Fursa kwa wasanii wa Tanzania ya kufanya kazi na Akon

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
12,813
18,145
Boomplay na Hitlab wametangaza Shindano la kuvumbua vipaji kidijitali kwa wasanii Chipukizi linalomshirikisha nyota wa muziki wa Marekani mwenye asili ya Senagali, Akon. Dar es Salaam, Tanzania, Mei 26, 2021. Boomplay na Hitlab wameungana kuwawezesha wasanii chipukizi kufanya kazi na nyota wa muziki mwenye tuzo nyingi kimataifa wa Marekani mwenye asili ya Senegali, Akon.

WhatsApp-Image-2021-05-26-at-14.55.39.jpeg


Mashindano hayo ya kwanza na ya aina yake barani Afrika yanatoa fursa ya kurekodi na kufanya kazi na lebo ya muziki Kimataifa, kutumbuiza kwenye majukwaa ya kimataifa, kuwa chini ya uangalizi wa msanii Akon pamoja na zawadi nyingine mbalimbali.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari, Meneja Mkuu wa Boomplay nchini Tanzania, Natasha Stambuli alisema “Hii ni hatua muhimu kwetu katika kufanikisha azma yetu ya kukuza wigo wa muziki wa Kiafrika na tunafurahi sana kuhusu fursa ambazo ushirikiano huu wa kimkakati utakavyowasaidia wasanii wetu wanaochipukia wa Kitanzania”.

Shindano la kuvumbua vipaji kidijitali kwa wasanii Chipukizi (DEAS) ni Shindano la kwanza la kimataifa kwa wasanii chipukizi litakaloendeshwa kidijitali pekee.


Wasanii wanaweza kuwasilisha nyimbo zao kwa ajili ya uchambuzi kupitia mfumo wa teknolojia mbadala wa Hitlab, Digital Nuance Analysis (DNA) technology, ambayo inapanga kwa viwango nyimbo zilizowasilishwa, kuonesha uwezo katika soko la kimataifa. Miongoni mwa vitu vinavyozingatiwa kidijitali baada ya utengenezaji wa nyimbo ni pamoja na mdundo (beat) na ukamalishaji wa nyimbo (mastering).

Ili kuwasilisha nyimbo, kwa msanii ambaye yupo tayari anapaswa kuchangia shilingi za Kitanzania 2,296 ($0.99) kwa wimbo mmoja, shilingi 9,254 ($3.99) kwa nyimbo tano 5 na shilingi 23,169($ 9.99) kwa nyimbo 15.

Unachopaswa kufanya ni kuwasilisha nyimbo zako kupitia ‘link’ ifuatayo Hitlab.com DEAS | DIGITAL EMERGING ARTIST SHOWCASE. Mara baada ya kuwasilisha nyimbo, itatokea chati inayopanga ubora wa nyimbo na msanii kupewa alama muda huo huo. Nyimbo ni lazima ziwe na ubora na vigezo vya kupita zaidi ya alama 49 kwenye mfumo wa kidijitali wa DEAS.
Shindano hili litaendeshwa hadi Oktoba 20, 2021. Baada ya hapo washindi watatangazwa.
# # #

Taarifa kwa Wahariri

Kuhusu Boomplay
Boomplay, ni App inayoongoza kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki kupitia Transsnet Music Limited. Kampuni ina ofisi Tanzania, Kenya, Ghana na Nigeria. App hii inapatikana duniani kote kupitia programu tumishi ya Android na iOS na katika tovuti ya www.boomplay.com
Tangu Machi, 2021, Boomplay imekua na zaidi ya watumiaji milioni 50 huku ikiwa na zaidi ya nyimbo milioni 50.

Kuhusu HITLAB (A Digital and Media Entertainment Company)
HITLAB ni kampuni ya masuala ya habari kidigitali na kampuni ya burudani ambayo imebeba mageuzi makubwa ya kiugunduzi, uzalishaji na kuwasilisha kwa wa walaji burudani ya uhakika.

Ikiwa inatumia teknolojia ya hakimiliki ya AI na programu ya ubunifu iliyoundwa katika kuunganisha, kushiriki na kuunda mwingiliano wenye nguvu kati ya watumiaji na chapa.

Kampuni hii ina mahusiano mazuri ya kitaifa na Kimataifa na wataalamu wa ubunifu, kampuni za kurekodi, wachapishaji, watendaji, watayarishaji, mameneja, vituo vya habari, kumbi na watangazaji.

Kwa mawasiliano: –
Harrison Lwanga
Meneja Uhusiano Boomplay Tanzania
harrison.lwanga@transsnet.com
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom