Fursa Zipo Nyingi , Vijana Tuchangamkeni

Hall of famer

Member
Jan 12, 2021
45
142
Tukiachana na wito wa wanasiasa wengi wanaohimiza vijana kujiajili bila kutoa a way forward ya namna yakujiajili au bila ku sight fursa zilizopo nchini, binafsi nimejaribu kufanya analysis kwenye maeneo kadhaa ambayo kama nchi yanatupa advantage zaidi kulinganisha na majirani zetu. Lakini pia vijana au watanzania tulio wengi, hua tunapenda kusikia ama kufatilia matamko ya wanasiasa ambayo sometimes yamekua hayana impact kwa maisha yetu binafsi.

Tanzania, ukiangalia geographical location yake tumezungukwa na nchi nyingi sana. Jamani ,yan tuna borders nyingi sana ambazo nchi za wenzetu hawajapata bajati iyo .... Unawezatoka Tz ukaingia nchi hizi straight bila kupita ndani ya nchi nyingine (Yaani tuna direct access na nchi hizi).... Kenya, Uganda, Burundi,DRC, Zambia, Rwanda, Malawi, Zambia, Mozambique) . Tafsiri yake ni kwamba, tuna advantage kibiashara na nchi zote hizo. Pia tuna advantage kidiplomasia almost na nchi zote, tuna historia nzuri nazo, baadhi ya nchi ni land locked zinatutegemea kwa importation (Through bandari zetu). Lakini pia,kwa record zilizopo ni kwamba wabongo tunapendwa na nchi jiran zilizo nyingi, yaan watu wa uko hawana shida na wabongo. Nenda DRC Congo ,ulinganishe wacongo wanavyo watreat wabongo na wanavyo watreat Wazambia au Wazimbabwe.

Udhaifu wa wabongo tulio wengi, hasa vijana wakibongo wamejaa uoga, mbongo sio mtu wakwenda front kupambania deal hasa linalohusisha kuvuka border ( Sijui shida ni mfumo wa elim yetu ulivyo tutengeneza??!!) Hua tunawaogopa wakenya ,lakin wanachotuzid wao ni ile spirit yakuwania fursa (they are go getters). Wabongo wengi hawatakagi mishe zakumiiza kichwa, anataka akute kila kitu kimenyooka. Nilishangaa sana ,nilienda Malawi kum introduce mshkaji wangu ana kampin ya Clearing & Forward ,jamaa wa Malawi wakashangaa wakawa wanauliza ni kwanin port iko kwenu TZ ila wanaokuja kuchukua contract za Clearing apa Malawi wengi ni wakenya??!!

My Advice
Tuamkeni jamani, nchi yetu ipo kwenye economic blocs km EAC, SADC yaani mkikaa tu hum ndan bila kutoka hata apo jiran mtashangaa wa Zimbabwe, Kenyas, UGs et all ndo wanafaidi. Najua wengi tutasema issue ni capital,but trust me wengine hatukuanza na capital hata kdg but we made some deals hadi kufika hapa. Tutafute na tupeane connections, tuache roho zakukunja. Mwisho wa siku serikal sio baby sitter wetu, we need to go forward ,be confident enough tusilegee legee watu wanasaka fursa jaman. Zunguka kwny borders ,sio mtu unapajua mkoani kwenu ulikotoka na Dar tuu basii unaona km umemaliza. Halaf km hamjui, wabongo tuko talented sn yani tuko fasta hasa kwenye deals na hua tuna sifa nzuri -Kwa wale wanaothubutu - (Pongez kwa founders wa nchi waliweka mazingira mazuri sn diplomatically) . Km una mchango wako ,karibu n let's share vijana tutoke. Sio kijana kununua tu ka IST na kujenga nyumba ya rum 2 unaona ushatoboa ,let's think Big jaman.

Ahsanteni!
 
vijana unaowasema ni wengi sana, hata hapa wapo.....ila ni waoga kwenye ku-take risk... kutoboa hakuna shortcut....na hata mtaji ukikata....kama unaamini hapo ulipo ndio sahihi...songa mbele.....wapo mijini...masimu makubwa wanadunda na " vi don touch" 😂 , akikuzoea tuu lazima akupige mzinga......mimi wengi nawaambia mimi siku hizi sikopesho...njooo nikupe kazi maliza nakulipa nenda....akion akazi utasikia ntakuja kesho.....hawaji...na kijiweni yupo anagongea fegi...
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom