Habari zenu wakuu,
Nategemea mnaendelea vizuri na pirikapirika za kujitafutia kipato.
Nashkuru kuifahamu jf, kwa kweli ni sehemu muafaka ya kuzidisha maarifa binafsi ya fani fulani na ya maisha kwa ujumla, kiasi ya kwamba imesheheni taarifa,mawazo huru,miongozo na kubwa zaidi inatoa nafasi ya fikra endelevu.
Kwahivyo nami nimeonelea niwasilishe dukuduku langu ili nipate kutoka kwenu ushauri na maelekezo yatayoweza kunisaidia kupata rizki na kuinuka kimaisha.
Kwa kua ugumu wa maisha unazidi kila kukicha huku fursa za ajira zikiwa chache kulinganisha na idadi ya wahitimu kila mwaka, nimeamua kujiingiza ktk ujasiriamali, hivyo napanga napangua, nafanya upembuzi wa biashara husika/namna ya kujiajiri.
Maelezo binafsi:-
ELIMU: Mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza ktk fani ya usimamizi wa fedha ( finance ).
UZOEFU: niliwahi kujishughulisha na masuala ya utalii zanzibar; kubook malazi, kuandaa tours,kuwaunganishia watalii usafiri n.k ila siku hizi kwa mtu binafsi(na hata kwa kampuni ndogo) imekua ngumu sana.
SEHEMU KUSUDIWA: Zanzibar, mjini unguja.
MTAJI WA FEDHA: milioni 1.
MTAJI WA WAZO: bado haupo sawa - najaribu kujiepusha na kucopy na kupesti bila mpango maalumu.
Kutokana na maelezo hayo, naomba ushauri wenu:
1- nifanye nini?
2- Biashara gani inaweza kunitoa na ujanja+skills zipi zinahitajika kwayo?
3-Fursa gani zilizopo Unguja na vipi naweza kuzichangamkia?
Mawazo na michango yenu naithamini.
Hatibu Golo
Jang'ombe - ZnZ