Fursa za Kazi kibao kwa Watanzania Kampala

matunge

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
442
426
Ndugu watanzania wenzangu: Kwa muda wote ninapokwenda Kampala huwa nachunguza sana kuhusu nafasi ya Mbongo katika mji huo wa kibiashara. Jambo kuu nililoiona kuhusu fursa ya kazi kwa mtanzania ni ile ya upishi yaweza kuwa pia kuanzisha kiji-restaurant kidogo hii inalipa sana. Tafadhali soma sababu zifuatazo;

  1. Sijawahi kula chakula kizuri katika mgahawa wowote wa makabwela wala hotel kubwa kwa kifupi waganda hawajui kupika
  2. Kwa ninavyofahamu watanzania kuhusu mapishi wana ujuzi wa hali ya juu. Hasa kwa watu wa Tanga, DSM Morogoro na Pwani hata kwetu Shinyanga si wabaya sana
  3. Kazi hii haihitaji mtaji mkubwa wala utaalam wa hali ya juu waweza pata elimu ndogo tu kwa mama lishe yeyote na kwenda huko kuanzisha kazi
  4. Maisha ya huko ni ya amani sana hizo habari unazosikia wala zisikutishe, Kampala inapokea kila mtu
  5. Waganda wanapenda sana kula shasa chakula kitamu kama vile pilau, biliani na mambo yote ya kipwani pwani.
  6. Kuhusu uhamiaji tafuta paspoti na pia omba kibali cha kuishi na kufanya kazi.

Jamani tuchangamkie fursa hii.
Nawasilisha
 
Ni rahisi sana kuipata ukiwa huko kwani waweza ishi hadi miezi 3 ukiwa na pasipoti kipindi hiki waweza jifunza mambo mengi sana...
 
Tatizo waganda hawaongei kiswahili, Ukianzisha biashara hapo lazma hili likupe tabu maana hata hao wahudumu wenyewe watashindwa kuwasiliana na wapishi ambao wengi wao watakuwa wa TZ.
 
Chakula shida siyo siri. Tatizo wenzetu hawana tamaduni ya kutumia spices. Really missing chips kuku ya mitaa ya Dar, supu, mishikaki.............. .
 
Tatizo waganda hawaongei kiswahili, Ukianzisha biashara hapo lazma hili likupe tabu maana hata hao wahudumu wenyewe watashindwa kuwasiliana na wapishi ambao wengi wao watakuwa wa TZ.
Si wote wapo wanaoongea Kiswahili pia. Pia si mbaya nawe ukajifunza kiganda. Mbona ukihitaji waweza kujifunza ndani ya wiki 3 tu..
 
Ndugu watanzania wenzangu: Kwa muda wote ninapokwenda Kampala huwa nachunguza sana kuhusu nafasi ya Mbongo katika mji huo wa kibiashara. Jambo kuu nililoiona kuhusu fursa ya kazi kwa mtanzania ni ile ya upishi yaweza kuwa pia kuanzisha kiji-restaurant kidogo hii inalipa sana. Tafadhali soma sababu zifuatazo;

  1. Sijawahi kula chakula kizuri katika mgahawa wowote wa makabwela wala hotel kubwa kwa kifupi waganda hawajui kupika
  2. Kwa ninavyofahamu watanzania kuhusu mapishi wana ujuzi wa hali ya juu. Hasa kwa watu wa Tanga, DSM Morogoro na Pwani hata kwetu Shinyanga si wabaya sana
  3. Kazi hii haihitaji mtaji mkubwa wala utaalam wa hali ya juu waweza pata elimu ndogo tu kwa mama lishe yeyote na kwenda huko kuanzisha kazi
  4. Maisha ya huko ni ya amani sana hizo habari unazosikia wala zisikutishe, Kampala inapokea kila mtu
  5. Waganda wanapenda sana kula shasa chakula kitamu kama vile pilau, biliani na mambo yote ya kipwani pwani.
  6. Kuhusu uhamiaji tafuta paspoti na pia omba kibali cha kuishi na kufanya kazi.

Jamani tuchangamkie fursa hii.
Nawasilisha

Sahii kabisa anachoshesema jamaa, KUBWA zaidi ni kwamba waganda hawajui kupika, pili waganda Hawajibani

kabisa katika kula..mganda hata awe masikini vipi lazima atakula vizuri tu bora atembee uchi lakini sio kaitka

menu atakula Katogo, samaki mkubwaa, chipsi, yaaani vyoote ivyo mlo mmoja...ivyo basi wale ambao

wanaanzisha restaurant hupata sana hasa wabongo sababu ya kujua kupika..Mwisho ule mji una wageni sana

kila taifa liko pale, wasudan,waethiopia, waelitrea, wasomali, wakenya ndoi usiseme, warwanda n.k

Hawana habari ya kumindiana..nenda aanzisha biashara chapchap.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom