Fuvu la albino lililokutwa baa: RPC Kinondoni hajui kama ni la binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fuvu la albino lililokutwa baa: RPC Kinondoni hajui kama ni la binadamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Jul 19, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,127
  Trophy Points: 280
  Mara nyingine nashangazwa sana na kauli za Polisi, kama hii iliyotolewa na RPC wa Kinondoni kwamba lile fuvu lililopatikana katika baa ya mfanyabiashara pale Kawe, haijulikani kama ni la binadamu. Taarifa zinasema ni fuvu (au kichwa) la albino, RPC anasema hajui kama ni binadamu. Hivi kauli za polisi kama hizi ni kutoa mwanya fulani kwa ajili ya kusafisha watuhumiwa au nini hasa?

  Je, RPC anachotaka ni kwamba tusishangae polisi watakapotangaza kwamba lile fuvu si la binadamu bali la sokwe na hivyo mtuhumiwa atashitakiwa kwa kosa la kuwa na nyara za serikali na sio mauaji ya binadamu?

  Kweli Tanzania kila kitu kinawezekana.
   
Loading...