Fursa mbalimbali katika Sekta ya Bahari zenye kuingiza kipato kikubwa

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
5,064
12,889
Hizi ni fursa mbalimbali katika sekta ya bahari ambazo mtanzania yeyote anaweza akafanya au kuanzisha kampuni ya kutoa huduma hizi.

1. Clearing and Freight Fowarding
Hii huusisha kazi za kutoa mizigo bandarini kwa niaba ya mteja au kusafirisha nje ya nchi.

Ili kufungua kampuni hii inatakiwa uwe na cheti cha mambo ya forodha kutoka chuo cha kodi au unaweza ukamtumia mtu mwenye cheti hicho akufanyie mtihani ili upate kibali cha kufungua kampuni.

Angalizo;Hii inataka mtaji mkubwa kulingana na mizigo utayokuwa unatoa.
Maana katika kuendesha kampuni inatakiwa uwe na pesa Bank kama Bond kulingana na thamani ya mzigo ukiwa njiani kupelekwa nje ya nchi.

2.Cargo Consolidator and Denconsolidation
Hii inahusisha kazi za ukusanyaji mizigo ambayo itasafirishwa na meli au usafiri mwingine na kuiweka pamoja.
Mfano upo Dar umeletewa mizigo ya wateja 6 kutoka sehemu tofauti na inaenda Zanzibar.
Utaikusanya kwa kuifunga na kuiweka kwa pamoja vizuri kisha kuipakia kwenye kontena.

Pia kutenganisha mizigo mfano watu 4 waliagiza bidhaa kutoka China baada ya kontena kufika Dar. Wewe utapewa nyaraka za mzigo na utatenganisha bidhaa za hao wateja zilizo katika kontena hilo na kuhakiki idadi na usalama wa hizo bidhaa.

3.Ship Agency
Hii ni biashara ya kuwa agency wa meli.Wewe unakuwa kwa niaba ya mmiliki wa meli inapokuwa imefika katika bandari ya nchi uliyopo.

Majukumu yako ni kuandaa taarifa bandarini kwa ajili ya gati ya meli,mizigo iliyopo,manunuzi yoyote ya meli itapokuwa hapa.

Hii haiitaji uwe na taaluma hii ili ufungue kampuni ila kwa sasa Tanzania Shipping Agencies Corporation wanataka wafanyakazi wako wawe na taaluma ya ship agency.
Kuwa ship agency wa kampuni ya meli inategemea mkataba wako na wamiliki na unaweza ukawa unahudumu hata kwa makampuni mawili ya Shipping Line.

4. Ship Chandlering
Hizi ni kampuni za kutoa huduma mbalimbali kwa meli. Mfano kuwanunulia mahitaji kama chakula,vinywaji,mavazi,vifaa na spea.

Ukiwa na kampuni kama hii unapokea oda kutoka kwenye meli na kuchukua list na kuwanunulia hayo mahitaji kisha unapewa malipo yako.
Hii unalipa ada kwa kipindi cha mwaka kwa mamlaka ya bandari nadhani ni Usd 500.

5.Garbage Collector (Ukusanyaji taka kutoka melini).
Ukifungua kampuni kama hii unatakiwa uwalipe bandari (TPA) ada ya kutoa huduma hizo.

Hapa wewe ni kutafuta konection na ma agent wa meli au watu wa bandari. Meli inapokuwa njiani taka za plastic na vyakula hukusanywa hazitupwi baharini, hivyo wakifika bandarini hutafuta kampuni ya kutoa taka au wanaomba list ya kampuni zinazotoa huduma ambazo zimeruhusiwa hapo.

Wewe hautaji kuwa na gari la kuzoa taka ukipata email au simu inabidi ukodi gari na vijana hii mtaji ni pesa kidogo.

6.Kazi ya kuzoa mafuta machafu melini
Meli kubwa nyingi zinatumia mafuta mazito (Heavy oil/Fuel oil) baada ya matanki ya mafuta kubaki na mafuta machafu zaidi ambayo hayawezi kutumika tena.

