‘Future’ ya siasa za Tanzania ni mitandao ya kijamii, sio kampeni kwenye mikutano ya hadhara

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Ndugu zangu, dunia inabadilika kwa kasi sana na hivyo kumfanya mwanadamu abadilike kwa hiari au kwa lazima.

Moja ya changamoto kubwa ambayo imekuwa ikitukabili, ni kumsikiliza mtu kwa muda wa dakika 2, na kudhani ushamuelewa vizuri huyo mtu ni nani hasa, na kumpa au kutompa nafasi ya uongozi. Hivyo ndivyo ambavyo imekuwa ikitokea huko nyuma.

Kwa mfano, mwaka 2017, wakati wanatafutwa wawakilishi kuwakilisha kwenye EALA; wagombea walipewa dakika 3, kujieleza. Sasa ni kwa vipi unaweza kumjua mtu vizuri kwa dakika 3, kiasi cha kujiridhisha kumpa au kutompa jukumu kubwa? Kwenye uchaguzi 2015 kurudi nyuma; unakuta kwenye kila mkutano mgombea ana dakika 2 za kuongea, Unawezaje kumjua mtu kwa dakika 2 na kumwamini au kutokumwamini?

Kwa kulielewa hili, sasa hivi Serikali na makampuni makubwa ya nchi mbalimbali mbali yanapotaka kuchagua,kuteua au kuajiri mtu; hufuatilia kwa siri au muhusika hutakiwa kuwasilisha Account zake za kwenye mitandao ya kijamii kwa jopo la usaili na huko ndipo usaili hasaa unakofanyika.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba, ili ujue hasa rangi ya mtu; unahitaji muda wa kutosha kumsoma, na ni vizuri kumsoma wakati hajui kama anasomwa (hajajianda). Kwa hiyo kwa kurejea vitu ambavyo mtu anaandika mtandaoni kwa miaka kadhaa, inatosha kabisa kumjua mtu husika ni nani. Aidha, kama zama hizi mtu 'hasa kijana' hatumii mitandao ya kijamii na anataka kuwa kiongozi wa kisiasa, hiyo tu inatosha kujua huyo mtu ni wa namna gani.

Kumbuka, yamtokayo mtu ndio yaliyojaa kichwani mwake, lakini kama anajua anafanyiwa usaili kwa dakika 2, ata ‘Fake’ kwa hizo dakika 2, kisha atarudi kwenye maisha yake ya kawaida na hiyo inafanya wasipatikane viongozi 'genuine'. Tumshukuru Mungu teknolojia imetupa solution ya hili.

Katika dunia ya sasa, mafanikio yamejificha nyuma ya vitu vyenye gharama nafuu lakini matokeo makubwa, ufanisi mkubwa kwa usumbufu kidogo, na mafanikio ndani ya muda mfupi kwa nguvu kidogo.

Mitandao ya kijamii inawezesha kufikia watu wengi kwa muda mfupi, kwa gharama nafuu na bila usumbufu. Kwa mantiki hiyo, mitandao ya kijamii ndio ‘future’ ya siasa za Tanzania kuliko kampeni kwenye mikutano ya hadhara.

Kuna hoja kwamba watanzania wanaotumia mitandao ya kijamii ni wachache. Hoja hii si sahihi kwa sababu takwimu za TCRA zinaonesha kuwa angalau watanzania 23 Milion wanatumia internet na 22M kati ya hao wanatumia internet kupia simu zao na idadi inaongezeka kila siku. Hiyo ni kama nusu ya idadi ya Watanzania wote.

Kuna hoja ya kwamba yanayofanyika mitandaoni kwa kiwango kikubwa ni ujinga. Ijapokuwa hoja hii ni ya kweli na ina uzito mkubwa; huo ujinga unaofanyika kwenye mitandao ya kijamii ni ‘reflection’ ya ujinga ulioko mtaani. Kwa lugha nyingine tulivyo ndivyo tulivyo na hivyo ndivyo tulivyo pamoja na mitandao, au bila mitandao. Kwa hiyo hii haiondoi ukweli kuwa mitandao ya kijamii ndio ‘future’ya siasa za Tanzania zaidi ya kampeni za majukwani.
 
