Futuhi ya Star TV Vs Ze Comedy

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Kwa sasa kuna Commedy huko Star Tv inajulikana kama Futuhi, kimsingi Futuhi ni neno la kiswahili linalomaanisha Commedy, yaani tamthiliya ya ucheshi, jamaa kipindi chao kinarushwa saa 3 Usiku Alhamisi na kurudiwa Saa 5.30 asubuhi.

Wanawachambua wanasiasa na maamuzi yao, na noana wanaingiza hata clip halisi - mfano hata ya Muungwana halafu wanaitwanga kejeli za Kikomedi. Inaonekana wakiendelea hivi wanaweza kuwa spika nyingine ya kupigania maendeleo ya kweli, wacha zile bla bla ya kupakana mafua kwa mgongo wa chupa. Sijui wanajiamini nini?

Lakini pia kuna wasi wasi kuwa, Ze commedy baada ya kuingia TBC 1 hawataweza kuwa jeuri ya kuwakejeli mabwana wakubwa, na huu kama ndiyo mtindo hatutashangaa wakitumiwa kuwasafisha mafisadi, maana, maana mbwa huchezesha mkia kutoka mluzi wa mwenye mbwa.

Lakini ndiyo maendeleo haya.
 
Back
Top Bottom