Huwa yanatakiwa kumwagwa sasa kulingana na sheria za bahari ni maeneo machache sana meli hurusiwa kumwaga baharini na kwa kiasi huo uchafu wa mafuta.

Hivyo wengi huyamwaga wakifika bandarini kwa kuja kuvutwa na magari(Bozzer) kama yale ya kuvuta maji taka na kwenda kutupwa maeneo ya nchi kavu kwenye sewage plant.

Hii biashara inafaida kubwa maana haitaki mtaji mkubwa wala kumiliki gari la kubeba, gari hukodishwa na vijana wa nguvu kazi hulipwa kama vibarua.

Kwa watoto wa mjini walikuwa wakibeba mpaka mafuta masafi na kuyauza mtaani.Ila kwenye hayo mafuta kunakuwa na diesel chafu hii unaweza ukauza pia.

7. Kampuni ya kusafisha vyumba vya kubebea mizigo(Holds) na kupuliza dawa za wadudu.

Kazi za kusafisha vyumba vya kubebea mzigo hutolewa na meli endapo ina wafanyakazi wachache au Cargo inspector akakupa dili au akakataa usafishaji wa watu wa melini na kutaka watu wanao safisha waje.
Hii unatafuta vijana na vifaa vya kusafisha vyumba vya kubebea mizigo melini.

Kazi ya kupuliza wadudu.
Meli ikifika bandarini haitakiwi wadudu au wanyama kama panya au mende watoke melini waje nchi kavu au nchi kavu waende melini.

Baada ya watu wa afya au bandari kukagua au kuona wadudu inabidi meli ipuliziwe sawa na iwekewa mitego ya kuzuia panya wasije nchi kavu au melini.

Hivyo ukiwa na kampuni ya kupuliza dawa za wadudu unaweza ukawa unatoa huduma bandarini.

8. Kazi ya kulinda meli ikiwa nangani (Watch guard)
Hii unatakiwa uwe na kampuni au unaweza ukaomba kazi za kulinda meli ikiwa nangani au nje ya bandari.

Wengi wanatafuta vijana na kuwapa kazi ya kulinda pale nangani. Maana kipindi cha nyuma vijana walikuwa wanasogea na boti na kuzamia melini kisha kuiba vitu au kuwapora wafanyakazi wa meli. Meli za kiraia nyingi huwa hazina mlinzi ni mabaharia wanapeana zamu kukaa katika njia ya kuingia melini (Gangway).

Pia mwenye kampuni ya ulinzi anaweza akaomba kazi hizi kwa agent wa meli au nahodha akihitaji huduma anapohofia usalama wa meli ikiwa pale nje.
Makadirio kwa mtu kulinda huwa ni Usd 100, ila huyu mlindaji hupewa kiasi kama Tsh 20,000.

9.Kubeba sihala zilizo melini na kuzipeleka sehemu ya kutunzia meli ikija nchini.

Kutokana na matukia ya uharamia na ugaidi baadhi ya meli kutoka nchi nyingine hubeba silaha melini au askari wenye silaha wanaolinda meli ikiwa safarini.

Hivyo hiyo meli ikiingia Tanzania kutokana na sheria zetu watatakiwa wakabidhi hizo silaha na kuchukuliwa na kampuni kisha kupelekwa kutunzwa kwenye kambi ya jeshi-Amala (Armour) na siku meli inapoondoka hukabidhiwa silaha zao.

Ukiwa na kampuni kama hii wewe inabidi upate vijana wenye mafunzo ya Jkt au Mgambo wenye uelewa na tahadhari na silaha.
Kampuni ikiwa imesajiliwa na inajulikana na bandari meli yenye silaha ikifika wao watapewa mawasiliano ya kampuni hizi na kukutafuta kwa kazi.

Angalizo: Hizi ni meli za kawaida si za kijeshi. Kuna meli zinabeba silaha kwa matumizi ya kukabiliana na uovu baharini au wanakuwa na walinzi wenye silaha kutoka nchini kwao.

Hii pia haiitaji mtaji mkubwa wala ofisi kubwa.

10.Kutoa huduma za kubeba mabaharia na kupeleka mahitaji melini kwa boti.

Unatakiwa uwe na boti ndogo ambayo utakuwa ukiwabeba mabaharia wa meli ikiwa pale nje nangani kuwapeleka nchi kavu wanapokuwa wanataka mahitaji yao kama starehe,kwenda supermarket au kuja kutembea nchi kavu.

Pia mahitaji kama vyakula na vinywaji vikinunuliwa boti yako itakodiwa uwapelekee vitu vyao pale nangani.
Malipo huwa ni kwa mtu au trip.

Hapa mtaji ni boti ndogo yenye injini, kuisajili boti na ada ya kuipaki boti yako ikija bandarini hii ada ulipwa kwa mwaka haizidi laki moja.

Tanzania fursa za baharini bado nyingi, bahari ni mgodi usio na kikomo.

"SEA NEVER DRY"
 
Hz fursa n nzuri sana.....hasa hasa hyo ya kununua chakula na kuwauzia,,, mana ww unanunua bei chn waenda kuuza bei juu

je hvi vyakula vinakuwa ni cooked food mfano wali au raw food mfano mchele
 
Ungekuwa mbele yangu ningekunasa kibao siku zote ulikuwa wapi anyway sio kesi embu chukua mirinda kubwa nakuja hapo
 
Hz fursa n nzuri sana.....hasa hasa hyo ya kununua chakula na kuwauzia,,, mana ww unanunua bei chn waenda kuuza bei juu

je hvi vyakula vinakuwa ni cooked food mfano wali au raw food mfano mchele
Vyakula ambavyo havijapikwa kama mchele,mafuta na nyama au wanyama walio hai kama mbuzi,ng'ombe na kuku kisha wao wataenda kuwachinja.
 
mkuu hv fursa namba 2,4,6 zinahitaji minimum capital kias gan mana nmekuta narudia rudia sana kusoma huu uzi
 
Hizi ni fursa mbalimbali katika sekta ya bahari ambazo mtanzania yeyote anaweza akafanya au kuanzisha kampuni ya kutoa huduma hizi.

1. Clearing and Freight Fowarding
Hii huusisha kazi za kutoa mizigo bandarini kwa niaba ya mteja au kusafirisha nje ya nchi.

Ili kufungua kampuni hii inatakiwa uwe na cheti cha mambo ya forodha kutoka chuo cha kodi au unaweza ukamtumia mtu mwenye cheti hicho akufanyie mtihani ili upate kibali cha kufungua kampuni.

Angalizo;Hii inataka mtaji mkubwa kulingana na mizigo utayokuwa unatoa.
Maana katika kuendesha kampuni inatakiwa uwe na pesa Bank kama Bond kulingana na thamani ya mzigo ukiwa njiani kupelekwa nje ya nchi.

2.Cargo Consolidator and Denconsolidation
Hii inahusisha kazi za ukusanyaji mizigo ambayo itasafirishwa na meli au usafiri mwingine na kuiweka pamoja.
Mfano upo Dar umeletewa mizigo ya wateja 6 kutoka sehemu tofauti na inaenda Zanzibar.
Utaikusanya kwa kuifunga na kuiweka kwa pamoja vizuri kisha kuipakia kwenye kontena.

Pia kutenganisha mizigo mfano watu 4 waliagiza bidhaa kutoka China baada ya kontena kufika Dar. Wewe utapewa nyaraka za mzigo na utatenganisha bidhaa za hao wateja zilizo katika kontena hilo na kuhakiki idadi na usalama wa hizo bidhaa.

3.Ship Agency
Hii ni biashara ya kuwa agency wa meli.Wewe unakuwa kwa niaba ya mmiliki wa meli inapokuwa imefika katika bandari ya nchi uliyopo.

