FUTIKA FUTIKA: Kilevi kinachofuta akili ndani ya muda mchache baada ya kunywa

kacnia

JF-Expert Member
Sep 16, 2014
3,893
15,247
Maandalizi

*Pukuchua mbegu zake
*Changanya na maji lita 1
*Acha baada ya masaa 6+
*Kunywa

Matokeo:
Kati ya matukio haya manne, moja nimelishuhudia juzi kwa kijana mmoja ninayefahamiana naye na leo aliponiletea mmea huu ilibidi niupige picha nilete humu kwa ajili ya kujuzwa zaidi juu ya mmea huu.

1. Bwana mmoja alipokunywa alikua eneo lake la kazi (anaosha magari) mara baada ya dakika kadhaa alionekana akiwa amehama kimawazo ndipo rafiki yake alipomshika na kumtoa kwenye ile hali, cha kustaajabisha ni pale bwana huyo aliyekunywa futika futika aliposhtuka na kudai kutomtambua yeyote kati ya wale aliokua nao pale ile hali wanafanya nae kazi kila siku, akaenda kununua sabuni ya unga ya elf moja, akachukua ndoo yenye maji akalifuata jiwe moja lipo karibu na wanapooshea magari akaanza kuliosha kwa muda mrefu.

2. Mwingine alipokunywa futika futika alienda mpaka kwenye nyumba ambayo haijui na kuvua nguo kisha akamuagiza aliye mkuta amuite mke wake "oya niletee mke wangu kwanza" aliskika mnywaji wa futika futika. Alipokea kipigo kutoka kwa mwenye nyumba akaokolewa na majirani waliokua wanamfahamu.

3. Huyu mnywaji wa futika futika mwingine yeye alipokunywa alienda ofisi ya mkuu wa mkoa kudai pikipiki yake akidai kuwa alinunua na kuipeleka huko, naye alipigwa sana na walinzi akatupwa nje akiwa hoi

4) Huyu wa nne siku nimesikia habari hizi za futika futila nilikuwa naye nikajiapiza kutafuta mmea unaotengenza kilevi hiki na kutafuta taarifa zake kumbe yeye alijiapiza kujaribu kabisa. nitanukuu maelezo yake baada ya kutumia "nilikunywa funda kubwa badala ya kamfuniko kamoja, ilipofika saa tisa usiku hali ikabadilika sikujua nilikua naongea nini ila baada ya muda nilishtuka nimezungukwa na watu ambao sikuwatambua na koo lilikuwa limekabwa na ninaongea kwa shida sana kisha nikaanza kutapika"

Mmoja wa marafiki zake walioshuhudia tukio hilo anasema "alivua nguo akawa anaongea lakini anaskika kwa mbali kuwa anataka muda huo afuate abiria kwa bajaji ili hali hana bajaji muda huo wala hajawasiliana na mtu yeyote"
Huyu bwana anasema alitapika sana usiku huo katika hali ya kupambania maisha.

Futika futika inaisha nguvu baada ya masaa zaidi ya 10 mwilini, watumiaji wanadai ukinywa kiwango cha mfuniko wa kopo ni kilevi kizuri, nawasilisha kwenu kwa aliye na ujuzi zaidi wa mmea huu unaoleta kilevi ambacho kimepewa jina futika futika kutokana na matokeo yake anijuze zaidi

20211130_121608.jpg
 
Back
Top Bottom