Fursa ya mafunzo kukuza ujuzi kwa njia ya uanagenzi(apprentice), Kwa hatua hii vijana tutanufaika sana tuwahi fursa

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
230
402
C&P
OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU

*TAARIFA KWA UMMA*

*FURSA YA MAFUNZO KUKUZA UJUZI KWA NJIA YA UANAGENZI*

1. Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu inatekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi kwa njia mbali mbali ikiwemo uanagenzi, mafunzo ya vitendo mahali pa kazi na utambuzi wa ujuzi uliyopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo. Katika kufanikisha utekelezaji wa Programu hii, Ofisi ya Waziri Mkuu imeingia mkataba na Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania iliyopo Oysterbay Dar es salaam wa kutoa mafunzo katika fani mbalimbali. Lengo ni kuwezesha vijana kuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na kuongeza wigo mpana wa kujiajiri au kuajiriwa au kuendelea na mafunzo ngazi ya juu. Fani zitakazofundishwa ni Kubuni Mitindo ya Mavazi na Ushonaji, Ufundi Bomba, Useremala, Uchomeleaji Vyuma, Uchongaji wa Vipuri vya Mitambo, Uashi, Uwekaji waTerrazo na Vigae kwenye majengo, Ufundi Magari na Mitambo, Kilimo na Ufugaji, Kutengeza Komputa, Kuchapa Vitabu na Nyaraka, pamoja na Kufunga Umeme ukiwemo wa mwanga wa jua (Solar) wa majumbani na viwandani. Mafunzo ya kukuza ujuzi yanafanyika Mikoa yote ya Tanzania Bara na yataanza kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itaanza Mwezi Julai inayojumuisha mikoa 12 na Awamu ya pili itaanza Mwezi Agosti, 2019 itakayojumuisha mikoa 14.

2. Mikoa na Vituo vitakavyotoa Mafunzo
Vituo vilivyokubalika na Serikali kutoa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Taasisi ya Don
Bosco Net Tanzania pamoja na fani zitakazotolewa ni:

*ENEO CHUO FANI*

1 *MUSOMA - MARA ST. ANTHONY VTC*

Ufundi umeme
Kubuni mitindo ya mavazi na
Ushonaji
Uashi
Mapishi ya vyakula

2 *GEITA (Location: Moringe Sokoine & Sophia Town) GEITA VOCATIONAL TRAINING CENTER*
Ufundi magari
Ufundi umeme
Ufundi umeme wa magari
Kubuni mitindo ya mavazi na
ushonaji
Utengenezaji wa kompyuta
Uashi
Ufundi bomba
Useremala
Kuweka terrazzo na vigae

3 *DAR ES SALAAM-*DON BOSCO OYSTERBAY VTC*
Ufundi wa magari
Useremala
Uchomeleaji vyuma
Uchongaji vipuri
Terrazo na Vigae
Kutengeneza Kompyuta
Ufundi umeme
Ufundi umeme wa jua (solar)
Kubuni mitindo ya mavazi na
ushonaji

*MATUMAINI YOUTH TRAINING CENTRE*
Mapishi ya vyakula
Utengenezaji wa kompyuta
Kubuni Mitindo ya Mavazi na
Ushonaji

*DON BOSCO YOUTH CENTRE UPANGA*
Kutengeneza Kompyuta
Kubuni mitindo ya Mavazi na
Ushonaji

4 *DODOMA-DON BOSCO DODOMA TECHNICAL INSTITUTE*
Ufundi magari
Useremala
Ufundi Bomba
Uashi
Terrazo na Vigae
Mapishi ya vyakula
Kutengeneza kompyuta
Kuhudumia vyakula na vinywaji
Uchomeleaji vyuma
Uchongaji vipuri
Ufundi umeme
Ufundi umeme wa jua (solar)
Kubuni Mitindo ya mavazi na
Ushonaji

5 *IRINGA-DON BOSCO YOUTH TRAINING CENTRE IRINGA*
Ufundi magari
Useremala
Ufundi Bomba
Uashi
Utengenezaji Kompyuta
Uchomeleaji Vyuma
Ufundi Umeme
Ufundi umeme wa Jua
Kubuni Mitindo ya mavazi na
ushonaji

*DON BOSCO MAFINGA*

Utengenezaji wa Kompyuta
Kubuni Mitindo ya Mavazi na
Ushonaji

6 *SHINYANGA-OLA SISTERS VTC-BUGISU*
Kutengeneza Kompyuta
Ufundi Umeme
Uchakataji wa vyakula ( food
processing)
Kubuni mitindo ya mavazi na
ushonaji