Majukumu yako ni kuandaa taarifa bandarini kwa ajili ya gati ya meli,mizigo iliyopo,manunuzi yoyote ya meli itapokuwa hapa.

Hii haiitaji uwe na taaluma hii ili ufungue kampuni ila kwa sasa Tanzania Shipping Agencies Corporation wanataka wafanyakazi wako wawe na taaluma ya ship agency.
Kuwa ship agency wa kampuni ya meli inategemea mkataba wako na wamiliki na unaweza ukawa unahudumu hata kwa makampuni mawili ya Shipping Line.

4. Ship Chandlering
Hizi ni kampuni za kutoa huduma mbalimbali kwa meli. Mfano kuwanunulia mahitaji kama chakula,vinywaji,mavazi,vifaa na spea.

Ukiwa na kampuni kama hii unapokea oda kutoka kwenye meli na kuchukua list na kuwanunulia hayo mahitaji kisha unapewa malipo yako.
Hii unalipa ada kwa kipindi cha mwaka kwa mamlaka ya bandari nadhani ni Usd 500.

5.Garbage Collector (Ukusanyaji taka kutoka melini).
Ukifungua kampuni kama hii unatakiwa uwalipe bandari (TPA) ada ya kutoa huduma hizo.

Hapa wewe ni kutafuta konection na ma agent wa meli au watu wa bandari. Meli inapokuwa njiani taka za plastic na vyakula hukusanywa hazitupwi baharini, hivyo wakifika bandarini hutafuta kampuni ya kutoa taka au wanaomba list ya kampuni zinazotoa huduma ambazo zimeruhusiwa hapo.

Wewe hautaji kuwa na gari la kuzoa taka ukipata email au simu inabidi ukodi gari na vijana hii mtaji ni pesa kidogo.

6.Kazi ya kuzoa mafuta machafu melini
Meli kubwa nyingi zinatumia mafuta mazito (Heavy oil/Fuel oil) baada ya matanki ya mafuta kubaki na mafuta machafu zaidi ambayo hayawezi kutumika tena.

Huwa yanatakiwa kumwagwa sasa kulingana na sheria za bahari ni maeneo machache sana meli hurusiwa kumwaga baharini na kwa kiasi huo uchafu wa mafuta.

Hivyo wengi huyamwaga wakifika bandarini kwa kuja kuvutwa na magari(Bozzer) kama yale ya kuvuta maji taka na kwenda kutupwa maeneo ya nchi kavu kwenye sewage plant.

Hii biashara inafaida kubwa maana haitaki mtaji mkubwa wala kumiliki gari la kubeba, gari hukodishwa na vijana wa nguvu kazi hulipwa kama vibarua.

Kwa watoto wa mjini walikuwa wakibeba mpaka mafuta masafi na kuyauza mtaani.Ila kwenye hayo mafuta kunakuwa na diesel chafu hii unaweza ukauza pia.

7. Kampuni ya kusafisha vyumba vya kubebea mizigo(Holds) na kupuliza dawa za wadudu.

Kazi za kusafisha vyumba vya kubebea mzigo hutolewa na meli endapo ina wafanyakazi wachache au Cargo inspector akakupa dili au akakataa usafishaji wa watu wa melini na kutaka watu wanao safisha waje.
Hii unatafuta vijana na vifaa vya kusafisha vyumba vya kubebea mizigo melini.

Kazi ya kupuliza wadudu.
Meli ikifika bandarini haitakiwi wadudu au wanyama kama panya au mende watoke melini waje nchi kavu au nchi kavu waende melini.

Baada ya watu wa afya au bandari kukagua au kuona wadudu inabidi meli ipuliziwe sawa na iwekewa mitego ya kuzuia panya wasije nchi kavu au melini.

Hivyo ukiwa na kampuni ya kupuliza dawa za wadudu unaweza ukawa unatoa huduma bandarini.

8. Kazi ya kulinda meli ikiwa nangani (Watch guard)
Hii unatakiwa uwe na kampuni au unaweza ukaomba kazi za kulinda meli ikiwa nangani au nje ya bandari.

