Fursa pekee iliyobaki Tanzania ambayo haina changamoto ni kuwa mganga wa kienyeji

kamituga

JF-Expert Member
May 31, 2019
1,195
1,919
Wandugu nimetafakari sana kutokana na hali ya sasa ya Tanzania hususani kwenye vipengele vya kujikwamua kimaisha kama KUAJIRIWA, KUFANYA BIASHARA, UVUVI AU KILIMO.

Kila kukicha nimekuwa natafakari wapi pa kutokea na katika kuumiza kichwa kwa kuangalia impact pande zote mbili za faida na hasara nikagundua fursa iliyobaki tena pekee isiyo na zengwe ambayo watu wanaleta mpunga wenyewe huku wewe umejikalia tu kwenye kigoda tena Wasomi na wasiokua na Elimu tajiri na maskini ni kuwa MGANGA WA KIENYEJI maana kila mtu hii awamu anahisi amelogwa.
 
hahaaa..mkuu umenikimbusha jamaa yangu wakati anaanza kutafta maisha alijifanya mganga,,ye mzaramo,,sasa alienda kujifanya mganga dodoma,,kapiga kazi,,watu wanajiona wanapona,,dawa za uongo nakweli,,anaongea kizaramo harakaharaka watu wakajua kweli huyu mganga,sasa siku moja dada mwenye majini akaenda,,weee alipigwa mabanzi afu yule dada ndo yupo upande wa mlangoni,,uko nje watu wanajua mganga ndo anatoa majini,kumbe mwenzao anakula kibano,,afu akawa anabadilika macho ya kutisha ..wee ilibidi apige ukunga ndo watu kuja kumshka yule dada,,jamaa alivochomoka moja kwa moja hadi stendi akarud dar kusoma veta asa ivi fundi mzuri tu
😁😁😁....sasa siyo kazi rahisi kama unavodhani😁😁
 
....sasa siyo kazi rahisi kama unavodhani
Aina vyeti iyo kazi na miti shamba kibao nikiwachanja nawapaka pili pili ikiwasha namwambia dawa imeingia kwenye damu.
 
Mkuu asikwambie mtu ile kazi ni ya hatar sana.
Yaani ukishaanza tu kutibia watu Kuna wazee vigagula lazima usiku wakufuate kukujaribu nguvu yako.
Maana wanahisi unataka kuwavurugia mission zao za usiku,Sasa hapo ndio shughuli inapoanza kuwa nzito.
 
Hapo ndio shughuli inapoanzia!!!!
 
Hahaha hahahqhqhw
hahaaa..mkuu umenikimbusha jamaa yangu wakati anaanza kutafta maisha alijifanya mganga,,ye mzaramo,,sasa alienda kujifanya mganga dodoma,,kapiga kazi,,watu wanajiona wanapona,,dawa za uongo nakweli,,anaongea kizaramo harakaharaka watu wakajua kweli huyu mganga,sasa siku moja dada mwenye majini akaenda,,weee alipigwa mabanzi afu yule dada ndo yupo upande wa mlangoni,,uko nje watu wanajua mganga ndo anatoa majini,kumbe mwenzao anakula kibano,,afu akawa anabadilika macho ya kutisha ..wee ilibidi apige ukunga ndo watu kuja kumshka yule dada,,jamaa alivochomoka moja kwa moja hadi stendi akarud dar kusoma veta asa ivi fundi mzuri tu
....sasa siyo kazi rahisi kama unavodhani
 
Kwakweli ata mimi nmefikiria awamu hii waganga wanapata hela sana
Maana kila mtu anahisi karogwa
 
Wandugu nimetafakari sana kutokana na hali ya sasa ya Tanzania hususani kwenye vipengele vya kujikwamua kimaisha kama KUAJIRIWA, KUFANYA BIASHARA, UVUVI AU KILIMO.

Kila kukicha nimekuwa natafakari wapi pa kutokea na katika kuumiza kichwa kwa kuangalia impact pande zote mbili za faida na hasara nikagundua fursa iliyobaki tena pekee isiyo na zengwe ambayo watu wanaleta mpunga wenyewe huku wewe umejikalia tu kwenye kigoda tena Wasomi na wasiokua na Elimu tajiri na maskini ni kuwa MGANGA WA KIENYEJI maana kila mtu hii awamu anahisi amelogwa.
HAHAHA WAGANGA WA KIENYEJI NAO UPANDE WAO WANA CHANGAMOTO NYINGI SANA TU.

1. WENGI WAMEJIKUTA KATIKA MIKONO YA SHERIA BILA VIBALI MAALUM KUTOKA KWENYE VYAMA/TAASISI ZAO HUSIKA.
2. WENGI WAMEJIKUTA KATIKA MIKONO YA VYOMBO VYA DOLA WAKIPATIKANA WAKIFANYA AU KUJARIBU RAMLI CHONGANISHI KWENYE JAMII.
3. KUNA MIKOA WAKIJUA WEWE NI MSHIRIKINA AU MGANGA WA JADI UJUE MAISHA YAKO YAPO HATARINI.
4. KUNA WAGANGA WAMEJIKUTA WAKIISHI KAMA WAKIMBIZI KWENYE TAIFA LAO JUU YA MATUKIO YA UTAPELI YALIYOKITHIRI.
5. KUNA WAGANGA WANASOTEA JELA KUTOKANA NA MAUAJI YA VIFO WALIVYOTEKELEZA AU KUSHIRIKI. MF; ALBINO
6. KUNA WAGANGA HAWAPATI MAENDELEO KUTOKANA NA MUUNDO WAO WA KIMAISHA ALIOJIWEKEA NA PIA UNATOKANA UVIVU AMBAO UMEA WIVU/CHUKI NA MWISHOWE KUWA MCHAWI/MWANGA KABISA.

NB: STICK TO YOUR DREAMS OR AMBITIONS NA FURSA ZOTE SIO MAKINI KUNA ZINAZOPOTEZA AU KUKUPA MEMA ZAIDI. NISINUKULIWE VIBAYA KUWA UGANGA NI MBAYA AU SIO WA MAANA NA HESHIMU MILA NA DESTURI ZETU.
 
Kwakweli ata mimi nmefikiria awamu hii waganga wanapata hela sana
Maana kila mtu anahisi karogwa
Umeona dadake tufanye korabo mimi nakua mganga wew unakua jini mimi takua nakaa sebuleni wew unakaa chumbani chini tumechimba pipe imepita kutoka chumbani kuja sebuleni af tunaweka na mtungi pale pipe inapo tokea unakua unaongelea chumbani saut ya jini sasa inapita ikifika kwenye mtungi inatoa mwangwi zinakua sauti tatu tatu mbona fresh tu tunapiga pesa.
 
mjini mipango😀😀
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom