Fursa ya kupiga hela tumeletewa mlangoni na Makampuni ya Simu & TCRA

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,462
21,945
Wapendwa ninaleta kwenu mbinu mpya ya kupiga hela bila jasho. Kwa kosa walilolifanya makampuni ya simu kuzima internet bila taarifa huku wakiendelea kutuuzia vifurushi vya internet ambavyo havifanyi kazi bali vimetupotezea hela zetu pasipo faida.

Nawiwa kuwashawishi wote makapuku ambao tunalia kila siku kuwa hamna hela hebu njooni hapa tuajili mwanasheria nguli tumlipe hela yake tuwadai fidia hawa wenye makampuni ya simu kwa kutusababishia hasara kubwa.

Wapendwa hela haiji pasipo kutumia mtaji, hebu mkuje wote wenye hasira na haya makampuni tuchange milioni 20 za advocate na sisi tudai kulipwa fidia ya billion 3 na hayo makampuni ya simu yaliyotusababishia hasara.

Hela hiyo ya fidia ipo nje nje wapendwa njooni sasa tuanze mchakato nimeshampata mtu mmoja ambaye ni mke wangu amekubaliana na wazo langu ila akapendekeza wakili asiwe wa kutoka Tanzania akaenda mbali zaidi kwa kumpendekeza Robert Amsterdam.

Hayo malipo ya million 20 nimekisia tu ila Wadau tukisha kamilika na kumpata wakili tutajua na bei yake mkuje sasa tupige hela

NB
Bahati haiji mara mbili
 
Hayo makampuni yapo kimya mpaka sasa yanakazana kututumia sms za kubet tu, kuhusu kututaarifu kuwa hamna internet hapo hawatupi taarifa na wala hawajasitisha uuzaji wa bando
Sasa je watakwepaje lawama za wateja? 😔
Ninadhani ratizo la kutatua hapa ni kwanini Internet zimezimwa na wala si kuwalaumu wenye makampuni ya simu.
 
Back
Top Bottom