*ST. FRANCIS DE SALES TECHNICAL INSTITUTE- MWAKATA- ISAKA*
Kubuni Mitindo ya Mavazi na
Ushonaji

7 *ARUSHA KIITEC-MOSHONO*
Ufundi Umeme wa Jua (solar)
Kutengeneza Kompyuta
Ufundi umeme

8 *MOSHI - KILIMANJARO DON BOSCO MOSHI*
Kutenegeneza Kompyuta
Mafunzo ya ufugaji
Kilimo cha matunda, maua
(horticulture crops)

9 *BUKOBA - KAGERA KASHOZI HOME CRAFT VTC*
Kubuni mitindo ya mavazi na
Ushonaji
Mapishi ya vyakula

10 *SINGIDA RC MISSION VTC MANYONI*
Kubuni mitindo ya mavazi na
ushonaji
Mapishi ya vyakula

11 *LINDI LINDI RVTSC - VETA*
Uchomeleaji Vyuma
Ufundi umeme
useremala
Uashi
Ufundi magari

12 *RUVUMA PERAMIO VOCATIONAL TRAINING CENTRE*

Kubuni Mitindo ya Mavazi na
Ushonaji
Ufundi magari
Ufundi bomba
Ufundi umeme
Kuchapa vitabu, Makala na
nyaraka
Uashi
Ufugaji
Useremala
Utengenezaji wa Komyuta

13 *MOROGORO -HOLY CROSS SOCIAL TRAINING CENTRE*
Kubuni mitindo ya mavazi na ushonaji
Utenegenezaji wa kompyuta
Mapishi ya Vyakula

3. Sifa za Kujiunga na Mafunzo
Kwa wote wanaopenda kujiunga na mafunzo wanapaswa kuwa na sifa zilizoainishwa hapa chini :
(a) Elimu ya Msingi au zaidi kwa fani za Nguo, Mitindo na Ushonaji, Ufundi bomba,
Ujenzi, Useremala, Uchomeleaji na Uungaji vyuma;
(b) Elimu ya kidato cha nne kwa fani ya Utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi
magari, umeme wa majumbani na viwandani, TEHAMA, Umeme wa magari,
Umeme wa jua (Solar) na kuchapa vitabu;
(c) Awe Mtanzania;
(d) Awe na umri kati ya miaka 18 – 35; na
(e) Awe mwenye Afya njema

4. Fomu zitatolewa bila malipo katika vyuo husika kuanzia tarehe tarehe 17 hadi 23 Julai,
2019. Mwombaji anatakiwa kurudisha fomu kuanzia tarehe 24-26 Julai ikiambatana na:

(a) Barua ya maombi yenye anuani kamili ikiwa na namba za simu pamoja na barua pepe (kama anayo);
(b) Nakala ya Cheti cha Elimu uliyohitimu;
(c) Nakala ya Cheti cha kuzaliwa au Kitambulisho cha uraia au kadi ya mpiga kura;
(d) Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa anaoishi mwombaji (lazima); na
(e) Picha nne za paspoti zenye rangi ya bluu kwa nyuma.


5. Vijana watakao kidhi vigezo watafadhiliwa na Serikali kwa asilimia 100 kwa kulipiwa ada ya mafunzo yatakayofanyika katika vyuo vilivyotajwa hapo juu kwa muda wa miezi sita. *Kijana atakayechaguliwa atagharamiwa kiasi cha Tsh. 100,000/- kwa mwezi kama nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani*. Majina ya vijana wote waliochaguliwa kushiriki mafunzo yatatolewa magazetini na tovuti za vyuo husika kuanzia tarehe 1 Agosti mpaka tarehe 5 Agosti. Mafunzo ni ya kutwa na yataanza rasmi tarehe 19 Agosti, 2019. Hivyo, inashauriwa kwamba kijana kuomba mafunzo haya katika kituo kilicho karibu au ambapo atapata pa kuishi. Mwombaji atatakiwa kurejesha fomu ya maombi yeye mwenye katika chuo husika kabla ya tarehe 26 Julai, 2019. Tangazo la mafunzo katika mikoa mingine ya awamu ya pili litatolewa kuanzia tarehe 22 Julai, 2019.



Imetolewa na

Katibu Mkuu

17.07.2019
IMG-20190629-WA0006.jpeg
 
Ni kweli wapo out of time but nahisi tatizo people ilikuwa nyomi saana ndo maana wamechelewa Ku relies.
 
Poa ndugu zanguni tuendelee kupeana updates humu ndani in case kuna atakayepata mrejesho kwa kinachoendelea
 
Back
Top Bottom