Fursa za Biashara na kilimo cha nyanya, Iringa Ilula

Mar 21, 2021
10
11
Za jioni wandugu,

Nimetembelea mkoa wa Iringa, niweza kujionea maajabu na fursa nilizozikuta. “Kweli tembea ujione”.

Tenga la nyanya, ambalo linatoa mbaka ndoo kubwa tatu, linauzwa 15,000 .

Kukodi kwa eka ni 30,000.
Kutumia ng’ombe kwa eka moja ni 30,000.
Kutumia treka ni 50,000 kwa eka mafuta na dereva ni wa wenye treka.

Muda mwingine unaweza elewana na mwenye shamba na akakupa bure ulime coz yeye mwenyewe anahitaji shamba lake liwe safi. Kama alitumii lakini.

Mbolea ambayo mara nyingi wanaweka kila baada ya siku 21 moja ama mara 14 ukipenda bei ni 48,000 mbaka 58,000.

Kuhusu kumwagilia, tunasubili mvua. Ama kama upo kalibu na maji, yaani mto ama kisima chako mwenye raha tu.

Unaweza enda kuuza nyanya zako pale soko la nyanya ama kutokea shambani kwako.

Changamoto kubwa ni:

Nyanya ni nyingi, viwandwa vya kutengenezea nyanya vipo viwili, kimoja kipo hapo Ilola na kingine ni Iringa mjini.

Cha apo Ilola ni kidogo, kina uwezo wa kuchukua maximum tenga 200 mbaka 250.

Pia umwagiliaji. Sema huku wamebalikiwa na mvua na udongo mzuri. Kwaiyo wanalima kwa msimu. Ila kama kutakua na tecknologia nzuri ya umwagiliaji, hawa watu wanauwezo wa kulima mwaka mzima, yani misimu yote.

Bila kusahau madawa nayo ni muhimu kwa nyanya zako.

Fursa nilizozifikiria.

1.Kiwanda cha kuzindika ama kuhifadhi nyanya kwa mda mrefu ili zisiharibike. Mfano kipindi nyanya zipo nyingi zinaweza zikachukuliwa zikachemshwa kwa usafi wa hali ya juu, na kuekwa kwenye packaging ambazo zitahifadhi radha yake halizi kwa mda mrefu.

2. Sijaona kiwanda cha tomato paste.

3. Viwanda vya chill pamoja na tomato za chips viongezeke itapendeza saidi. Maana uku nyanya kuna msimu wakulima wanaacha tani za nyanya zinaharibika mashambani.

Maona yangu kutokana na uharisia niliouona shambani:

Heka mbili zilizo limwa vizuri na kufatiliwa vizuri zaweza kukupa zaidi ya matenga 800.

Tafakari na chukua hatua.

#TheGardenerTraveller#
 
Yaani wewe lazima umezaliwa huko,

Nikufungue macho kiasi. Neno kiwanda mkuu inabid kujipanga...shida yetu watz tunalima in a small scale...kiwanda kinahitaji kulishwa kwa tons za kutosha ili kilete faida sasa unakutana na mkulima analima kwa msimu..then anaishia eka 10..utatoa ulimi nje...utawalipa nn watenda kazi?

Hicho kipindi unachosema wanaachaga tons mashambani ni.msimu tu..wangekuwa wanaacha nyanya shambani toka jan to jan baasi wachina wangeshatia timu mapeema.
 
Hayo maajabu uliyoyaona ingia field na hizo eka 2 ulizosema july tuletee mrejesho pia..all the best
 
Ili uweze kupata faida kwenye kilimo cha nyanya tumia kilimo cha umwagiliaji,hii ina maana unalima msimu tofauti ambao hauna wakulima wengi na supply ya nyanya inakuwa ni ndogo sana while demand ni kubwa.

NB;Karibu nikuhudumie kufunga mifumo ya umwagiliaji wa matone uweze kupata faida maradufu katika kilimo cha nyanya.
 
Mkuu unauhakika na inachosema au hicho kiwanda cha nyanya kinanunia nyanya mbovu mbovu tu tena kwa bei ya unyonyaji
 
Nakupongeza sana mkuu naheshimu mawazo yako, me huwa napenda mtu akielezea atoe maelezo kwa mpangilio kama wako, kuwe na njia ya kuchagu afuate au aache
 
1.Viwanda vipo darsh industries na dabaga bila kusahau collection centre zipo kibao njiani humo

Unajua bei ya kuuza kiwanda sh ngapi? 100-150tsh kwa kilo hivyo tenga/box la ndoo 3 ni tshs.5000-6000

2.ilula wanatoa nyanya nyingi ila bado sana.

Wanalima kienyeji sana ma ekari na maekari ya mbegu za kienyeji,elimu ndogo,ubora mdg.Kwa kilimo chao faida ipo km umelima eneo kubwa sana hlf misimu ambayo bei inakuwa chini sana ukabahatisha ukakuta bei juu.

Maji wengi wao wanategemea ya mvua.

Kifupi ilula bado ina kilimo cha bahati nasibu.

Kuwa makini unapotaka kulima nyanya kwa bahati nasibu.Nyanya sio zao la mazoea kabisaaaa.

Sababu nyanya ekari moja ukilima kisasa ni tenga 800-1200 za ndoo 3.Wakati ilula mtu kupata mavuno hayo inabidi awe hadi na ekari 5-10.

Mtu analima ekari 50 anavuna mara mbili anasumbua sokoni anatoweka..
 
Umeongea ukweli mtupu, nipo ilula hapa,kwakweli tunalima kwa bahati nasibu sana,
Ilula nzima hii ukisema ukusanye ekari 10 za hybrid Nina uhakika hutopata
Ila MTU mmoja analima mpaka ekari 30 za Rio grande tena mbegu za kukamua, in shot ilula kwetu tunategemea zaidi bei iwe juu ili tupate na sio quantity na quality ya mavuno
 
Back
Top Bottom