mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 473
- 1,448
Nimekuwa mwalimu wa Serikali tangia mwaka 2015, niliyajua haya kabla ya kuajiriwa na baada ya kuajiriwa nimeyathibitisha, ualimu ni moja ya kazi ambazo zinatoa nafasi kidogo sana kwa wajiriwa kufanikiwa kiuchumi kiasi kwamba mtumishi yoyote ukiijitambulisha ni mwalimu watu hukuunganisha na umaskini na ukweli ni huo.
Mafanikio ya walimu ni kujenga nyumba ya kuishi, akipata gari na kufanikiwa kumiliki kipande kidogo cha ardhi walimu wengi huridhika na kujiona wamefanikiwa, the same kwa watumishi wengi wa local government huwa na mtazamo huu.
Kwa nini hii hali ipo hivyo sababu ni
1. Mbali na mshahara hakuna njia nyingine ya kuingiza pesa iliyowazi labda uwe na connection pale NECTA at least kila mwaka utakuwa unapata vijipesa kidogo utakavyopewa baada ya kusahisha mitihani (hili lipo na kazi ya kusahisha ni reserved duty kwa baadhi ya walimu tu,pale necta pana namna).
Pamoja na hayo yote sisi tulioamua kutafuta pesa na kupingana na umaskini kwa nguvu zetu zote bado tunaona kazi ya ualimu wa serikali bado ina fursa, fursa zenyewe ni hizi
1. Muda, kazi ya ualimu sio complicated kabisa kiasi kwamba mwalimu unapata muda wa kutosha kufanya kazi zako za nje ya ajira, hapa muhimu upate shule ambayo mkuu wako sio mshamba na anajitambua, ukipata mkuu mshamba anakushikilia muda wote na anataka uwepo kituoni bila hata kuwa na kazi hii fursa hupotea.
Mfano mwalimu wa Kiswahili anafundisha mikondo miwili inamanisha una dk 40*6 =240dkk za kuwa darasani na ongeza dkk nyingine 240 za kufanya kazi nje ya darasa , ina maana una masaa nane kwa wiki ya kufanya kazi.
2. Mikopo, mwalimu usipokopa hakuna unachoweza kipata kwenye maisha zaidi ya nyumba fulani, gari fulani, na shamba fulani hivi, muhimu mwalimu akikopa ajielekeze kwenye shughuli za kiuchumi.
Mimi sijafanikiwa kwenye maisha ila naamini hizo ndizo fursa za ualimu mjue, kujipendekeza kwa wakuu na viongozi ili upate kusimamia mitihani, mara ufundishe jumamosi wanafunzi wakuchangie Tsh 200, kutoboa kwako hapo ni mbingu na ardhi.