Fursa ya kuuza bidhaa zetu China bila kodi isitupite kabisa

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Kupitia kwa balozi wa Tanzania China kuna taarifa muhimu za Biashara kati ya Tanzania na China.

Sehemu ya ujumbe huo imesomeka hivi namnukuu.

“Serikali ya China kuijumuisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 10 zitakazonufaika na uamuzi wake wa kutotoza ushuru kwa 98% ya bidhaa zitakazouzwa katika soko la china ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuuza zaidi bidhaa mbalimbali katika soko la china.”

Sehemu hii ya ujumbe huu umeniamsha ari zaidi ya kujua nini kilichopo kati ya Tanzania na China kwanini tumepata fursa hii muhimu?

Tukiangalia kwa mujibu wa matakwa ya mikataba ya kimataifa ya Biashara ya WTO - China inatakiwa kutoa misamaha ya kodi ya bidhaa zinazoingia China kutoka katika nchi zilizo na uchumi wa chini (low income country).

Ukiangalia kwenye orodha utaona nchi tisa (9) kwenye kundi la Low income countries.

Sisi Tanzania pekee ndiyo ipo kwenye middle income- maana yake China imetupa upendeleo-- kwasababu wanaruhusiwa kufanya hivyo.

Nimeenda mbali zaidi kuangalia juu ya matokeo ya ziara ya Mheshimiwa Rais wetu na hii ndiyo faida ya kujenga diplomasia.

Nchi zilizopewa ruhusa ya kuuzwa china bila vikwazo vya kodi ni pamoja na:

1. Benin
2. Afghanistan
3. Burkinafaso
4. Guinea Bissau
5. Lesotho
6. Malawi
7. São Tomé
8. Tanzania
9. Uganda
10. Zambia

Ni Tanzania pekee yenye uchumi wa kati iliyopewa hii fursa muhimu.

Ni fursa ambayo ukiitazama ni neema tupu kwa Wafanyabiashara.
 
Naona Rais Samia kamzunguka mzambia kiaina maana sasa Soya yetu pia itanunuliwa kwa bei nzuri na china, parachichi pia tuchangamkie fursa ndio hizo tusilale jamani,
 
Hapa nimekaa nafikiria kitu gani cha kupeleka china manake nyumbani kwangu kila kitu made in PRC. Hakuna hata kimoja made in Tanzania
 
Hawa watu wana tuona kama ngo'mbe na kutuchezea akili.

They know kitu pekee tunaweza uza kwao ni raw material...... so what mwisho wa siku bado tutazidi kuwafaidisha tu.
 
Back
Top Bottom