Ndugu watanzania wenzangu: Kwa muda wote ninapokwenda Kampala huwa nachunguza sana kuhusu nafasi ya Mbongo katika mji huo wa kibiashara. Jambo kuu nililoiona kuhusu fursa ya kazi kwa mtanzania ni ile ya upishi yaweza kuwa pia kuanzisha kiji-restaurant kidogo hii inalipa sana. Tafadhali soma sababu zifuatazo;
Jamani tuchangamkie fursa hii.
Nawasilisha
- Sijawahi kula chakula kizuri katika mgahawa wowote wa makabwela wala hotel kubwa kwa kifupi waganda hawajui kupika
- Kwa ninavyofahamu watanzania kuhusu mapishi wana ujuzi wa hali ya juu. Hasa kwa watu wa Tanga, DSM Morogoro na Pwani hata kwetu Shinyanga si wabaya sana
- Kazi hii haihitaji mtaji mkubwa wala utaalam wa hali ya juu waweza pata elimu ndogo tu kwa mama lishe yeyote na kwenda huko kuanzisha kazi
- Maisha ya huko ni ya amani sana hizo habari unazosikia wala zisikutishe, Kampala inapokea kila mtu
- Waganda wanapenda sana kula shasa chakula kitamu kama vile pilau, biliani na mambo yote ya kipwani pwani.
- Kuhusu uhamiaji tafuta paspoti na pia omba kibali cha kuishi na kufanya kazi.
Jamani tuchangamkie fursa hii.
Nawasilisha