Na ndio maana itabidi tuangalie namna ya kutengeneza software itakayofichua alama zenu za vidole ili mpatiwe haki yenu ya mikesi isiyo na dhamana
 
Na ndio maana itabidi tuangalie namna ya kutengeneza software itakayofichua alama zenu za vidole ili mpatiwe haki yenu ya mikesi isiyo na dhamana
 
Sisi hatu update hata website zetu
Ni uelewa tu mkuu, zamani inasemekana mababu zetu walitumia vipande vya almasi, dhahabu, tomaline za kijani na nyekundu, rubby, sapphire na tanzanite kuchezea draft na bao hadi alipokuja mzungu akawastua kuwa zilikuwa ni mali za thamani kubwa. kwa hiyo ni suala la muda tu, mtagundua kipi ni kipi.
 
Katika zama hizi, haitarajiwi kiongozi wa kisiasa mwenye angalau umri wa chini ya miaka 50, asiwe anatumia mitandao ya kijamii kuwasilisha mawazo yake, ili watu wawe wanamuelewa ni mtu wa namna gani wakati wote. Kama wapo wasiofanya hivyo, hilo ni tatizo la kwanza kubwa kwenye zama hizi.na pengine wanafanya hivyo ili siku ikibidi ku 'fake' iwe rahisi
 
Katika zama hizi, haitarajiwi kiongozi wa kisiasa mwenye angalau umri wa chini ya miaka 50, asiwe anatumia mitandao ya kijamii kuwasilisha mawazo yake, ili watu wawe wanamuelewa ni mtu wa namna gani wakati wote. Kama wapo wasiofanya hivyo, hilo ni tatizo la kwanza kubwa kwenye zama hizi.na pengine wanafanya hivyo ili siku ikibidi ku 'fake' iwe rahisi
Kumbuka wapiga kura wa kweli na waaminifu ni wale WANYONGE wenzangu,hawajui hata mitandao ikoje?sisi tunaojidai tunajua mitandao hatuna hata vitambulisho vya mpiga kura.
 
Kumbuka wapiga kura wa kweli na waaminifu ni wale WANYONGE wenzangu,hawajui hata mitandao ikoje?sisi tunaojidai tunajua mitandao hatuna hata vitambulisho vya mpiga kura.
Kwa hiyo unataka kusema 'future'ya Tanzania I mikononi mwa wanyonge na kwa kadiri watu wanavyotoka kwenye kundi la wanyonge ndivyo wanavyokuwa tatizo, kwa hiyo tunatakiwa kufanya juu chini kuhakikisha tunakuwa na wanyonge wengi Zaidi ili kupunguza tatizo?
 
mdudu ninaowazungumzia hapa ni watu ambao tayari ni viongozi wa kisiaasa, wana mpango wa kuwa viongozi katika level za vyama au kitaifa, au wanadhani ni wadau muhimu kwenye masuala ya kisiasa.

Kwa mfano juzi juzi kulikuwa na uchaguzi wa viongozi wa jumuia ya vijana wa chama kimojawapo. Washiriki wakawa wanasifiwa walivyo mahiri, n.k

Sasa badala ya kuwasifu au kuwaponda kutokea hewani, tunarejea kuona mawazo yao kwenye mitandao ya kijamii kwa miaka mitatu nyuma wanasema nini kuhusu nini. Hapo unaweza kuelewa kwa uhakika kila mmoja ni nani hasa.

Na kama ikitokea hawapo kwenye mitandao ya kijamii, katika zama hizi kwa maoni yangu wanakuwa disqualified automatically.
 
Kadhalika ukitoa hiyo 23 milioni, maana yake inabaki kama 27milioni, ukitoa wenye umri ya miaka chini ya 18, kama 20 milioni, inabaki kama 7 milioni tu.
 
Back
Top Bottom