Wengi wanatafuta vijana na kuwapa kazi ya kulinda pale nangani. Maana kipindi cha nyuma vijana walikuwa wanasogea na boti na kuzamia melini kisha kuiba vitu au kuwapora wafanyakazi wa meli. Meli za kiraia nyingi huwa hazina mlinzi ni mabaharia wanapeana zamu kukaa katika njia ya kuingia melini (Gangway).

Pia mwenye kampuni ya ulinzi anaweza akaomba kazi hizi kwa agent wa meli au nahodha akihitaji huduma anapohofia usalama wa meli ikiwa pale nje.
Makadirio kwa mtu kulinda huwa ni Usd 100, ila huyu mlindaji hupewa kiasi kama Tsh 20,000.

9.Kubeba sihala zilizo melini na kuzipeleka sehemu ya kutunzia meli ikija nchini.

Kutokana na matukia ya uharamia na ugaidi baadhi ya meli kutoka nchi nyingine hubeba silaha melini au askari wenye silaha wanaolinda meli ikiwa safarini.

Hivyo hiyo meli ikiingia Tanzania kutokana na sheria zetu watatakiwa wakabidhi hizo silaha na kuchukuliwa na kampuni kisha kupelekwa kutunzwa kwenye kambi ya jeshi-Amala (Armour) na siku meli inapoondoka hukabidhiwa silaha zao.

Ukiwa na kampuni kama hii wewe inabidi upate vijana wenye mafunzo ya Jkt au Mgambo wenye uelewa na tahadhari na silaha.
Kampuni ikiwa imesajiliwa na inajulikana na bandari meli yenye silaha ikifika wao watapewa mawasiliano ya kampuni hizi na kukutafuta kwa kazi.

Angalizo: Hizi ni meli za kawaida si za kijeshi. Kuna meli zinabeba silaha kwa matumizi ya kukabiliana na uovu baharini au wanakuwa na walinzi wenye silaha kutoka nchini kwao.

Hii pia haiitaji mtaji mkubwa wala ofisi kubwa.

10.Kutoa huduma za kubeba mabaharia na kupeleka mahitaji melini kwa boti.

Unatakiwa uwe na boti ndogo ambayo utakuwa ukiwabeba mabaharia wa meli ikiwa pale nje nangani kuwapeleka nchi kavu wanapokuwa wanataka mahitaji yao kama starehe,kwenda supermarket au kuja kutembea nchi kavu.

Pia mahitaji kama vyakula na vinywaji vikinunuliwa boti yako itakodiwa uwapelekee vitu vyao pale nangani.
Malipo huwa ni kwa mtu au trip.

Hapa mtaji ni boti ndogo yenye injini, kuisajili boti na ada ya kuipaki boti yako ikija bandarini hii ada ulipwa kwa mwaka haizidi laki moja.

Tanzania fursa za baharini bado nyingi, bahari ni mgodi usio na kikomo.

"SEA NEVER DRY"
Asante sana ..nitazichukua hizo
 
Hiyo biashara ya kutoa mafuta machafu watu wanapiga sana pesa.

Pia hawatoi taarifa ya hizi biashara wengi huishia kusema nina kampuni yangu bandarini.
Mkuu hii fursa inahitaji uwe na gari,vipi mtaji wake kiasi gani ukitaka kuomba hii tena kuna vibali vyovyote wanataka?au vyeti vya kusomea?
 
Haihitaji kuwa na gari wala kusomea.
Wewe unachotakiwa ni kufungua kampuni au jina la biashara na kulipa TPA ada kwa mwaka unapotoa huduma hii.

Baada ya hapo unakuwa tayari kuomba tenda za kufanya hizo kazi au kampuni yako inakuwa imeorozeshwa kama mtoa huduma wa kutoa mafuta machafu melini.Basi utakuwa ukitafutwa kupitia namba zako au kuwa na connection na watu wa karibu wanaohudumu pale ikitokea kazi hiyo wanakuita haraka.
 
Back
Top Bottom