombea wa Republic na Democratic walikuwa ni wanachama wa jamii hii. Ingawa haya hayakusemwa sana maana ilikuwa ni siri. Johnn Kerry alipoulizwa jambo hili alijibu kifupi tu kuwa “ni siri na siwezi zungumzia jambo hilo” na Bush W. naye pia alipata kuzungumzia hili kwa hali ya kutotaka liendelee kuwa gumzo hivyo kwa Kiswahili kingine ni kuwa alilipotezea. Uhusika wa watu katika Jamii hii ni wa siri sana.
William Russell alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Yale. Huyu ndiye aliyeanzisha jamii hii ya kishetani yenye nguvu kubwa bada ya kuwa aliwah kukaa Ujeruman akiwa mwanchama wa kundi moja la siri sana duniani likiwepo kundi pia la ILLUMINATI. Rusell alirudi USA akiwa amedhamiria kuanzisha jamii ya siri ya aina yake na akamwambia Alfonso Taft ambaye mtoto wake alikuja kuwa Rais William H. Taft kuwa mmoja ya wanachama wa Kundi hili la Udugu wa Kifo “The Brotherhood of Death” ambalo baadaye ndo likaja kufahamiaka kuwa ni “The order of Skulla and Bones” wanachama walikuwa wakimuabudu Eulogia huyu ni mungu ambaye inasemekana alikuwa na nguvu za kufanya mtu awe na nguvu ya kuongea mbele za watu na kukubalika, kutukuzwa na kuwa mwenye Umiliki wa Dunia.
Fuvu na Mifupa ilianzishwa chuo kikuu cha yale ambacho ni cha Tatu kwa Uzaman Huko Marekani kwa maana ya kuwa ni chuo cha zamani sana katika namba ya vyuo vya zaman usa kinashika namba tatu. Jamii hii imekuwa n ibada zake na mambo mablimbali ambayo yamekuwa ni alama zao I pamoja na nyoka na kutoka sadaka zao kwa mungu wao maybe actually ni shetani ila kwa jina linguine. Wanachama wa kundi hili hupatikana kwa njia ya siri sana na wala huwezi ona matangazo au mtu akijitangaza kuwa yeye ni wmanachama wa kundi hili. Baadaye hupelekwa sehemu ya ibada yao kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya kuapishwa kuwa atakuwa mwanachama mwaminifu mpaka kufa.
Wengi wamekuwa wakisikia habari za freemason na illuminati, kundi hili ni kubwa sana na lenye nguvu kubwa sana kiuchumi na kiutawala duniani. Umakini wao umewafanya waendelee kuwa kimya pasipo kujulikana sana kama yalivyo makundi mengine. Na bado limekuwa likihusika sana katika makundi mengine kwa nia ya kujitanua na kujipa nguvu.
Hii dunia tunaishi ila kuna watu wanaiendesha na kupanga matukio mbalimbali. Kuna watu wanaamua nani awe rais na kwa sababu zao wao. Ni mambo machache sana ambayo yanatokea pasipo watu flan kuwa wamepanga yawe.